Engineer...
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza jinsi EAMWS iivyovunjwa na serikali na nimeeleza sababu kwa nini ilivunjwa.
Hayo sitayalelza hapa.
Hapa nitaeleza jinsi serikali ilivyoshughulikia mali za Waislam na kuipa BAKWATA:
''Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Said Mswanya kwa kuamriwa na Rais Julius Nyerere akatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.[1]
Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao.
Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo la mgogoro wa EAMWS.
Viongozi wa EAMWS wakiongozwa na Rais wa EAMWS Tawi la Tanzania Tewa Said Tewa waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.
Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama.
Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza.
Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali na Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam.
Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kutoa mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.
Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe.
Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu lililokuwa likishirikiana na serikali na vyombo vyake vyote vya usalama.
BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa.''
Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyopotea mali ambazo BAKWATA leo inadai ni mali zao.
Hata hapo Kinondoni ulipojengwa msikiti mkubwa wa Mfalme Hassan wa VI wa Morocco hicho kiwanja pamoja na shule ys Sekondari ya Kinondoni vimejengwa katika ardhi ya EAMWS na shule ilijengwa na EAMWS.
File la Tewa Said Tewa lenye taarifa za mgogoro wa EAMWS
Tewa Said Tewa akisalimiana na Waislam
wakati alipokuwa kiongozi wa EAMWS
Inatakiwa umakini sana pale BAKWATA inapounganishwa na Waislam kwa kuwa BAKWATA haikuundwa na Waislam.
Tafuta muhtasari wa mkutano ambao Waislam walikutana na kuamua kuwa hawaitaki EAMWS.
Haupo.
Waislam wengi wako kimya kuhusu BAKWATA kwa ajili ya kuweka staha ya hawa viongozi waliokuwapo madarakani hivi sasa ili wapate utulivu na waendeshe shughuli zao.