Rais Samia: Nilipoingia ofisini tu Mufti alinijia na furushi la migogoro ya mali za BAKWATA, ila tatizo wamelitengeneza wenyewe

Mkuu wewe ni mwanahistoria tusaidie historia ya Bakwata na mali zake ili tujue ni kweli kuna mali zilizoporwa ili tujue waliopora hizo mali ni akina nani.
Frank...
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza jinsi EAMWS iivyovunjwa na serikali na nimeeleza sababu kwa nini ilivunjwa.

Hayo sitayalelza hapa.

Hapa nitaeleza jinsi serikali ilivyoshughulikia mali za Waislam na kuipa BAKWATA:

''Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Said Mswanya kwa kuamriwa na Rais Julius Nyerere akatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.[1]

Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao.

Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo la mgogoro wa EAMWS.

Viongozi wa EAMWS wakiongozwa na Rais wa EAMWS Tawi la Tanzania Tewa Said Tewa waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.

Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama.

Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza.

Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali na Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam.

Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kutoa mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.

Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe.

Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu lililokuwa likishirikiana na serikali na vyombo vyake vyote vya usalama.

BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa.''

Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyopotea mali ambazo BAKWATA leo inadai ni mali zao.

Hata hapo Kinondoni ulipojengwa msikiti mkubwa wa Mfalme Hassan wa VI wa Morocco hicho kiwanja pamoja na shule ys Sekondari ya Kinondoni vimejengwa katika ardhi ya EAMWS na shule ilijengwa na EAMWS.
 
Kuna lile dude kule Kigoma na Kanisa Katoliki ambalo Askofu aliandika waraka kutishia kuendesha kampeni ya kuifuta CCM Kigoma kama wakiporwa eneo lao. Sijui imefikia wapi hilo dude [emoji851]
Na mimi nilikuwa nasikilizia. Nahisi walifanikiwa kumuondosha mkuu wa wilaya mana ndiye alituhumiwa kuchochea huo mgogoro. Kwenye ule mkeka wa mwisho mwisho yule mkuu wa wilaya alihamishiwa maeneo ya pwani kitu kama vile.
 
Frank...
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza jinsi EAMWS iivyovunjwa na serikali na nimeeleza sababu kwa nini ilivunjwa.

Hayo sitayalelza hapa.

Hapa nitaeleza jinsi serikali ilivyoshughulikia mali za Waislam na kuipa BAKWATA:

''Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Said Mswanya kwa kuamriwa na Rais Julius Nyerere akatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.[1]

Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao.

Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo la mgogoro wa EAMWS.

Viongozi wa EAMWS wakiongozwa na Rais wa EAMWS Tawi la Tanzania Tewa Said Tewa waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.

Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama.

Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza.

Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali na Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam.
lakini nini ilikuwa dhima ya welfare society za waislam
Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kutoa mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.

Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe.

Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu lililokuwa likishirikiana na serikali na vyombo vyake vyote vya usalama.

BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa.''

Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyopotea mali ambazo BAKWATA leo inadai ni mali zao.

Hata hapo Kinondoni ulipojengwa msikiti mkubwa wa Mfalme Hassan wa VI wa Morocco hicho kiwanja pamoja na shule ys Sekondari ya Kinondoni vimejengwa katika ardhi ya EAMWS na shule ilijengwa na EAMWS.
EAMWS ni ya waislamu na Bakwata ni ya waislamu, shida ipo wapi.

Muslim welfare dhima yake ilikuwa nini, ambayo leo hii Bakwata hawaifanyi.

Kwenye kuuza ningeomba serikali ikitoa ardhi kwa NGO iweke sheria ya kuzuia mali hizo zisiuzwe mpaka kuhusisha na vyombo vingine vya kiserekali na jamii husika
 
Ni shida sana,unakuta kosa limefanywa na muislamu lakini anatafutwa wa kulaumiwa ambaye sio muislamu
Kwakweli hata mimi naona ni kama haya mambo wangekaa wajitizame vizuri aidha Mufti mwenyewe au aunde jopo la ukweli na maridhiano ili ikibidi hii migogoro iishe iwe kwa kusamehe na kuanza upya au kutumia gharama kuyakomboa maeneo haya.
 
EAMWS ni ya waislamu na Bakwata ni ya waislamu, shida ipo wapi.

Muslim welfare dhima yake ilikuwa nini, ambayo leo hii Bakwata hawaifanyi.

Kwenye kuuza ningeomba serikali ikitoa ardhi kwa NGO iweke sheria ya kuzuia mali hizo zisiuzwe mpaka kuhusisha na vyombo vingine vya kiserekali na jamii husika
Hapana ndugu pana uhasama fulani hivi usioisha kati ya bakwata na taasisi nyingi za kiisilamu wengi wakiituhumu bakwata kuwa imeanzishwa na kuwekwa na serikali ili kudhoofisha umoja na nguvu ya waisilamu na hata ukimsomoma ndugu yetu Mohammed said anaeleza hili jambo.
 
August,
Shida ni kuwa BAKWATA haikuundwa na Waislam.

Shida ni kuwa EAMWS ilivunjwa na serikali kuzuia isijenge Chuo Kikuu ili Waislam wabakie nyuma katika elimu kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni.
 
The Phy...
KIsa chote kipo hapo chini:
 
August,
Shida ni kuwa BAKWATA haikuundwa na Waislam.

Shida ni kuwa EAMWS ilivunjwa na serikali kuzuia isijenge Chuo Kikuu ili Waislam wabakie nyuma katika elimu kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni.

Sasa kwa nini msiungane kuivunja hiyo bakwata,ili mjenge taasisi imara moja,mana kinachoendelea sasa ni kuzidi kulalamika na kujitenga zaidi mama kila dhehebu la kiislam sasa lina taasisi yake.
 
Hapa ndipo shida yao unaanzia,kila kukicha wanatafuta makosa ya miaka ya 70 huko.
Waombe waoneshe hata mikakati yao tu maendeleo ndani ya jumuiya zao utakuta hawana.
Lakini kila siku wanalalamikia Serikali.
 
Hii idea ni nzuri sana kwamba hawa kina mzee Mohamed ambao ni wanazuoni wa kiisilamu wapandikize masnichi ndani ya bakwata kama sio kujipenyeza wao wenyewe ili waifumue na kuisuka upya kwa sura na namna itakayowaridhisha kwamba ni chombo cha waisilamu.
Ingawa naona ugumu katika hilo kwani sina shaka kwamba huko ndani ya bakwata kwa vyovyote iwavyo Kuna jicho la kuhakikisha bakwata inabaki kama ilivyo kwa manufaa ya Dola.

Na kama hivyo ndivyo basi hakuna chaguo jingine la kuleta suluhu isipokuwa kuandaa watu kimkakati na kuwapandikiza ndani ya bakwata ili waiue wakiwa humohumo.

Vinginevyo wakubali maumivu kuendelea kudhni kwamba Kuna kitu serikali itafanya kuleta hali tofauti ni kujidanganya
 
Huko Waislam walishapita miaka mingi sana.

Waislamu hawashughulishwi na BAKWATA baada ya serikali kutoa rukhsa ya kusajili taasisi nyingine za Kiislam.

Waislam wanaichukulia BAKWATA kama moja ya taasisi za Kiislam.

Hata pale wakati mwingine BAKWATA inapodai kuwa wao ndiyo wawakilishi wa umma wote wa Waislam wa Tanganyika.

Waislam hawajibu kukataa ugomvi.
Hubakia kimya.
 
Hapa ndipo shida yao unaanzia,kila kukicha wanatafuta makosa ya miaka ya 70 huko.
Waombe waoneshe hata mikakati yao tu maendeleo ndani ya jumuiya zao utakuta hawana.
Lakini kila siku wanalalamikia Serikali.
Dingi...
Hali haipo hivyo.
 
Sasa kwa nini msiungane kuivunja hiyo bakwata,ili mjenge taasisi imara moja,mana kinachoendelea sasa ni kuzidi kulalamika na kujitenga zaidi mama kila dhehebu la kiislam sasa lina taasisi yake.
Jiwe...
Neno dhehebu umelitumia sivyo na ndiyo sababu hata uliyoandika hayako sawa.

Hakuna taasisi ya dhehebu.

Waislam baada ya kuruhusiwa kusajili taasisi zao zinasajiliwa taasisi kwa ajili ya malengo ya maendeleo ya umma wote.

Waislam wenye fikra na mtazamo mmoja wanajikusanya wanasajili taasisi yao.

Madhehebu katika Uislam ni kitu kingine kabisa.
 
Back
Top Bottom