Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Si rais tu, viongozi wote waandamizi wanapeana maghorofa wakistaafu sasa hivi. Huu ni utaratibu waliojiwekea lakini sisi wapiga kura hatuambiwi.
Si huwa mnaambiwa mjitokeze kupiga kura, au hilo haliwatoshi?.
 
..as long as sio MUUAJI mimi nimeridhika.

..mabadiliko hayaji kwa mara moja.

..huwezi kutoka kwenye utawala wa KIKATILI halafu ghafla ukaingia kwenye moja kwa moja kwenye demokrasia, rule of law, na utawala bora.
Nyota njema inaonekana asubuhi. Sasa hivi watu wengi wanamkubali na wana matumaini makubwa nae. Lakini siku zinavyoenda bila mabadiliko yeyote ya maana ndio hayo matumaini yatazidi kufifia. Watu wengi tuli appreciate kuwa anatuambia ukweli kuhusu hali ya uchumi, lakini hili la zawadi ya Benz linampunguzia.
Waswahili wanasema kuwa samaki mkunje angali mbichi. Mambo ya utawala wa haki na demokrasia hayatakiwi subira maana kuna watu wanaumia. Kitendo cha DPP kutangaza kuwa hana nia kuendelea na kesi za watu kama Mdude Nyangali kinge mjengea sana credibility. Leo angesema wanambadilishia gari badala ya kuwa ni zawadi ingepokelewa vizuri sana katika mazingira ya sasa.

Amandla...
 
Miaka 96 amepewa benz

Kweli mwenye nacho uongezewa
 
Vipi yule mshamba wenu alikuwa akipita barabarani akigawa kodi za wananchi kama pipi huku mkimpongeza?

Mpongezeni na huyu

Tanzania imebarikiwa maliasili, ardhi na maji ya kutosha tatizo ni kuwa haijawahi kipata rais mwenye vision.
JPM alikuwa Rais mwenye maono,simaanishi kwamba hakuwa na kasoro, hata pesa alizotoa ,ni kwa watanzania wenye shida kweli.
Na hilo si la ajabu kwani kuna watanzania wangapi ambao kila ijumaa wanatoa misaada kwa wtanzania wenzao?
kwanini iwe ajabu kw Rais kusaidia wananchi wake? au kwa sababu u don't fall into that group?
 
Hiyo benzi ya chini sijui ataitumia wapi maana pale mikocheni na hizi mvua lazima pafurike, muulizeni Extrovert gari ya mjerumani ikikutana na maji inakuaje, bado mashimo, wangemfanyia modification vieti iwe na kingazi cha kushukia🤣
Hahaha hio tunaisubiria baada ya masika moja!
 
Nchi yetu ni maskini sana bila kupindisha maneno.
Watu hawana maji.
Clinics hazina vifaa vya kutosha.
Baadhi ya mashule hali ni yakutisha.
Baadhi bara bara hazipitiki!
Miundo mbinu hapa Dar sio mizuru.
List ni ndefu halafu unasema nina mawazo ya kimaskini!
Kwa nini wengine waishi maisha ya kifahari kwa kodi zetu wakati wengine maji kwetu ni shida!
Utaambiwa huwezi kifanikiwa kwa kuchukia matajiri 😂😂😂!!!
Pambana na hali yako mzee
 
Inachezewa sana kivipi we jamaa.. Mbona unakuwa na roho ya kimaskini sana?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Zawadi ya Ml 450 kwa mtu alie simamia ustawi wa taifa letu.. tena ukiangalia hata kwenye baadhi ya sarafu kuna sura yake hiyo tsh ml 450 bado ni ndogo sana Ndugu yangu
Jamaa anashangaa zawadi ya 450M wakati kwenye benki ana sarafu yenye sura zake zaidi ya 450M katika thamani ya pesa aliohifadhi!
 
Kama itakuwa hivi, siku si nyingi nitakuwa mpinzani
Kinachowatesa wabongo wengi ni roho ya kwanini tu! Sio kingine yani...

Nimewaza sana hivi kwanini watanzania wengi ni vigeu geu namna hii. Nikagundua kumbe kiroho cha kinyongolilo ndio kinawatesa wengi! Hawana furaha flani akipata
 
thamani yke ni kituo kimoja cha afaya anaenda kumpa huyo mzeee mmoja ambaye hata hivyo kikatiba bado serikali inamlea
 
Juzi amesema uchumi wetu umeshuka kutokana na Janga la Corona, binafsi nilitegemea serikali ingejikita katika matumizi ya Msingi tu kuliko Matumizi ya anasa ya namna hii yasiyo na tija wala manufaa kwa nchi hii.
Kwahiyo babu kupewa gari we unaona matumizi ya anasa! Unasahau kuwa babu ni Rais mstaafu aisee
 
Back
Top Bottom