Kilimbatzz
JF-Expert Member
- Feb 11, 2023
- 9,134
- 14,593
🥰🥰🥰🥰🥰
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🥰🥰🥰🥰🥰
Hadi Bakwata wanaiba, tutaponea wapi sasa 😏Ni hivi, mali za Bakwata zinauzwa na viongozi waliopo, sasa wanapoingia viongozi wapya wanadai mali hizo zimedhulumiwa.
Nilishuhudia mgogoro mmoja kule mabwepande heka karibu 50 zimeuzwa kihuni kabisa na viongoziNdio maana umesikia hiyo kauli ya Rais
Frank...Mkuu wewe ni mwanahistoria tusaidie historia ya Bakwata na mali zake ili tujue ni kweli kuna mali zilizoporwa ili tujue waliopora hizo mali ni akina nani.
Kwambw Bakwata wametambua kuwa RAISI ni MUISLAMU ila nchi haina DINI.Sijaielewa unakusudia kusemaje
tatizo kubwa la ndugu zetu waislamu wanaamini wakristu na wengine wasio waislamu ndiyo adui yao mkuu, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo
Na mimi nilikuwa nasikilizia. Nahisi walifanikiwa kumuondosha mkuu wa wilaya mana ndiye alituhumiwa kuchochea huo mgogoro. Kwenye ule mkeka wa mwisho mwisho yule mkuu wa wilaya alihamishiwa maeneo ya pwani kitu kama vile.Kuna lile dude kule Kigoma na Kanisa Katoliki ambalo Askofu aliandika waraka kutishia kuendesha kampeni ya kuifuta CCM Kigoma kama wakiporwa eneo lao. Sijui imefikia wapi hilo dude [emoji851]
EAMWS ni ya waislamu na Bakwata ni ya waislamu, shida ipo wapi.Frank...
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza jinsi EAMWS iivyovunjwa na serikali na nimeeleza sababu kwa nini ilivunjwa.
Hayo sitayalelza hapa.
Hapa nitaeleza jinsi serikali ilivyoshughulikia mali za Waislam na kuipa BAKWATA:
''Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Said Mswanya kwa kuamriwa na Rais Julius Nyerere akatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.[1]
Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao.
Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo la mgogoro wa EAMWS.
Viongozi wa EAMWS wakiongozwa na Rais wa EAMWS Tawi la Tanzania Tewa Said Tewa waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.
Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama.
Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza.
Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali na Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam.
lakini nini ilikuwa dhima ya welfare society za waislam
Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kutoa mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.
Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe.
Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu lililokuwa likishirikiana na serikali na vyombo vyake vyote vya usalama.
BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa.''
Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyopotea mali ambazo BAKWATA leo inadai ni mali zao.
Hata hapo Kinondoni ulipojengwa msikiti mkubwa wa Mfalme Hassan wa VI wa Morocco hicho kiwanja pamoja na shule ys Sekondari ya Kinondoni vimejengwa katika ardhi ya EAMWS na shule ilijengwa na EAMWS.
Ni shida sana,unakuta kosa limefanywa na muislamu lakini anatafutwa wa kulaumiwa ambaye sio muislamutatizo kubwa la ndugu zetu waislamu wanaamini wakristu na wengine wasio waislamu ndiyo adui yao mkuu, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo
👩🏻🦰🥰🥰🥰🥰🥰
Kwakweli hata mimi naona ni kama haya mambo wangekaa wajitizame vizuri aidha Mufti mwenyewe au aunde jopo la ukweli na maridhiano ili ikibidi hii migogoro iishe iwe kwa kusamehe na kuanza upya au kutumia gharama kuyakomboa maeneo haya.Ni shida sana,unakuta kosa limefanywa na muislamu lakini anatafutwa wa kulaumiwa ambaye sio muislamu
Hapana ndugu pana uhasama fulani hivi usioisha kati ya bakwata na taasisi nyingi za kiisilamu wengi wakiituhumu bakwata kuwa imeanzishwa na kuwekwa na serikali ili kudhoofisha umoja na nguvu ya waisilamu na hata ukimsomoma ndugu yetu Mohammed said anaeleza hili jambo.EAMWS ni ya waislamu na Bakwata ni ya waislamu, shida ipo wapi.
Muslim welfare dhima yake ilikuwa nini, ambayo leo hii Bakwata hawaifanyi.
Kwenye kuuza ningeomba serikali ikitoa ardhi kwa NGO iweke sheria ya kuzuia mali hizo zisiuzwe mpaka kuhusisha na vyombo vingine vya kiserekali na jamii husika
August,EAMWS ni ya waislamu na Bakwata ni ya waislamu, shida ipo wapi.
Muslim welfare dhima yake ilikuwa nini, ambayo leo hii Bakwata hawaifanyi.
Kwenye kuuza ningeomba serikali ikitoa ardhi kwa NGO iweke sheria ya kuzuia mali hizo zisiuzwe mpaka kuhusisha na vyombo vingine vya kiserekali na jamii husika
The Phy...Hapana ndugu pana uhasama fulani hivi usioisha kati ya bakwata na taasisi nyingi za kiisilamu wengi wakiituhumu bakwata kuwa imeanzishwa na kuwekwa na serikali ili kudhoofisha umoja na nguvu ya waisilamu na hata ukimsomoma ndugu yetu Mohammed said anaeleza hili jambo.
August,
Shida ni kuwa BAKWATA haikuundwa na Waislam.
Shida ni kuwa EAMWS ilivunjwa na serikali kuzuia isijenge Chuo Kikuu ili Waislam wabakie nyuma katika elimu kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni.
Hapa ndipo shida yao unaanzia,kila kukicha wanatafuta makosa ya miaka ya 70 huko.Sasa kwa nini msiungane kuivunja hiyo bakwata,ili mjenge taasisi imara moja,mana kinachoendelea sasa ni kuzidi kulalamika na kujitenga zaidi mama kila dhehebu la kiislam sasa lina taasisi yake.
Hii idea ni nzuri sana kwamba hawa kina mzee Mohamed ambao ni wanazuoni wa kiisilamu wapandikize masnichi ndani ya bakwata kama sio kujipenyeza wao wenyewe ili waifumue na kuisuka upya kwa sura na namna itakayowaridhisha kwamba ni chombo cha waisilamu.Sasa kwa nini msiungane kuivunja hiyo bakwata,ili mjenge taasisi imara moja,mana kinachoendelea sasa ni kuzidi kulalamika na kujitenga zaidi mama kila dhehebu la kiislam sasa lina taasisi yake.
Sasa kwa nini msiungane kuivunja hiyo bakwata,ili mjenge taasisi imara moja,mana kinachoendelea sasa ni kuzidi kulalamika na kujitenga zaidi mama kila dhehebu la kiislam sasa lina taasisi yake.
The Phy...Hii idea ni nzuri sana kwamba hawa kina mzee Mohamed ambao ni wanazuoni wa kiisilamu wapandikize masnichi ndani ya bakwata kama sio kujipenyeza wao wenyewe ili waifumue na kuisuka upya kwa sura na namna itakayowaridhisha kwamba ni chombo cha waisilamu.
Ingawa naona ugumu katika hilo kwani sina shaka kwamba huko ndani ya bakwata kwa vyovyote iwavyo Kuna jicho la kuhakikisha bakwata inabaki kama ilivyo kwa manufaa ya Dola.
Na kama hivyo ndivyo basi hakuna chaguo jingine la kuleta suluhu isipokuwa kuandaa watu kimkakati na kuwapandikiza ndani ya bakwata ili waiue wakiwa humohumo.
Vinginevyo wakubali maumivu kuendelea kudhni kwamba Kuna kitu serikali itafanya kuleta hali tofauti ni kujidanganya
Dingi...Hapa ndipo shida yao unaanzia,kila kukicha wanatafuta makosa ya miaka ya 70 huko.
Waombe waoneshe hata mikakati yao tu maendeleo ndani ya jumuiya zao utakuta hawana.
Lakini kila siku wanalalamikia Serikali.
Jiwe...Sasa kwa nini msiungane kuivunja hiyo bakwata,ili mjenge taasisi imara moja,mana kinachoendelea sasa ni kuzidi kulalamika na kujitenga zaidi mama kila dhehebu la kiislam sasa lina taasisi yake.