Rais Samia ni zawadi kwetu Watanzania tunayopaswa kujivunia na kuiheshimu

Mama mwenyewe hapumzika Sasa vijana tunaomuunga mkono tutapumzikaje wakati kazi anazozifanya Ni nyingi na kila siku mama analeta fursa hapa nchini? Huoni wawekezaji wanavyopigana vikumbo kuja Tanzania? Huoni watalii wanavyoshindana kuwahi kukata tiketi za kuja kutalii Tanzania? Hizo zote Ni juhudi za mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kipenzi Cha watanzania na Tumaini la watanzania katika kuwaletea maendeleo, mama anapiga kazi muda wote bila kuchoka na Wala huwezi kumaliza kuyaelezea mambo makubwa anayofanya ukayamaliza
Lucas pumzika akili ipate walau "fresh air"...duh!
 
Ni mamilioni ya watanzania wanaridhishwa na utendaji kazi uliotukuka wa Rais Samia ulioacha Alama katika mioyo yao
Labda useme mamia ya Wakojani! Watanzania siyo wajinga kama ulivyo wewe. Njoo mtaani uwaulize halafu uone watakacho kufanya.
 
Alambe asali ya wapi huyu! Anajikomba komba tu ili afikiriwe kwenye uteuzi. Amechagua kujitoa ufahamu, ili maisha yaendelee!

Hawa ndiyo wale uvccm ambao akili zao zote wamezihamisha kutoka kichwani, na kuzipeleka tumboni.
Duu inasikitisha Sana.
 
Kazi ya kupuyanga hovyo na kupanda Kimbinyiko za kwa Malkia siyo!!
 
Hivi hujisikii hata aibu! Maana unapambana peke yako humu kumsifia! Hakika umekuwa kama mtoto yatima!
Kwani wewe huoni aibu kumpinga na kumkosoa mh Rais wetu mpendwa kwa kila kitu afanyacho ambacho kina maslahi na faida kwa watanzania? Mbona kila siku unatamani kuona watanzania wakiteseka? Wewe huwa huoni aibu? Mbona hata mafuta yakishuka wewe unakosoa tu kwa kuanza kupotosha potosha tu kana kwamba Raha yako wewe Ni kuona watanzania wakiteseka? Kwanini moyo wako hauna shukurani katika mema?
 
Kazi ya kupuyanga hovyo na kupanda Kimbinyiko za kwa Malkia siyo!!
Anapuyanga? Huoni mambo makubwa na fursa zinazoletwa hapa nchini kutokana na mh Rais wetu mpendwa kuimarisha diplomasia na mahusiano mema yanayotufungia milango watanzania? Ni juhudi za mh Rais wetu mpendwa zilizotusaidia wakulima mwaka huu kuuza kwa Bei nzuri hasa kwaajirani zetu,lakini pia pembejeo zimeshuka Bei baada ya kutoa mabillioni ya Ruzuku,
 
Mimi siku zote huwa najiona shujaa sana pale ninaposema ukweli. Watanzania wanateseka na tozo kandamizi zilizoanzishwa na huyu Rais wako!

Mshauri aondoe matozo yake yote ili wananchi wapate unafuu wa maisha! Wananchi kwa sasa wanalia na kusaga meno kutokana na mfumuko wa bei uliosababishwa na Rais wako kuongeza tozo kwenye mafuta ya petrol, diesel na mafuta ya taa!
 
--Huoni mfumuko wa bei za chakula huku mtaani?
--
 
Wakulima wa wapi hao wanao uza mazao yao kwa bei nzuri? Yaani kwa akili yako umeshindwa kutofautisha kati ya wakulima, na madalali (middlemen)! Wanaokwenda kununua mazao yakiwa shambani kwa hao wakulima, na baadaye kwenda kuyauza tena kwa bei ya juu!!

Pole sana.
 
Samia hassan first of her name the queen of Andal and first men protector of seven kingdom the mother of dragons the khaleesi of the Great Grass sea and the breaker of chain
 
Acha kujadili na kuandika vitu vya upotoshaji, Mimi Naheshimu Sana michango yako humu jukwaani lakini nashangaa unavyopenda kupotosha, hivi Rais Samia Ndiye aliyepandisha Bei ya Nishati ya mafuta? Huoni kuwa hiyo Ni sababu ya kupanda katika soko la Dunia hasa baada ya wazalishaji wa mafuta kuingia katika Vita huko ukrein? Je hukuona juhudi za mh Rais kukabiliana na suala Hilo kwa uamuzi wake wa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi katika mafuta? Hukuona pia mh Rais wetu mpendwa akitoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika kilimo na kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni? Juhudi hizi zote hukuziona kweli? Au umeamua kujipa upofu tu na kuamua kuendeleza utamaduni wako wa kupinga kila kitu kinachofanywa na mh Rais wetu mpendwa?
 
Alambe asali ya wapi huyu! Anajikomba komba tu ili afikiriwe kwenye uteuzi. Amechagua kujitoa ufahamu, ili maisha yaendelee!

Hawa ndiyo wale uvccm ambao akili zao zote wamezihamisha kutoka kichwani, na kuzipeleka tumboni.
Mimi naongelea mazuri na kazi njema inayofanywa na mh Rais wetu mpendwa ambayo kiukweli kwa kiasi kikubwa imegusa maisha yetu watanzania wanyonge, Ni Haki yangu na nipo huru kufanya hivyo Kama ambavyo nawe ulishaamua kujipa upofua wa kutoona zuri lolote na kubaki unakosoa kila kitu mpaka watu wanabaki wanakushangaa na kuona unastahili matibabu ya kisaikolojia
 
Mimi mwenyewe nipo mtaani huku ndio naona namna mh Rais wetu mpendwa anavyokubalika na kukonga nyoyo za watanzania
Labda useme mamia ya Wakojani! Watanzania siyo wajinga kama ulivyo wewe. Njoo mtaani uwaulize halafu uone watakacho kufanya.
 
Bora hata hapa umejitahidi kujenga hoja! Natambua fika kuna ongezeko la bei ya mafuta kutokana na hiyo vita ya Urusi dhidi ya Ukraine!

Lakini usisahau Rais wako kipenzi kwa kumtumia Waziri wake wa fedha, wameongeza tozo kwenye hayo mafuta ili hela itakayo patikana, ikajengee madarasa na vituo vya afya!


Na hata hiyo ruzuku anayoitoa, haina maana yoyote ile! Maana itaishia tu mikononi mwa wafanyabiashara wakubwa na wasio waaminifu!

Alichotakiwa Bi tozo kufanya, ni kuiondoa kabisa ile tozo yake aliyo ianzisha, mpaka hapo hali ya uchumi itakapo tengemaa.
 
Sikiliza wewe Mimi Ni mkulima na ninaongea uhalisia wa kile nachokiishi na kukifanya, mwaka huu Bei ya mazao ilikuwa nzuri tangia wakati wa mavuno na hivyo kutufanya kuuza kwa Bei nzuri tokea wakati tunavuna mazao yetu, tofauti na miaka mingine ambapo tuliuza kwa Bei ya hasara wakati wa mavuno
 
Tangu lini wewe Lucas mwashambwa umekuwa msemaji wa watanzania?
Hii tabia ya kushinda mitandaoni kusifia viongozi ni ya hovyo sana siku nyingine jisemee mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…