Rais Samia ni zawadi kwetu Watanzania tunayopaswa kujivunia na kuiheshimu

Hakuna chá zawadi wala nini hata jiwe mlikuwa mnamsujudia kama huyu wasasa hamna jipya hata moja.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Ukijivunia wewe inatosha!
Vijana wengine ni kama wale waliopoteza fursa walizo pewa wanajaribu sasa kuzirudisha fursa,sijui kama wanaijua ile misemo ya wahenga,wakati ukuta,bahati huja mara moja.Maskini akipata ......,Mawazo ya anga zananiambia hivi ni jamii ya akina Konda boy na akina Saa mbovu🥱
 
Ukakasi upi, unataka kupingana na reality, tena reality of science?
Sawa mwana sayansi bila shaka huwa maneno ya namna hiyo huwa unayazungumza hata kwa wazazi wako bila hofu kwa kuwa hayo ndio matunda ya gharama ya Elimu waliyo kulipia shuleni kusoma sayansi
 
Ni mamilioni ya watanzania wanaridhishwa na utendaji kazi uliotukuka wa Rais Samia ulioacha Alama katika mioyo yao

Alisemwa hivo kila Rais aliyewahi kuiongoza nchi hii. Kuanzia JKN, HAM, BWM, JMK, JPM na hata SSH na hata wengine watakaokuja. Unatosha wewe kusifia SSH na kwa tabia yako hii hata JPM alipokuwa madarakani - ulisifia hivi hivi.

Kujipendekeza ni tabia. Lakini si tabia ya ujumla. Kitu kimoja cha wazi kwa wanaojipendekeza - kupenda kuwakilisha wengine. Kama hapa unavotuwakilisha kupitia mawazo yako binafsi.

Jitenge na kuniwakilisha!
 
Maoni yako tu
 
Labda wewe ndio uliyejitenga lakini huku niliko mtaani Ni watanzania wengi Sana wenye Imani na mh Rais Samia
 
Mnataka demokrasia gani Zaid ya hii kubwa iliyopo hapa nchini ambayo badala ya kuzitumia vyema nyinyi mmejikita katika kuporomosha matusi tu kwa kila Jambo kana kwamba mmevurugwa akili
Ni Imani yangu kuwa hakuna kijani yeyote aliye wahi kuwa Zawadi kwa Mtanzania wa kawaida,siku ikitokea

Kama yalivyo kuwa maoni yako na ndiyo Demokrasia wanayoiogopa Kijani🥱
 
Unalipwa shilingi ngapi?
 
Unalipwa shilingi ngapi?
Silipwi chochote zaidi ya kazi anazofanya mh Rais wetu katika kututumikia watanzania kwa moyo wa uzalendo na wakutukuka, labda nikuulize wewe huwa unalipwa shilingi ngapi mpaka unashinda muda wote ukipinga na kukosoa kila kitu kizuri kinachofanywa na serikali hii ya mama Samia? Kwambaa Kwako hakuna jema la serikali hii? Naona wewe Hata akija malaika kuongoza Tanzania utampinga kwa mazuri anayoyafanya na kusema Ni shetani anayejipa jina la umalaika
 
Nawaona namna mlivyofura hasira na kusononeka mnapoona namna mh Rais Samia anavyokubalika na watanzania na namna nchi ilivyo na amani na utulivu huku watanzania wakiendelea na kazi zao kwa Uhuru na aman
Basi atamteua mumeo kama shukrani kwako
 
Alambe asali ya wapi huyu! Anajikomba komba tu ili afikiriwe kwenye uteuzi. Amechagua kujitoa ufahamu, ili maisha yaendelee!

Hawa ndiyo wale uvccm ambao akili zao zote wamezihamisha kutoka kichwani, na kuzipeleka tumboni.
Hata maneno ya huyu jamaa yanaonesha kuwa na yeye alikuwa anajikomba komba ili afikiriwe na yeye kama alivyofikiriwa mwenzake Mbatia enzi zile.
Tanzania hatuna wana siasa bali tuna wachumia tumbo tu.
 

Attachments

  • Screenshot_20220605-082514_1.jpg
    159.8 KB · Views: 5
Usichoke kada. Watu watakukatisha tamaa lakini usichoke. Najua unakumbuka maneno aliyokuwa anakuambia shaka siku ile nimewakuta pale hotel. Utatoka tu la msingi ni kutokata tamaa..juhudi zako zinaonekana. Unajitahidi.
 
Usichoke dogo. Watu watakukatisha tamaa lakini usichoke. Najua unakumbuka maneno aliyokuwa anakuambia shaka siku ile nimewakuta pale hotel. Utatoka tu la msingi ni kutokata tamaa..juhudi zako zinaonekana. Unajitahidi.
 
Hata Uganda enzi za Amini walisema ni zawadi iliyoletwa kutoka Mbinguni kuiongoza Uganda!

Cc. dronedrake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…