Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Acha tu ampe ilo gari,hata akiamua kumpa Bombadier moja ni sawa tu.Aliyenacho ndiye atakayeongezewa.Nyie wazee wadar'slam endeleeni kupigwa vikumbo kwenye daladala.
 
Muwe mnaelewa. Hilo gari halijanunuliwa kwaajili ya mzee bali lilikuwepo
 
Kwani yeye mwinyi hana hiyo hela ya kununua Benz? Au hajui km anatakiwa kununua Benz imrahisishie ufasiri? Mambo mengine yanakera sana.
Usikereke kaka... ipo kisheria na kumbuka ndio hazina tulizobaki nazo za viongozi tulionao , Mstaafu Mwinyi anauwezo hata yeye angenunua kwa pesa yake ila kwa Heshima na kutambua mchango wake ni vizuri akinunuliwa .. Ni vzr kumuenzi mzee wetu maana hawa wazee soon watabaki Historia...
 
Mnasahau mwendazake aliwape majumba ya kifahari hawa wastaafu wote....Mama amesema yeye na mwendazake ni walewale tu....nyumba wanazo walipewa na mwendazake, mama kaona naye awape magari, mwingike awamu ya saba atawapa mitumbwi...
 
Nimwonee wivu Mwinyi? Ha ha ha najifananishaje namimi?

Sijakataa kununuliwa benzi, shida gharama ni kubwa

Kwani hakuna benzi za bei ya chini?

Japo naaamini aliyetoa mwada mwongo kwenye gharama
Ile gari haizidi milioni 50 hata ikizidi kwa kuwa ni brand new haifiki milioni 100 .

Nyie watu hata angepewa cake ya Tsh 100,000 pale mngetoa povu tuu kwanini apewe zawadi "cheap " kiasi kile.
 
Milioni 450 zawadi katika nchi ambayo uchumi unaporomoka?
 
Huyu mzee pensheni yake kwa mwezi ni 80% ya mshahara wa rais. Kajengewa jumba la kifahari na serikali, leo kapewa gari la kifahari. Watumishi wa umma wakiomba nyongeza za mishahara wanaambiwa wasubiri.

Nchi ina wazalendo na wajalendo.
Na kuna mabunge yasio na vyama yanakula tu hela, ila watumishi uchumi umeshuka....
 
Kwani mwanae kule Zanzibar anasemaje?
 
Hivi Mwinyi anakosa milioni 400 ya kununua gari?
Zawadi ni zawadi hata kama unauwezo wa kuinunua mwenyewe.. cha muhimu ni kumjali mtu akiwa angali hai, sio anaondoka ndio tunaanza kushadadia mitandaoni kwa mazuri ya mtu husika kwa upande wangu huyu raisi Mwinyi alistahili zaidi lakini kwa uwezo wetu Mama akaona aishie kwenye hiyo Benz sio mbaya sana..
 
Hiyo zawadi ameitoa kupitia mshahara wake, au ni kupitia kodi za watanzania? Na hiyo 80% anayopokea kila mwezi haimtoshi kununulia gari dogo?

Huyo Mzee alimuomba hilo gari, au ni mihemko tu ya Rais Mpya kutaka kujitutumua?
Kwahiyo ukiwa na uwezo wa kununua kitu huwezi kupewa zawadi? Wewe mshamba wa wap? Umeona wapi zawadi mpaka uombe?

Hizi roho za kwanini mtakufa na vijiba vya roho.

Ameshapewa sasa andamana
 
Na kuna mabunge yasio na vyama yanakula tu hela, ila watumishi uchumi umeshuka....
Na kuna mwengine kang'ang'ania ubunge wakati chama chake hakitambui matokeo ya uchaguzi uliyompa yeye ushindi wa ubunge, kweli ubunge mtamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…