Modest...
Soma kitabu, "Development and Religion in Tanzania," (1981) cha Jan P van Bergen kinaeleza mikutano ya Nyerere na viongozi wa Kanisa Katoliki Ikulu.
Mimi hujizuia sana kuandika haya lau kama nayajua mengi.
Lakini kwa kuwa hukuwa unayajua hayo nimekupa rejea hiyo ili uijue nchi yetu na matatizo yake.
Kitabu hiki kilikuwa kinauzwa Cathedral Bookshop lakini kwa unyeti wa yaliyokuwa ndani ya kitabu hicho kimya kimya kiliondolewa sokoni kisiuzwe.
Hiki kitabu kilikuwa maarufu sana kwa Waislam katika miaka ya 1980.
Taarifa hizo zilizokuwa katika kitabu hicho ziliandikwa katika kitabu cha Prof. Njozi, "Mwembechai Killings..." (2002)na serikali ya Rais Mkapa ikapiga marufuku kitabu hicho.
Kuitaka serikali ijitenge na dini kwa maana yake kwa Tanzania ni kulitaka Kanisa likae nje ya serikali.
Huu ni muhali mkubwa kwani Kanisa limehodhi uendeshaji wa nchi kwa asilimia 80:20.
Hii ni kama vile Waislam hawapo.
Hili la waumini wa dini zote halipo Tanzania.
Dini kubwa zenye maslahi na serikali ni Uislam na Ukristo.
Waislam maslahi yao katika serikali ni historia yao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Wakristo maslahi yao ni kuwa ndiyo walioshika madaraka ya kuendesha nchi toka uhuru upatikane mwaka wa 1961 hadi hivi sasa.
Vipi leo utawataka waachie madaraka haya?
Busara ni walioshika madaraka yote ya serikali wawe tayari kuona na wengine wanapata fursa walizopata wao za elimu nk na wanaingi serikalini bila wao kuwa pingamizi.