Rais Samia ni Nuru na Mwanga wa Taifa letu na watanzania wote kwa ujumla wake

Ulitaka huyo mkurugenzi achaguliwe na nani.
Asichaguliwe bali aombe nafasi na professionals wampitishe kwa ushindani kama ilivyo kenya. Ushindi wa rais uhojiwe mahakamani. Hapa kwetu anaweza hata kupata kura 2 na bado akatangazwa mshindi na hakuna wa kushtaki popote. Upuuzi mtuupu. Lowasa alimgalagaza magufili lakini tume ikaamua kumtangaza jpm
 
Mama akilipa madeni ya Jangwani kwenye ule mradi upo funded na world bank tunambwagia kura kama zote. Mama anatosha. Tutaishije bila mama
 

Mathayo 5: 13.... inasema
Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni




Ndio maana CAG anapotoa taarifa zake, tunaficha sura maana kuna mambo mengi ni aibu. Wizi wa mali ya umma na kukosekana kwa uwajibikaji, nayo pia ni nuru na mwanga wa Taofa letu?

Nakushauri, uwe unaangalia nini unaandika. Mengine haya yanaonyesha uwezo wako mdogo wqa kupambanua mambo
 
Wabadhirifu wa mali ya umma huchukuliwa hatua kali za kisheria baada ya kubainika. Hakuna Mtumishi mbadhirifu aliye salama katika uongozi huu wa Jemedari wetu hodari.
 
Huko huko Kenya unakokusifia tumejionea kila wakati Raila Odinga akilia na kupiga makelele ya kuibiwa kura na kuhujumiwa mpaka kufikia hatua ya kufanya uhaini wa kwa kuliapisha..
 
Dr.Samia Suluhu Hassan si nuru na mwanga wa Taifa tu,

bali pia ndie mbeba maono ya waTanazania wote, Dr.Samia ni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…