Rais Samia ni zawadi kwetu Watanzania tunayopaswa kujivunia na kuiheshimu

Kweli hii ni zawadi kwa watanzania maana Rais Samia Suluhu aliahidi kufanya maendeleo yanayomlenga direct mwananchi na amefanikiwa ndani ya siku 570 za utawala wake ameboresha sekta ya elimu, afya, miundombinu, kilimo na mengine mengi.
 
Mnampiga hela, halafu mnakuja kumsifia...Ila NYIEEEE[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Alambe asali ya wapi huyu! Anajikomba komba tu ili afikiriwe kwenye uteuzi. Amechagua kujitoa ufahamu, ili maisha yaendelee!

Hawa ndiyo wale uvccm ambao akili zao zote wamezihamisha kutoka kichwani, na kuzipeleka tumboni.
Tatizo la watanzania hamtaki watu wameseme mazuri ya serikali mnataka kila mtu apinge tu kusema maendeleo yanayoonekana ni moja ya uzalendo na sio kutafuta teuzi Rais Samia Suluhu anafanya kazi kubwa ya maendeleo kwaajili yako wewe na mimi
 
Kwenye uongozi tena wa kuomba kupigwa kura hakuna Cha zawadi hapa, wakati anakua Mgombea mwenza alijua kwamba bila kujali rais you hai au la Yapo majukum atayatekeleza endapo Rais amesafiri au hayupo kabisa( kifo)

Kama angeona hawezi angekataa kua Mgombea mwenza so afanye kazi hakuna Cha zawadi hapa ,umesikia wewe mwanaccm ,mfikishie ujumbe mwenyekiti wako
 
Ni zawadii kwa kuwa anatekeleza majukumu yake vizuriii Sanaa hivyo lazima tumpongeze Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania wote
 
Mwezi huu ni wa afya ya akili wahi mirembe ukapate matibabu
 
Wewe hatutaki sifa na wala hutofanywa mbunge wa viti maalum wala hutopandishwa cheo wala hutopewa uongozi wowote hiyo tunaijua hiyo
 
Mimi nimejiajiri katika kilimo ambako Rais wetu mpendwa ametuangalia kwa jicho la huruma na upendo kwa kuhakikisha kuwa mbolea inapatikana kwa Bei tunayoweza kuimudu kwa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini na kuongeza bajeti ya kilimo kufika billioni Mia Tisa na point
Wewe hatutaki sifa na wala hutofanywa mbunge wa viti maalum wala hutopandishwa cheo wala hutopewa uongozi wowote hiyo tunaijua hiyo
 
Ni zawadii kwa kuwa anatekeleza majukumu yake vizuriii Sanaa hivyo lazima tumpongeze Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania wote
Lazima afanye kazi kwani si analipwa mshahara, Sasa hapa tumpongeze KWa lipi kwati ni wajibu wake ,ndo maana akakubali iyo kazi ,na ndo maana analipwa mshahara na kutunzwa KWa kodi za watanzania, Sasa pongenzi za nini hapa tena ,

We mwana ccm vipi tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…