Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,199
- 7,562
Kwanza nianze kwa kusema, hata mtu awe mwema au mtaalam wa kiwango gani, hawezi kutatua matatizo yote ya dunia hii peke yake. Anachotakiwa ni kufanya kwa nafasi yake akitanguliza dhamira njema na sisi wengine kila mtu afanye kwa uwezo wake na nafasi yake.
Aidha, kwa kadiri wengi wetu tunavyochukua hatua sahihi kulingana na mazingira yetu na uwezo wetu, ndivyo uwezekano wa kufanikiwa kutatua matatizo yanayotuzunguka unavyoongezeka na kinyume chake.
Rais Samia ni kiongozi muadilifu aliejaa hekima anayeongoza nchi kisayansi na kwa dhamira njema.
Kwenye uchumi: Anajitahidi sana kuifungua nchi kiuchumi na kuiunganisha na dunia, ambapo kwa sasa hii ni muhimu sana ili kufanikiwa kiuchumi. Ikumbukwe kuwa hata China ilipata maendeleo ya haraka baada ya Deng Xiaoping na succesors wake kuifungua China kwa Dunia na kuyaalika makampuni makubwa kuwekeza huko ShenzHen na Shaghai.Sasa mtu anachukia kwa hili unataka nini sasa?
Kisiasa: Ni mtu anayeamini kwenye siasa za mazungumzo, majadiliano na maridhiano na tayari tunaona reforms anazofanya. Sasa mtu anachukiaje kwa aina hii ya siasa?
Kijamii: Ni mtu anayeamini kwenye haki, na tumeona reforms anazofanya ambazo ziko wazi sana. Sasa mtu unachukiaje kwa mfano mama akipinga dhulma?
Swali: sasa kwa nini maisha bado ni magumu? bado kuna haki za kisiasa hazipo sawa? bado kuna watu wanadhulumiwa hapa na pale? Jibu ni kwamba, matatizo hayatatuliwi yote siku moja ukiamka asubuhi yameisha. Ni mchakato. Aidha, kuna 'actors' wengi ambapo kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu wake ili kupata mafanikio ya maana kama Taifa.
Katika mazingira kama hayo, ni sahihi mtu kuhitmisha kuwa anayemchukia Rais Samia ni amma ana tatizo la husuda, au ni mtu dhalimu au ana roho ya uchawi ambapo wachawi hawapendagi vitu positive.