Massa,
Waislam walipounda African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 hadi kuunganisha wananchi wote kupigania uhuru wa Tanganyika waliiga kutoka kwa nani?
Ali Mnjale na Salum Mpunga waliposafiri kutoka Lindi kuja Dar es Salaam kushawishi viongozi wa TANU kumleta Nyerere Lindi, Southern Province kuvunja propaganda kutoka Peramiho wakiwazuia waumini wao kujiunga na TANU wakiwatisha kuwa harakati za uhuru zilikuwa Maji Maji nyingine Waislam wanataka kupambana na Waingereza mipango hii waliiga kutoka wapi?
Haiyumkiniki kuwa waliwaiga Wakatoliki.
Nani aliyekuambia Waislam hatuna umoja?
Nyerere kafika Dar-es-Salaam 1952 nani walimpokea na kuishinae hadi uhuru ukapatikana?
Waislam wangekuwa hawana umoja Nyerere angechaguliwa vipi na Waislam wa Dar-es-Salaam kuongoza TAA 1953 na TANU 1954?
Nani aliyekuambia kuwa haki ya Waislam inaweza kutolewa na Rais Muislam peke yake?