Rais Samia, nimefurahi sana Taifa Stars Kufungwa ili Pesa zako zikasaidie hasa Watu wenye Uhitaji na siyo Goigoi wa Viwanjani

Ungekuwa we ndo prezida fedha ungezielekeza WAPI?
Ndugu yangu, Tz mambo mambo ya msingi ya vipaumbele ni mengi, manake hata vitu kama ' matundu ya vyoo, shule zetu nyingi ni changamoto, Sasa bado ni shida. Hivyo pesa zingine zingeleta tija zaidi kwenye maeneo kama hayo, badala ya kuzipoteza kwenye timu ambayo ni 'mbovu'.... Mie napita ....
 
Wewe unaamini Tanzania ni tajiri?

Ni maskini wa vipaji
Ni maskini wa uaminifu
Ni maskini wa ubunifu
Ni maskini wa vipaji - hii imesababishwa na vitu kadhaa:-
(a). Uwekezaji kwenye soka ni dhaifu sana kiasi kwamba wachezaji wengi ni matokeo ya ndondo cup si pishi la academy;

(b). Athari za utapiamulo na udumavu - wahezi wetu wengi wanatoka familia maskini ambazo kukua kwa walikutana na changamoto ya lishe bora - matokeo yake akili zao zikapata udumavu "stanting" - hii humtafuna MTU maisha yote (ndiyo maana mchezaji anapiga chenga afu anasahau kwa nukta kadhaa kuwa alipiga chenga mpk anakumbuka tayari adui kishampokonya mpira.

(c). Usimamizi - wachagua wa nani acheze ktk klabu huendekeza rushwa - hawachukui mtoto kwa ubora bali kwa kujuana, rushwa na upendeleo. Sasa muunda timu anapochagua wachezaji toka kwenye vilabu huchukua waliobora lkn vilaza wa mchujo wa kwanza.
 
1. Mahospitalini
2. Mashuleni
3. Vijijini
4. Miundombinu
5. Elimu Vyuo Vikuu
6. Kulipia Bima Watoto wa Tanzania
7. Kuwakopesha Watanzania kwa Riba ndogo ili Wajiinue Kimaisha

Niombee Siku moja nije kuwa Rais TZ.
ongeza, Wazee wasojiweza- kiucbumi, kiafya, kimazingira. nakuombea uwe Rais uje na Katiba mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…