Captain 666
JF-Expert Member
- Nov 5, 2021
- 660
- 1,236
Waislam wenyeweNilimsikia Rais akihutubia Baraza la Eid alisikika akisema alipoingia madarakani tu Mufti alimjia na lundo la mafaili ya migogoro ya mali za Waisilamu.
Akasema kwa bahati mbaya nilipochunguza mafaili yale yana utata kwa kuwa wahusika wakubwa wa hizo sintofahamu ni wahusika wenyewe.
Naomba kwa mwenye uelewa mzuri kuhusu hii migogoro ya BAKWATA na wahusika anisaidie kuelewa vizuri ili tuwajue wahujumu wa mali za Waisilamu.
Pale Lumumba ni nyumba ya Muislam jamaa yake na Mohamed SaidMtaa wa Ufipa lilikuwa shamba la Bakwata
Ndo namna walivyoingia ule msikiti wa pale Mwenge ni wao wenyewe Bakwata wamempa mtu ubia matokeo jamaa kavunja msikiti woote kajenga frem za biashara bila kujenga sehemu ya kusalia. Aliyefanya madudu hayo katumbuliwa ila atakuja ajae atapeleka malalamiko Serikalini kuwa wamedhulumiwaKuna mahali niliwahi kwenda nikawaambia jamaa nataka.ninunue eneo including msikiti wakakubali.
Ndio maana umesikia hiyo kauli ya RaisKama ni hivyo kwa nini wanaisumbua Serikali si wasameheane tu au wadaiane wao kwa wao!!
Uturuki tatizo si dini kuwa na utajiri, uturuki geographically ipo kimkakati Sana,si ulaya si Asia, magharibi wanatamani zaidi iwe kisecular Kama ilivyokua huko nyuma,si unaona walimtumia sheikh kutaka mpindua Erdogan!!Yawezekana ilikuwa ni deliberate way kufanya wauze mali ili ushawishi upungue. Baada ya kutaifisha kuonekana kigumu, wengine wakinyang'anywa shule na hospitali wakaachiwa kidogo.
Ila nchi ambazo dini ina utajiri mkubwa huwa utengamano wake unasumbua kama ilivyo Uturuki
Engineer...Waislam wenyewe
Dini kuwa na nguvu sio tatizo kwa Uturuki, tatizo ni makundi ya kidini kuwa na utajiri. Gulenists wanakuwa na jeuri kwa kuwa ni matajiri wanamiliki uwekezaji mkubwa. Na haohao ndio walimsaidia Erdogan kuingia madarakani mwaka sijui 2001 ule.Uturuki tatizo si dini kuwa na utajiri, uturuki geographically ipo kimkakati Sana,si ulaya si Asia, magharibi wanatamani zaidi iwe kisecular Kama ilivyokua huko nyuma,si unaona walimtumia sheikh kutaka mpindua Erdogan!!
Napitia andiko lako kwa makini kisha ntakurehea mkuuEngineer...
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza jinsi EAMWS iivyovunjwa na serikali na nimeeleza sababu kwa nini ilivunjwa.
Hayo sitayalelza hapa.
Hapa nitaeleza jinsi serikali ilivyoshughulikia mali za Waislam na kuipa BAKWATA:
''Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Said Mswanya kwa kuamriwa na Rais Julius Nyerere akatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.[1]
Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao.
Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo la mgogoro wa EAMWS.
Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.
Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama.
Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza.
Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali ya Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam.
Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kutoa mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.
Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe.
Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu lililokuwa kikishirikiana na serikali na vyombo vyake vyote vya usalama.
BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa.''
Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyopotea mali ambazo BAKWATA leo inadai ni mali zao.
Hata hapo Kinondoni ulipojengwa msikiti mkubwa Mfalme Hassan wa Morocco hicho kiwanja pamoja na shule ys Sekondari ya Kinondoni vimejengwa katika ardhi ya EAMWS.
NYUMBA YA MAMA YAKE SHEIKH HAIDAR MWINYIMVUA BI.MWAMTORO BINT CHUMA NDIYO ILIYOBAKIA NA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKAPale Lumumba ni nyumba ya Muislam jamaa yake na Mohamed Said
Engineer...Napitia andiko lako kwa makini kisha ntakurehea mkuu
Ukimkamata mmoja tu ,Ndo namna walivyoingia ule msikiti wa pale Mwenge ni wao wenyewe Bakwata wamempa mtu ubia matokeo jamaa kavunja msikiti woote kajenga frem za biashara bila kujenga sehemu ya kusalia. Aliyefanya madudu hayo katumbuliwa ila atakuja ajae atapeleka malalamiko Serikalini kuwa wamedhulumiwa
Na kwa madudu hayo ya Bakwata ndo inapelekea kisiwe chombo kinachoheshimika, kukubaliwa na kupendwa wala kufuatwa na idadi kubwa ya waislamu hapa nchini japo ndo kinajinasibu kuwa ndo msimamizi wa waislam wote hapa nchini.
Kwakweli archbishop Tutu, maCCM baada ya kujiita chama cha Mapinduko yalijimilikisha viwanja vingi vya wazi hasa vile vilivyokuwa vya Mahakama ya Liwali, baadhi yao baadae yakavipiga bei hahah mfano wako unaelewaka zaidiBakwata na ccm ni kulwa na doto , bakwata Kaiga kwa ccm tabia hiyo.
Ndio maana alipomwomba afute kesi ya Mbowe wala hakuwaza akamwamuru DPP aifute mara moja. Hiyo ni baada ya mahakama kuu kuamua kuwa Mbowe ana kesi ya kujibu kwenye mashatska ya ugaidi.Nilimsikia Rais akihutubia Baraza la Eid alisikika akisema alipoingia madarakani tu Mufti alimjia na lundo la mafaili ya migogoro ya mali za Waislamu.
Akasema kwa bahati mbaya alipochunguza mafaili yale yana utata kwa kuwa wahusika wakubwa wa hizo sintofahamu ni wahusika wenyewe.
Naomba kwa mwenye uelewa mzuri kuhusu hii migogoro ya BAKWATA na wahusika anisaidie kuelewa vizuri ili tuwajue wahujumu wa mali za Waislamu.