Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Tunajua wanaopigia kelele Katiba mpya ni akina nani:makarai ya zege ya mafisadi.Wanadhani kupitia hiyo watapata nafasi ya kupenyeza agenda zao za kipuuzi.Sioni what we cannot do with the 1977 constitution as far as bringing development to our people is concerned and protecting our hard earned peace.Kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa.Hongera Rais Samia kwa msimamo wako.
Ndio waonakuweka mjini mpaka sasa ujue!
 
Halafu cha ajabu huyu mama alikuwa makamu mwenyekiti kwenye bunge la katiba, maana yake ni kwamba ama kipindi kile alikuwa haamini anachokifanya kuwa ni kwa maslahi ya nchi au sasa keshalewa madaraka kwa hiyo anafikiri kinachoweza kuendelea kumsaidia kumpa stimu zaidi ya ulevi huo ni kuendelea na katiba hii mbovu!

Huyu mama kafeli mapema sana kukataa katiba mpya, kiufupi hakuna hope yyote ya maana chini ya ungozi wake kama ataendelea kukaa kitu ambacho ni obvious!
Nimemsikiliza hotuba yake tone yake siyo ya kukataa katiba mpya
 
Muda utaongea
Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
 
Mbona kama hamjamsikiliza mama vizuri, Alivyosema sio mnavyotaka ionekane. Hata hivyo katiba mpya hatutapewa kama sahani ya matunda, Katiba mpya ni yakudai na ipo siku tutapewa. Katiba mpya ni ya muhimu, hata hao mawaziri wanaoinamisha inamisha vichwa wakisujudu hapo kama wapo kwenye nyumba za ibada kungekuwa na katiba mpya inayoainisha utu wa mtanzania yeyote bila kujali cheo wasingefanya hivyo.

Tumpe mama muda, tumsupport, sio rahisi ameingia jana leo aanze na katiba.

Naunga mkono hoja!

Lakini swala la katiba mpya awezi kujaribu kabisa.
 
Tunajua wanaopigia kelele Katiba mpya ni akina nani:makarai ya zege ya mafisadi.Wanadhani kupitia hiyo watapata nafasi ya kupenyeza agenda zao za kipuuzi.Sioni what we cannot do with the 1977 constitution as far as bringing development to our people is concerned and protecting our hard earned peace.Kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa.Hongera Rais Samia kwa msimamo wako.

Acha uchawi we jamaa!
 
Aliyekuwa na nia njema na nchi hii kuhusu katiba mpya alikuwa JK basi, huyo mwingine ni legacy ya Magu tu CCM ni ileile
Mazuzu ya Ukawa yaliacha kupambana mpaka mwisho yakakimbia vitani.. Matokeo yake ndio haya sasa..

Mazuzu ya Ukawa yalikimbia bungeni kisa serikali tatu zilipigwa pini. Leo hii wanalia lia
 
Mimi nilishajiandaa kisaikolojia tangu marehemu alipochaguliwa kuwa rais.
Nilijua Tu HAMNA KITU.binafsi sikuwa namkubali.hata Samia pia niseme ukweli bado hajanishawishi ila tumpe muda.
Na wewe utakuwa wapi?
 
Mbona hajasema kwanini tusubiri? nimefurahi kumbe kelele zimeshamfikia, sasa namwambia hizi kelele anazosikia hazitakoma mpaka Katiba Mpya ipatikane.
 
Mimi nilishajiandaa kisaikolojia tangu marehemu alipochaguliwa kuwa rais.
Nilijua Tu HAMNA KITU.binafsi sikuwa namkubali.hata Samia pia niseme ukweli bado hajanishawishi ila tumpe muda.
Basi tuungane tuongeze pressure nina hakika hata Wazanzibari wengi wataunga mkono.
 
Back
Top Bottom