Rais Samia ni Nuru na Mwanga wa Taifa letu na watanzania wote kwa ujumla wake

Sasa kama kila mtu anajua hicho unachosema unamwambia nani asiyejua ? Hii si ni kutumia rasilimali muda vibaya ?

Au ndio yale ya wahenga ya kibaya chajiuza ?
 
Labda kwa mashoga na wasagaji
Hata huu uhuru ulionao wewe wa kuandika utakacho ni kwa sababuya nuru na Mwanga aliouleta Rais Samia. Usingeweza kuandika hivyo Kabla ya Rais Samia kukaa kitini
 
Rais Samia ni chaguo la Mungu Mwenyewe na aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu. Mungu ndiye amemleta na kumuinua Rais Samia kuongoza Taifa letu kwa makusudi maalumu.
Kwanza SAMIA alishajua siku nyingi kwamba ww ni dishi ambalo hata kuchallenge haliwezi ila linasifu tu kama kasuku.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika Huyu Mama Mwenye moyo wa Upendo,huruma, Ukarimu, Unyenyekevu, Uzalendo na Moyo wa kujitoa na kujitolea Maisha yake kwa ajili ya kuwatumikia watanzania katika kuleta matumaini na tabasamu kwa watu wote.

Amekuwa ni nuru na Mwanga wa Taifa letu katika mioyo ya mamilioni ya watanzania. Kila mmoja anaona mwanga mbele ya Uso wake, kila mmoja anaona tumaini machoni pake ,Maisha ya watanzania yamejaa matumaini na Mwanga wa kesho iliyo bora zaidi . Kila kundi na kila rika linaona unafuu wa Maisha kwa siku ya kesho.

Rais Samia amefanyika kama Baraka na Neema katika maisha ya watu. Mikono yake imekuwa kwa ajili ya kuwainua watu, kuwashika mikono watu walioanguka, . Macho yake Yamekuwa yenye huruma kwa maisha ya watu. Hayupo Tayari kuona mtanzania akiteseka katika nchi yake,hayupo tayari kuona macho yake yakiona mtu mbele yake akionewa,kunyanyaswa,kukandamizwa,kuzurumiwa au kunyonywa .

Ni Mama mpenda haki na mtenda haki kutokana na kuwa na Mungu ndani yake. Ndio sababu ya kuona nyuso za watanzania zikiwa zimejawa furaha na tabasamu wakati wote. Huoni watu wakizungumza wenyewe mabarabarani kama vichaa au wendawazimu.

Ifahamike ya kuwa mkuu wa Nchi anaweza kuweka giza katika maisha ya watu, anaweza fanya watu wakawa wanajuta kuzaliwa ndani ya nchi husika,anaweza fanya watu wakakata tamaa na kupoteza Matumaini kila uchao, kutoona tumaini mbele yao,kuona ya jana ni bora kuliko ya leo. Kuona wanaishi kama wapo jehanamu na kutokuwa na uhakika wa kuiona kesho yao wakiwa wazima na wenye kupumua.

Hii hutokea pale aliyekalia kiti anapokuwa Dikteta ,katili na Asiyejali wala kuguswa na hali mbaya za watu wake. Taifa linakuwa linakuwa ni kama limefiwa au lipo katika maombolezo muda wote.kwa kuwa mioyo ya watu inakuwa ina huzuni na kukosa amani na furaha muda wote. Watu wanakuwa hawana mfariji wala wa kuwatia moyo kwa sababu aliyepo kitini hana hisia za upendo wala huruma wala kujali wala kuguswa na hivyo kufanya mambo na kuchukua hatua za kuwaumiza watu na kuleta mateso katika maisha ya watu. Kutoa lugha na maneno yenye kuchoma mioyo ya watu na kuwakatisha Tamaa.

Lakini Rais Samia Amekaa kitini na kuwa kama nyota ya asubuhi iletayo Matumaini ya Mapambazuko na kuondoka kwa giza .Mama Samia kwa hakika ni chaguo la Mungu aliyeinuliwa na Mungu Mwenyewe kuliongoza Taifa letu.View attachment 3307130View attachment 3307136View attachment 3307140

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Nuru na mwanga wa Taifa letu ni Mungu muumba wa mbingu na nchi , na elewa Mungu hachangii utukufu wake na wanadamu.
 
Rais Samia ni chaguo la Mungu Mwenyewe na aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu. Mungu ndiye amemleta na kumuinua Rais Samia kuongoza Taifa letu kwa makusudi maalumu.
Kwa hiyo akiwa chaguo la Mungu ndo anakuwa nuru kwako au mwanga kwako??? Unajua maana ya maneno hayo???? Usimfanye mwanadamu kuwa mungu wako sababu ya vihela ndugu yako! Acha kukufuru wewe! Mungu hafananishwi na mwanadamu wala hashei utukufu na mwanadamu! Ukiwa ccm sijui unarukwa na akili???? Lukas unapoelekea utaokota makopo utapigwa na laana!
 
Kwanza SAMIA alishajua siku nyingi kwamba ww ni dishi ambalo hata kuchallenge haliwezi ila linasifu tu kama kasuku.
Ukweli utabikia kuwa ukweli tu . Hata kama utaupiga kwa nyundo huwezi kubadilisha ukweli kuwa uongo
 
Kwa hiyo akiwa chaguo la Mungu ndo anakuwa nuru kwako au mwanga kwako??? Unajua maana ya maneno hayo???? Usimfanye mwanadamu kuwa mungu wako sababu ya vihela ndugu yako! Acha kukufuru wewe! Mungu hafananishwi na mwanadamu wala hashei utukufu na mwanadamu! Ukiwa ccm sijui unarukwa na akili???? Lukas unapoelekea utaokota makopo utapigwa na laana!
Embu angalia namna watu walivyokuwa na furaha na matumaini wakati huu wa Mama. Embu angalia namna maisha ya watanzania yalivyojaa Matumaini. Angalia watu wanavyoishi kwa amani na utulivu pasipo hofu wala uoga.
 
Toa neno Nuru na mwanga maana hayo hutolewa na MUNGU MWENYEZI MWENYEWE.
Mungu ndiye aliyemuinua Rais wetu kwa mkono wake. Ndio maana huwezi kupambana na kushindana na Rais Samia .ndio maana unaona Taifa limejaa baraka na neema kwa kila kitu.
 
Ukweli utabikia kuwa ukweli tu . Hata kama utaupiga kwa nyundo huwezi kubadilisha ukweli kuwa uongo
Ww ni dishi nashukuru umekubali na ukweli utabaki kuwa ukweli tu hata kama utaupiga kwa nyundo huwezi kubadikisha ukweli kuwa uongo.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika Huyu Mama Mwenye moyo wa Upendo,huruma, Ukarimu, Unyenyekevu, Uzalendo na Moyo wa kujitoa na kujitolea Maisha yake kwa ajili ya kuwatumikia watanzania katika kuleta matumaini na tabasamu kwa watu wote.

Amekuwa ni nuru na Mwanga wa Taifa letu katika mioyo ya mamilioni ya watanzania. Kila mmoja anaona mwanga mbele ya Uso wake, kila mmoja anaona tumaini machoni pake ,Maisha ya watanzania yamejaa matumaini na Mwanga wa kesho iliyo bora zaidi . Kila kundi na kila rika linaona unafuu wa Maisha kwa siku ya kesho.

Rais Samia amefanyika kama Baraka na Neema katika maisha ya watu. Mikono yake imekuwa kwa ajili ya kuwainua watu, kuwashika mikono watu walioanguka, . Macho yake Yamekuwa yenye huruma kwa maisha ya watu. Hayupo Tayari kuona mtanzania akiteseka katika nchi yake,hayupo tayari kuona macho yake yakiona mtu mbele yake akionewa,kunyanyaswa,kukandamizwa,kuzurumiwa au kunyonywa .

Ni Mama mpenda haki na mtenda haki kutokana na kuwa na Mungu ndani yake. Ndio sababu ya kuona nyuso za watanzania zikiwa zimejawa furaha na tabasamu wakati wote. Huoni watu wakizungumza wenyewe mabarabarani kama vichaa au wendawazimu.

Ifahamike ya kuwa mkuu wa Nchi anaweza kuweka giza katika maisha ya watu, anaweza fanya watu wakawa wanajuta kuzaliwa ndani ya nchi husika,anaweza fanya watu wakakata tamaa na kupoteza Matumaini kila uchao, kutoona tumaini mbele yao,kuona ya jana ni bora kuliko ya leo. Kuona wanaishi kama wapo jehanamu na kutokuwa na uhakika wa kuiona kesho yao wakiwa wazima na wenye kupumua.

Hii hutokea pale aliyekalia kiti anapokuwa Dikteta ,katili na Asiyejali wala kuguswa na hali mbaya za watu wake. Taifa linakuwa linakuwa ni kama limefiwa au lipo katika maombolezo muda wote.kwa kuwa mioyo ya watu inakuwa ina huzuni na kukosa amani na furaha muda wote. Watu wanakuwa hawana mfariji wala wa kuwatia moyo kwa sababu aliyepo kitini hana hisia za upendo wala huruma wala kujali wala kuguswa na hivyo kufanya mambo na kuchukua hatua za kuwaumiza watu na kuleta mateso katika maisha ya watu. Kutoa lugha na maneno yenye kuchoma mioyo ya watu na kuwakatisha Tamaa.

Lakini Rais Samia Amekaa kitini na kuwa kama nyota ya asubuhi iletayo Matumaini ya Mapambazuko na kuondoka kwa giza .Mama Samia kwa hakika ni chaguo la Mungu aliyeinuliwa na Mungu Mwenyewe kuliongoza Taifa letu.View attachment 3307130View attachment 3307136View attachment 3307140

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Hizi sifa zinafanana na za Kim Jong Un.
 
Mungu ndiye aliyemuinua Rais wetu kwa mkono wake. Ndio maana huwezi kupambana na kushindana na Rais Samia .ndio maana unaona Taifa limejaa baraka na neema kwa kila kitu.
Usiseme SAMIA ni Nuru na mwanga wetu utalaaniwa kijana na utapotezewa uwezo hata huo kidogo ulionao na hauta changia kitu hapa jamii forum,ujinga wenu ule ule wa kusema eti MUNGU amshukuru Magifuli bado mnaendeleza na kwa mama yenu shauri yenu mtapata mnacho kitafuta soon.
 
Huruma???.
"Kifo cha Kibao ni hali ya kawaida".
"wanaotekwa ni drama tu " hata Soka na wenzake?
Lissu akishindwa kesi jukumu ni kunyongwa mpaka kufa. nk.
Hivi Lucas Mwashambwa una akili timamu?
Hao akina lissu na hata lema wasingeweza kurejea Nchini kama siyo upendo na huruma iliyojaa katika moyo wa Mama yetu Mpendwa kipenzi cha watanzania.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika Huyu Mama Mwenye moyo wa Upendo,huruma, Ukarimu, Unyenyekevu, Uzalendo na Moyo wa kujitoa na kujitolea Maisha yake kwa ajili ya kuwatumikia watanzania katika kuleta matumaini na tabasamu kwa watu wote.

Amekuwa ni nuru na Mwanga wa Taifa letu katika mioyo ya mamilioni ya watanzania. Kila mmoja anaona mwanga mbele ya Uso wake, kila mmoja anaona tumaini machoni pake ,Maisha ya watanzania yamejaa matumaini na Mwanga wa kesho iliyo bora zaidi . Kila kundi na kila rika linaona unafuu wa Maisha kwa siku ya kesho.

Rais Samia amefanyika kama Baraka na Neema katika maisha ya watu. Mikono yake imekuwa kwa ajili ya kuwainua watu, kuwashika mikono watu walioanguka, . Macho yake Yamekuwa yenye huruma kwa maisha ya watu. Hayupo Tayari kuona mtanzania akiteseka katika nchi yake,hayupo tayari kuona macho yake yakiona mtu mbele yake akionewa,kunyanyaswa,kukandamizwa,kuzurumiwa au kunyonywa .

Ni Mama mpenda haki na mtenda haki kutokana na kuwa na Mungu ndani yake. Ndio sababu ya kuona nyuso za watanzania zikiwa zimejawa furaha na tabasamu wakati wote. Huoni watu wakizungumza wenyewe mabarabarani kama vichaa au wendawazimu.

Mama yetu akisimama kuzungumza na kufungua kinywa na mdomo wake unaona akitoa maneno ya kuwapa na kuwajaza matumaini hai watu juu ya kesho iliyo njema. Huoni wala kumsikia Mama yetu kipenzi akiwatia na kuwajaza hofu au uoga watu wala kuwakatisha Tamaa wala kuwatisha . Ni Mama mwenye kuonyesha na kuongoza njia yenye matumaini na kuonyesha watu ni vipi tutafika huko tuendako. Ndio maana watu wana imani na safari ya Mama yetu na wapo tayari kumfuata na kusafiri naye.

Ifahamike ya kuwa mkuu wa Nchi anaweza kuweka giza katika maisha ya watu, anaweza fanya watu wakawa wanajuta kuzaliwa ndani ya nchi husika,anaweza fanya watu wakakata tamaa na kupoteza Matumaini kila uchao, kutoona tumaini mbele yao,kuona ya jana ni bora kuliko ya leo. Kuona wanaishi kama wapo jehanamu na kutokuwa na uhakika wa kuiona kesho yao wakiwa wazima na wenye kupumua.

Hii hutokea pale aliyekalia kiti anapokuwa Dikteta ,katili na Asiyejali wala kuguswa na hali mbaya za watu wake. Taifa linakuwa linakuwa ni kama limefiwa au lipo katika maombolezo muda wote.kwa kuwa mioyo ya watu inakuwa ina huzuni na kukosa amani na furaha muda wote. Watu wanakuwa hawana mfariji wala wa kuwatia moyo kwa sababu aliyepo kitini hana hisia za upendo wala huruma wala kujali wala kuguswa na hivyo kufanya mambo na kuchukua hatua za kuwaumiza watu na kuleta mateso katika maisha ya watu. Kutoa lugha na maneno yenye kuchoma mioyo ya watu na kuwakatisha Tamaa.

Lakini Rais Samia Amekaa kitini na kuwa kama nyota ya asubuhi iletayo Matumaini ya Mapambazuko na kuondoka kwa giza .Mama Samia kwa hakika ni chaguo la Mungu aliyeinuliwa na Mungu Mwenyewe kuliongoza Taifa letu.View attachment 3307130View attachment 3307136View attachment 3307140

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Acha kukufuru ndugu. Sifa, heshima na utukufu wote anastahili yeye Aliye juu
 
Back
Top Bottom