Rais Samia ni dereva hodari, shupavu jasiri na mahiri wa taifa letu, Watanzania waridhishwa na kasi yake

Chief usijitoe ufahamu kwa ajili ya tumbo lako kwa tamaa za uteuzi.
Wewe na familia yako hamuwakilishi taifa zima.
Kama kipimo cha kujenga nchi ni kufanya kila kitu kuwa kigumu basi kwa hakika amefanikiwa.
Ndani ya nafsi unajua fika kuwa han dira wala muelekeo ila kwa vile umesikia kasema anataka kila mtu asupport maono yako (yasiyokuwepo) basi na wewe umejitoa ufahamu kusifia visivyokuwepo.
Umeweka jina na namba ya simu kwa matumaini kuwa atakutafuta. Sasa kwa taarifa yako watakaotufuta ni wazee wa tuma kwa namba hii na matangazo ya waganga wa kienyeji pekee.
 
Hizi porojo za kiccm ni toka enzi za Nyerere na hali inazidi kuwa mbaya, udhibitisho ni huu mgao wa umeme na maji.
Tambua kuwa Hata idadi yetu inaongezeka kila Siku na kila mwaka hivyo Mahitaji nayo lazima yaongezeke na kupelekea kuongezeka kwa baadhi ya changamoto ambazo serikali yetu inakuwa inapambana nazo kuzimaliza, embu fikria kuwa tulipokuwa tunapata Uhuru tulikuwa millini 12 na point lakini Leo hii tupo million 61 na laki Saba, je huoni kuwa hata changamoto lazima ziongezeka kulingana na mahitaji ya watu kuongezeka
 
Nawewe ni mkulima au WEWE mlamba asari?
 
Huo Ni mtizamo wako tu mkuu, lakini Tambua kuwa mioyo ya wakulima wa Tanzania kwa Sasa Ina amani Sana na Rais Samia
Wazungu wanasema picha inaongea maneno buku hao wakulima na mabango yao hawaonekani kama watu wenye amani mioyoni mwao kwani hata kupauka wamepauka wanaisoma namba hawawezi kusmile.
 
Rais wetu anamuelekeo na dira inayoeleweka katika kuliongoza taifa hili,anafahamu wapi tumetoka na wapi tunapaswa kuelekea, anafahamu Mahitaji ya watanzania ,Anayo mikakati ya kuhakikisha kero mbalimbali zinamalizwa na kuleta mwanga katika maisha ya watanzania
 
Wazungu wanasema picha inaongea maneno buku hao wakulima na mabango yao hawaonekani kama watu wenye amani mioyoni mwao kwani hata kupauka wamepauka wanaisoma namba hawawezi kusmile.
Wanamatumaini ya kesho yao kuwa njema kwa kuwa wanatambua mikakati ya serikali yao kuwainua kiuchumi kupitia kilimo na kauli mbiu ya kilimo Ni biashara,ambapo kwa Sasa kilimo Ni biashara inayolipa na inayotoa matumaini kwa wakulima wengi kujikwamua kiuchumi
 
Siku zote kipimo cha uanaume wa mtu ni uwezo wa kulinda utu wake hata ikiwa hana kitu.
Wewe kwa tamaa ya teuzi unautoa utu wako kwa kuhubiri vitu ambavyo hata kipofu anaviona.
Ukute una dhiki mpaka kwenye unyayo (kupelekea kutarajia teuzi kuwa pona yako) halafu uko hapa unaandika upuuzi ili tu uonekane na mtu ambae hatokuja kukaa akakuona.
Muda unaotumia kuandika huu upuuzi bora hata ungekaa kutafakari njia za kujikwamua kimaisha.
 
Embu rudia kusoma halafu uniambie mahali nilipozungumzia habari za uteuzi
 
Mimi Ni mkulima ambapo jembe langu ndio kalamu yangu na Shamba langu ndio daftari langu huku mabega yangu yakiwa ndio begi langu kubebwa jembe langu
Lini unaandamana kumpongeza mama tozo Kwa kuweka tozo mpaka Kwa wanawake wa kimboka?
 
Unaweza kukuta huyu mtoa mada ni baba wa familia na anategemewa kuiongoza familia yake na kuwapa ushauri........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…