Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Mwanamke gan msomi???

Angekua msomi, asingezungusha Kidato Cha nne.

Infact , ana Elimu ya kuunga unga sanaaa,

Na ukweli nikwamba, kwake yeye, Kuunga unga kumtokana na akili kua kiduchu.
Maisha yake mengi ameishi akiwa msambaza chai tu kwenye maofisi ya asasi za kisiasa (secretary& ukarani), huku kwenye uongozi kaibukia tu kwa ngekewa.
 
Tuna katiba ya hovyo sana
Ukiwa na katiba ya ovyo, halafu ukashindwa kuibadili, tatizo ni wewe hapo.

Kwa sababu kuna wengine walikuwa na katiba za ovyo lakininm wakaweza kuzibadili.

Kwa hivyo, tusisingizie katiba tu.

Katiba inawekwa na watu, watu hawawekwi na katiba.

Tatizo ni jamii yetu. Jamii ingekuwa na muelekeo mzuri, tungekuwa na katiba nzuri na viongozi wazuri.

Jamii yetu imebuma. Hivyo katiba yetu imebuma na uongozi wetu hivyo hivyo.

Tusisingizie katiba.
 
Kawa mkweli kwa hao anaozungumza nao kuliko kufanya ukatili wa chini chini.
Tutafika hatua ambayo mtasema ukatili wake sio mbaya kama ulivyokuwa ukatili wa yule aliyepita, nasema hivyo kwa sababu jinsi ambavyo watu walivyokuwa wanamchukulia na kumzungumzia Samia huko mwanzoni kabisa ni tofauti na sasa. Mwanzo tulidhani Samia yeye atakuwa ni mvumilivu kwenye kukosolewa na hata yeye alijisifu hivyo ila kwa mifano ya Ndugai na Bashiru hali imeonesha kuwa hana hiyo ngozi ngumu ila mkatetea kwamba bora yeye hateki wala kuuwa, na hili la sasa bado tena mnatetea kwamba bora yeye amesema ukweli kuliko angefanya ukatatili wa chini kwa chini.
 
Ni kama vile tunazama katika kujadili haiba za viongozi ambao ni binadamu kama mimi na wewe. Wapo wanaosema tubadili mfumo, nadhani tufike mahali twende hatua moja zaidi kwa mustakabali wa nchi yetu.
 
Ni kama vile tunazama katika kujadili haiba za viongozi ambao ni binadamu kama mimi na wewe. Wapo wanaosema tubadili mfumo, nadhani tufike mahali twende hatua moja zaidi kwa mustakabali wa nchi yetu.

..Raisi amekosea kutoa kauli ile.

..Kauli yake inawapa jina baya wanaharakati.

..Pia inatoa "green light " kwa sheria zetu na mahakama zetu kutumika dhidi ya wanaharakati.

..Tanzania tuna utamaduni kwamba Raisi hakosei. Au kauli ya Raisi ni maagizo au " sheria. "

..Mara nyingi tumeathirika vibaya kwasababu ya kulazimisha kutekeleza, au kuhalalisha, kauli au matamko ya Raisi ambayo yana makosa au ni kinyume cha sheria.

..Fikiria nguvu iliyotumika kuhalalisha kauli yenye makosa ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara.

..Tumeumiza watu wangapi? Watumishi wangapi wa umma wamechafuka kimaadili na kitaaluma ktk kutekeleza agizo lile?

..Kauli ya Raisi Ssh ikifanyiwa kazi italeta athari mbaya kwa jamii.
 

Uko sahihi mkuu.
 
Hoja ilikuwa nini mpaka kusema hayo!?

Halafu kazi mojawapo ya rais ni kuleta utengamano katika nchi hata kama unapata upinzani kiasi gani kauli za utata kama hizi angeshauriwa aziepuke maana hizo ndiyo zilizomfanya mwendazake kuchukiwa
Ulimchukia labda wewe mbona mimi nilimpenda tu.
 
..Shangazi amejibu vizuri sana hapa.

..Uanaharakati unaisaidia serikali kujua wapi panatakiwa kuboreshwa.

 
The President Woman is right. TLS was a den of thieves. The TLS president woman (small p small w) was one of the legal advisers to mining companies that looted our minerals. She inherited it from an even bigger crook with nothing but harsh abusive words. she (small s) came from a privileged background, schooled overseas and generally overpampered, she could not see the immense efforts being made ber Her (big H) for the vast majority.
 
Nakumbuka wakati Samia akiwa ni makamu wa rais aliwahi kutamka kwamba rais hakosei, ina maana hivyo ndivyo anavyoamini toka hajawa rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…