Rais Samia: Sasa Tanzania tumeuza (Bandari), wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?

14 Julai 2023
Dar es Salaam, Tanzania

Wahariri wa Vyombo vya Habari Tanzania Wakiwakaba Koo Watendaji wa Serikali Sakata la Uwekezaji Bandari


Source: The Chanzo

Serikali ya Kenya yaruka kimanga, ahadi ilizotoa kwa Dubai kuhusu bandari

09 July 2022



CHARLES WASONGA: Serikali Ijayo Ifutilie Mbali Mpango Fiche Wa Ubinafsishaji Bandari Zetu​


NA CHARLES WASONGA

SERIKALI inafaa kuondoa usiri unaogubika mpango wake wa kubinafsisha au kuuza mali yoyote ya umma ili kuondoa uwezekano wa maswali kuibuliwa kuhusu uwepo wa hila.


Hii ni baada ya wanasiasa wa mrengo wa Kenya Kwanza kudai kuwa, serikali chini ya Rais Uhuru Kenyatta, imeuza bandari za Mombasa, Lamu na Kisumu kwa kampuni moja kutoka Dubai, Umoja wa Milki za Kiarabu (UAE), kisiri.

Wakiongozwa na kiongozi ANC Musalia Mudavadi, wanasiasa hao walidai Katiba na sheria husika hazikufuatwa katika mpango huo ambao ulikamilishwa mnamo Machi 1, mwaka huu.

Lakini Waziri wa Fedha Ukur Yatani, ambaye walidai ndiye alitia saini mpango huo na kampuni ya Dubai Port World, alikanusha madai ya wanasiasa hao ambao ni wandani wa Naibu Rais William Ruto.

Kulingana na waziri huyo, mpango uliopo ni wa ubinafsishaji wa sehemu za kupakia konteina katika bandari hizo, ambao ulianza 2015 lakini haujakamilishwa.

Sasa maswali yanayoibuka ni je, mbona ni wakati huu ambapo Waziri anatoa maelezo finyu kuhusu mpango huo baada ya wanasiasa kuibua maswali kuuhusu?

Pili, mbona serikali haikutangaza zabuni kuhusu mpango huo katika vyombo vya habari vya humu nchini na vile vya kimataifa kwa mujibu wa sheria za ununuzi na uuzaji wa bidhaa za umma, 2005?

Mbona Serikali haikukusanya maoni kutoka kwa wananchi kuhusu pendekezo hilo, inavyohitajika kwa mujibu wa kipengele cha 118 cha Katiba ya sasa?

Bw Yatani hakutoa majibu sahihi kwa maswali kama haya na mengine wala kusema iwapo suala hilo lilijadiliwa na kupitishwa katika baraza la mawaziri.

Bandari za Mombasa, Lamu na Kisumu ni mali ya Wakenya ambayo husimamiwa na serikali iliyoko mamlakani kwa niaba yao.

Kwa hivyo, endapo kuna mipango yoyote ya kuuza au kuzibinafsisha, kwa sababu yoyote ile, wananchi wanafaa kujulishwa.

Njia mwafaka ambayo kwayo wananchi wanaweza kuhusishwa ni kupitia asasi ya bunge ambako kuna wawakilishi wao.

Kwa sababu mkondo wa kisheria haukufuatwa katika mpango huo kati ya Serikali na Dubai Port World, naomba serikali ijayo iufutilie mbali
 
Hatudanganyiki .
 
Mbona ccm sio waelewa!!?
Hakuna mtanzania ambaye hataki uwekezaji nchini. Wenye nchi wanataka uwekezaji wenye tija kwao na kwa vizazi vyao vijavyo. Jaribuni kulegeza akili zenu enyi ccm
 
Samia ni Rais mwanamageuzi sio Rais wa kukariri ujinga ujinga kisa tuu sijui wazee sijui upuuzi gani hakuna nonsense..

Kwanza amesema hakuna kuogopa kubadili muelekeo wa Nchi kama Kuna manufaa regardless of maumivu ,mtazoea tuu 🔥🔥
 
Mama siziache bandari za watu , usipokuepo wapo watakao kuja watajua cha kufanya , kwamba Dubei kuweka bendera ya Kenya basi wanataka kuuza bandari zao ?
Nakushauri hachana na hili jambo kwanza alitawezekana , pili ukilaendele likomalia utajijua , naishia hapa , asema Bwana, chukua maneno ayo machache utaki acha ,
 
Ndio yupo lazima afanye kwani unampangia wewe kama nani?
 
Kile kiti kina shida sana. Watu wanakataa Terms za mkataba, hawakatai kuwekeza. Hatuoni tija katika terms zile.

Sijui ni kupigwa upofu au kujipiga upofu.
Sasa kati ya Tanzania na Dubai,unazani nani mwenye shida ya uweekezaji!? Mwenye shid lazima uwe mpole,na ridhika utakachopewa, hutaki kaa na li Bandari lako!!
 
Mkuu, Safi sana kwa kuleta hii habari Katika muda muafaka kabisa. If possible, naomba uufungulie uzi wake huku ukim- quote Sa100 ili kuweka kumbukumbu sawa
 
Hapa tuu ndio Huwa namkubali Rais Samia,haijalishi makelele yakoje ila kama jambo Lina Tija anasomga mbele..
Huwezi sema puuza makelee ,wananchi wakiamua kesho hayupo ofisini , nyie ndo wapumbavu mnaomjaza upumbau rais ,naye kufanya upumbuvu kupitia ushauri wenu wa kipumbavu wenda kwa kujua au kutojua, pumbavu
 
Kwahiyo akaongea na wajomba zake waweke picha ya bendera ya Kenya ili apate cha kusema
 
Mkataba una shida gani?
Shida siyo uwekezaji, huko sisi tumeshapita. Si mnaona tunavyo furahia uwekezaji pale Simba na Yanga? Na timu zinafanya vizuri Sababu ya uwekezaji. Lakini tukiambiwa huyu mwekezaji atadumu milele na hakuna mwekezaji mwingine anaruhusiwa bila idhini ya mwekezaji aliyepo unadhani patakalika? Shida ipo kwenye MKATABA.Toeni utata, tusonge mbele.
 
Huwezi sema puuza makelee ,wananchi wakiamua kesho hayupo ofisini , nyie ndo wapumbavu mnaomjaza upumbau rais ,naye kufanya upumbuvu kupitia ushauri wenu wa kipumbavu wenda kwa kujua au kutojua, pumbavu
Wewe mpumbavu amua tuone,ni nyie wajinga wachache ndio mnahangaisha na ndio maana mnapuuzwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…