Rais Samia: Nimeshindwa kufanya PhD kutokana na majukumu kuwa mengi

Rais Samia: Nimeshindwa kufanya PhD kutokana na majukumu kuwa mengi

Licha ya hivyo lakini yule alitwaliwa kabla ya siku yake alikuwa hafai. Ndo Mungu akamleta mama kuokoa jahazi.
Kama Mungu ndio alikuwa na mpangilio huo nina mashaka na IQ yake maana ule hauelekei kuwa mpango wake.
 
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema alijaribu kufanya Shahada ya Uzamivu lakini kutokana na majukumu mengi ameshindwa huku akisema ataimalizia baadaye.

Mkuu huyo wa nchi amesema hayo leo Alhamishi Januari 27, 2022 wakati wa mahojiano maalumu yaliyorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) yaliyogfanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Rais Samia ambaye leo anaadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, ameeleza mambo mbalimbali tangu alipozaliwa mpaka kuwa Rais huku katika safari yake ya elimu akisema ameishia kwenye shahada ya uzamili (masters) akibainisha kuwa alikuwa na matarajio ya kufanya PhD lakini majukumu yamezidi.

“Nilijaribu kufanya PhD lakini ukweli ni kwamba pilika ni nyingi nimeshindwa, sijui niseme nimeshindwa au nitaimalizia baadaye, sijui. Labda nitaimalizia baadaye” amesema Rais Samia

Amesema kuwa katika hatua yake ya elimu ya awali mpaka kidato cha nne amesoma shule zisizopungua 10.

“Kuanzia darasa la awali mpaka nimefika kidato cha nne nimesoma shule kama 10 hivi, hiyo ni kwasababu baba yangu alikuwa mwalimu hivyo alikuwa anahamishwa vituo vingi vya kazi, akihamishwa name niko nyuma yake” amesema Rais Samia


Aajiriwa akiwa mtoto
Rais Samia ambaye leo anatimiza miaka 62 amesema kuwa alipata ajira yake ya kwanza lakini kabla ya kuanza kazi alirudishwa nyumbani kwa kuwa bado alikuwa mtoto.

Amesema alipata ajira ya karani masijala mwaka 1977 wakati akiwa na umri wa miaka 17 hivyo ikamlazimu kurudi nyumbani kusubiri kwa muda.

“Niliajiriwa nikiwa mdogo sana mwaka 1977 nikiwa na wa miaka 17 hivi na nakumbuka nilipokwenda kwenye ajira mara ya kwanza wakasema nenda nyumbani, hapa tutafanya child labor kwa hiyo rudi nyumbani, nikarudi nyumbani nikakaa nyumbani miezi sita hivi halafu ndio wakaniita tena”

Amesema kuwa ingawa alipata kazi hiyo lakini aliona kuwa nafasi hiyo hamtoshi hivyo kuamua kwenda kuongeza elimu.

“Niliajiriwa mwaka 1977 nikiwa karani masijala lakini nilikuwa najiona kabisa pale sio mahala pangu, kwa sababu nilikuwa nafanya zaidi kuliko niliowakuta sawasawa na maofisa, na ndicho kilichonifanya niondoke nikaongeze elimu na baada ya kuongeza elimu nikaajiriwa na Shirika la Chakula Duniani, nikafanya kwa miaka tisa” amesema

Jina la Bibi Mchele lampa ushindi ubunge

Akielezea mwanzo wa kuingia kwenye siasa na kilichompo ushindi wa ubunge wa viti maalumu, Rais Samia amesema jina la Bibi Mchele alilopewa wakati akifanya kazi kwenye Shirika la Chakula Duniani (WFP) lilimpa umaarufu kwa wananchi na kumfanya akubalike kwenye ulingo wa siasa.

Amesema kutokana na kufanya kazi kwa ukaribu na wananchi na kuzijua changamoto zinazowakabili alivutiwa kuingia kwenye uwakilishi ili kuwasemea wananchi na kuisimamia Serikali.

“Mwaka 2000 ndio nilipata mawazo ya kuingia kwenye siasa, ukiniuliza kwanini nilikuwa na sababu moja tu, nilikuwa naangalia Baraza la Wawakilishi linavyoendelea, wakati ule upinzania ulikuwa ndio unapamba moto kwa hiyo nikaamua kuingia ili nami niingie kwenye upambanaji” amesema

“Niliamua kuingia niisimamie Serikali na kujibu hoja kwa sababu nilishafanya kazi na wananchi kupitia NGOs kwa hiyo changamoto zote nazijua, sasa unakuta waziri anaulizwa anachojibu ni tofauti na kililichoko kwa wananchi ndio nikaamua niingie kujibu hoja au kupeleka hoja za wananchi”

Amesema kutokana na uhaba uliotokea wakati akifanya kazi Shirika la Chakula Duniani (WFP) alifanya jitihada za kuomba chakula na kupata mchele, samaki na mafuta ya kula ambavyo walivigawa kwa wananchi huku akipewa jina hilo la Bibi Mchele.

“Nilikuwa sijui mtu anaingiaje, nikauliza nikafahamishwa nikajaribu, nikaenda Kusini ya Unguja nikajitambulisha wengi walikuwa wananijua Bibi Mchele kwa sababu wakati nafanya kazi Shirika la Chakula Duniani (WFP) kulikuwa na tatizo la wadudu kuvamia mazao, kwa hiyo kukawa na uhaba wa chakula lakini kwa sababu niko kule nikafanya jitihada za kuomba chakula kwa ajili ya wananchi”

“Tukapata mchele, samaki na mafuta ya kupikia kwa wingi tukagawa kwa wananchi, kwa hiyo wakanipa jina la bibi mchale, nilipokwenda kujitambulisha wakawa wanasema bibi mchele tunampa, kwa hiyo nikaibuka kuwa mshindi kwenye viti vya wanawake ndio nilipenyea huko” Amebainisha
Mwananchi 27/01/2022
😀 😀 Aende kwenye kile chuo Cha ccm akachukue za michongo.
 
😀 😀 Aende kwenye kile chuo Cha ccm akachukue za michongo.
Chuo cha CCm si ndiyo chuo cha nchi!! Maana CCm ipo madarakani...hahap
Anaonesha kabisa shule kwake ilipita kushoto ,alikuwa analazimisha tu ,na kukabidhiwa kitengo ...
Tujifunze pia hakuna uhusiano kati ya shule kubwa na mafanikio ya maisha, na hakuna uhusiano kati ya shule kubwa na madaraka makubwa serikalini....what's matters is voters !
 
Hiyo ni fursa kwa wakuu wa vyuo....
Hapo wachumia tumbo wameshasikia wanajiandaa kumtunuku uyo chui jike PhD ya mchongo

Wanasiasa wanapenda PhD ila kusoma na ku-practise walichojifunza hawawezi
 
Kwa hiyo unataka kusema kila aliyesoma ualimu alifeli kwanza....
Hata Magufuli alikuwa kilaza ,alifeli mtihani wa kidato cha sita ,akakosa credit za kwenda Chuo kikuu,akaenda Ualimu (Mkwawa )
 
Atuoneshe vyeti vyake vya elimu ya sekondari kwanza, huwezi tamani vitu vikubwa ilihali vitu vidogo vinakutoa jasho..
Mkuu katika maisha kikubwa ni ufahamu na elimu ni sehemu ndogo ya ufahamu. Ufahamu hupatikana katika mazingira anyoishi mtu.
Tazama vitoto vikicheza utagundua katika watoto kuanzia wawili kuna mmoja anatenda kama kiongozi. Tambua huyu mtoto kiongozi ana ufahamu mkubwa kuliko hao wengine na sio kuwa kasoma kuliko wengine na hivyo kutambua vitu muhimu.
Hivyo, elimu ya darasani sio kigezo pekee bali ikiambatana na ufahamu ndio huwa vema zaidi.
Basi ni vema kupima mtu ufahamu wake kwa kuhusisha na matendo yake.
 
Kwa hiyo Chui jike ni Form Four Failure (FFF) ?
Huyu Samia alisoma elimu ya watu wazima tu aache kudanganya umma,miaka 17 aliyosema alikuwa anaanza kazi,enzi hizo ndio ilikuwa ya kumaliza darasa la 7 maana shule tulikuwa tunaanza la Kwanza tukiwa na miaka 9-11,ukiwa mfupi ndio usisogelee hiyo shule,Sasa Samia shule hiyo dalasa la Kwanza mpaka form four,aliisoma akiwa na miaka mingapi?
 
Hili lilikuwa tangazo kwamba natafuta PhD. Watafuta fursa wakaiona na kuanza kuuunda magfanikio hadi PhD
 
Atuoneshe vyeti vyake vya elimu ya sekondari kwanza, huwezi tamani vitu vikubwa ilihali vitu vidogo vinakutoa jasho..
Vidogo ni vipi? Hebu muache bi mchele kumbe alianza kuisaidia jamii kitambo sana.
Kongole
 
Back
Top Bottom