Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Pengine tumpe mama nafasi afanye kazi yake. Hii gari angeweza kumpa kimya kimya. Mzee Mwinyi is entitled. He is the property of the State. Why mourning for this little gesture of appreciation for his part in leading the country?
 
Kama n kweli basi tuna "RAHISI" na siyo RAIS

mzee wa Miaka 90+ unampa gari la mil 450 s alisema Corona imeyumbisha uchumi Sasa hii 450 mil kaitoa wapi

Hyo 450 M inalipa malimbikizo ya watu wangapi wanayodai

Mwinyi anamshahara au marupurupu Mengi Bado ana watoto wenye mamlaka huko visiwan

POLE MAMA TANZANIA SIKUMPENDA MAGUFULI LAKIN HUYU DAAAH
 
ameamua kumpa zawadi ya benzi la chinichini ambalo thamani yake ni milioni 450 tsh ,hii nchi inachezewa sana
Hayo ma Benz yalikuwepo kama matano hivi. Yalinunuliwa wakati wa mkutano wa SADC ﹰkwa ajili ya kuwabeba wakuu wa nchi za ﹰSADC ﹰkama sikosei. Hivi sasa yatakuwa yamebaki manne kama mwinyi kapewa moja. Sina taarifa sahihi sana.
Hata mimi niliwahi kumuomba Kabudi anipatie moja baada ya mkutano wa SADC kuisha ila akaninyima 😆😀
 
Ilianza kuchezewa Na Jiwe,kwani unafikiri zile VX- R zilizokuwa Kama mchanga kwenye misafara ya Jiwe ni sh ngapi moja? Rejea kashfa ya DED Geita
 
Mzee anatakiwa aendeshe Benz ya chini chini, gari za juu zinampa shida.
 
Shida iko wapi? Kwani hana hena binafsi ya kuweza kumpa zawadi mzee wetu? Acha majungu kijana. Rais naye ana maisha binafsi nje ya urais.
 
Kwanza, usahihi wa taarifa hii haujulikani.

Lakini kama ni kweli, hela kiasi hicho ingekuwa na matumizi bora zaidi ambayo hata mzee Mwinyi angefurahi kujua kwamba hela hiyo imefanya kazi ya manufaa zaidi kuliko kuimwaga tu hovyo namna ile.

Hawa viongozi mbona siku hizi wanapenda sana kushindana katika kutapanya hovyo mali za waTanzania?

Hela kiasi hicho ingenunua madawati mangapi?
 
Hivi mnajua wale wageni wa SADC zile gari zote ziliagizwa mpya 0km na kuwachukua airport na kuwarudisha baada ya hapo zililala tu.inawezekana kampa moja kati ya zile.
 
wastaafu wana mgao wa magari kila kipindi fulani.

huyo mzee na wenzake wana nissan patrol v8,labda angesema ameamua kumbadirishia ingesound better.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…