Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Kabisa mkuu!

Sasa hivi kwa mujibu wao mambo yote ni safi! Kila tatizo nchi hii ameondoka nalo Magu na sasa tuko nchi ya maziwa na asali na ccm ni mbele kwa mbele.
[emoji23][emoji23][emoji23]
Hii ndo logic ya hawa watu:

Kigogo anamponda sana Samia kule Twitter.

Salari Silipu wa humu naye anamponda kiaina Samia. Anasema Mama ni failure!

D31FD549-D97C-453C-8015-F1A20D4DA6F4.jpeg


Hata Tundu Lissu naye keshamponda Samia tokea awe Rais.

Kwa akili za hawa watu, yeyote yule sasa hivi amkosoaye Samia, kwao ni MATAGA.

Kwa hiyo ina maana:

1] Kigogo, Salari Silipu, na Lissu nao ni MATAGA?

2] Samia ni malaika. Ni genius. Hakosolewi.

3] Ukimkosoa tu kwa lolote lile, unaambiwa una chuki.

Hizo ndo logic za hawa viumbe walio chini ya nyumbu. Niamini ninaposema nimehitimisha kuwa nyumbu wana akili nyingi zaidi kushinda hawa watu!
 
Kwanza, usahihi wa taarifa hii haujulikani.

Lakini kama ni kweli, hela kiasi hicho ingekuwa na matumizi bora zaidi ambayo hata mzee Mwinyi angefurahi kujua kwamba hela hiyo imefanya kazi ya manufaa zaidi kuliko kuimwaga tu hovyo namna ile.

Hawa viongozi mbona siku hizi wanapenda sana kushindana katika kutapanya hovyo mali za waTanzania?

Hela kiasi hicho ingenunua madawati mangapi?
Bwana we! Hamna gari ya million 450 hapo! Hicho kigari kikizidi sana ni 100M kamili sababu serikali inaingiza gari Tax free
 
Acha kupotosha wewe, ile ripoti ya CAG dhidi ya upotevu wa 1.5 trilioni iliweka wazi kila kitu. CCM mnanufaika na nini kutetea uovu?
Mimi nnaandika vitu vilivyopo unaleta story za upotevu wa tillion 1.5!!!

Huna habari ilipanda ikafika 2.4??
 
Kinachowatesa wabongo wengi ni roho ya kwanini tu! Sio kingine yani...

Nimewaza sana hivi kwanini watanzania wengi ni vigeu geu namna hii. Nikagundua kumbe kiroho cha kinyongolilo ndio kinawatesa wengi! Hawana furaha flani akipata
Issue siyo kupata wala kukosa. Kuna vitu vinakuwa too much aisee.

Wakati watu wengine, wanapigwa sound wengine wanatafuna.

Mwinyi hapo alipo ni ni nusu Rais kimaslahi, mwanaye kapewa Urais Zanzibar ( tena kasimikwa kijeshi kwa ubabe, na mwanaye mwingine ni viti maalumu kama alivyo mtoto wa Samia )

Huyo huyo Mwinyi alipewa bonge la jumba na Magu mwaka jana.

Sasa wakati huo huo, vijana mnaambiwa mjiajiri yaani, watumishi wanaambiwa uchumi mdogo na wazee wanaambiwa pesa hakuna.

In short, credibility inashuka kuwa na ndimi mbili.

Anyway, hatujui thamani ya hilo gari wala hatujui kama lilikuwepo ikulu au limenunuliwa.
 
Issue siyo kupata wala kukosa. Kuna vitu vinakuwa too much aisee.

Wakati wengine, wanapigwa sound wengine wanatafuna.

Mwinyi hapo alipo ni ni nusu Rais kimaslahi, mwanaye kapewa Urais Zanzibar ( tena kasimikwa kijeshi kwa ubabe, na mwanaye mwingine ni viti maalumu kama alivyo mtoto wa Samia )

Huyo huyo Mwinyi alipewa bonge la jumba na Magu mwaka jana.

Sasa wakati huo huo, vijana mnaambiwa mjiajiri yaani, watumishi wanaambiwa uchumi mdogo na wazee wanaambiwa pesa hakuna.

In short, credibility inashuka kuwa na ndimi mbili.

Anyway, hatujui thamani ya hilo gari wala hatujui kama likikuwepo ikulu au limenunuliwa.
Lakini reason behind iko valid! Mzee amechoka kupanda truck kama V8 inataka uwe na stamina! Ila gari la chini anadumbukia tu. Bei ya gari sio halisi mtoa mada ame overstate!
 
Lakini reason behind iko valid! Mzee amechoka kupanda truck kama V8 inataka uwe na stamina! Ila gari la chini anadumbukia tu. Bei ya gari sio halisi mtoa mada ame overstate!
Wanaye wana uwezo kamili wa kumnunulia.

Wala siyo kwamba huyo mzee ni hohe hae anateseka kama wazee wetu.
 
Nadhani angepewa Quran ingefaa zaidi mzee wetu azidi kuwa karibu na Muumba wake.
 
Mercedes Benz kama hiyo ni milioni 100 tu?
Hio haijaoneshwa kote ila kimekaa kama C class tu jinsi navyokiona sasa kuna C-Class ya million 450??? C-Class ya mwaka 2021 ni U$D 42,000 and im pretty sure hiyo aliyopewa mzee ni toleo la 2020 kama si 2019.
 
Mzee Mwinyi aache kunesa nesa kwenye shock absorber za V8 kwa raha zake, akaingie kwenye gari ambalo diff linagonga mabonde.

Matumizi mabaya tu ya hela.
 
Samia anamwambia mzee Mwinyi, Kama "V8 haikufai basi chukua Benz" .

Ni sawa na kauli ya
Kama "Mkate haukufai basi kula keki".

Samia ameanza kuonyesha dalili za ubadhirifu na utapanyaji wa mali ya umma, Asipowekewa breki huyu anaweza kugawa hata rasilimali za nchi hii kama njugu!

Hebu tuwe wakweli, Mwinyi ameshindwa wapi kujinunulia gari inayomfaa?.

Nani ana uhitaji zaidi, Mwinyi au watoto ambao bado wanakaa chini kwa ukosefu wa madawati!

Ifikie Muda hawa viongozi wa serikali waone aibu, siyo kwa sababu wanamiliki hazina ya nchi basi wanagawana tu kama pipi!

Samia hapa kazingua sana!
 
mimi nnaandika vitu vilivyopo unaleta story za upotevu wa tillion 1.5!!!

huna habari ilipanda ikafika 2.4??
Kwa taarifa yako humo ndani yake (1.5 to 2.5 Trilion) ndio kuna hayo matumizi binafsi yenye KICHEFUCHEFU ya Rais, kama hujui kitu funga masaburi tu Mkuu. Usizidi kutukumbusha machungu ya Mwendazake.
 
Hekima ingetumika na hii ingetolewa bila matangazo. Kwa mtu anayepata pensheni ya mamilioni, nyumba kajengewa, watumishi na mafaa mengine, na hata mtoto wake ni rais.....jamani. Mwataka Mtanzania asiyeweza hata kulipia luku ya 2,000 watoto wake usiku huu walala gizani, asemeje? Kuweni na huruma na hekima na msichukulie Watanzania kwa vile hawasemi, kuwa hawawezi kubadilika! Sina kinyongo chochote na mzee rukhsa.
 
Halafu watu hawahawa wanawaza kuwafukuza wamachinga wanaotafuta mlo wa siku eti wanachafua miji.

Unamwambia mzee Mwinyi mtu mwenye miaka 96 kuwa V8 halikufai chukua benzi, lakini unaenda kumtisha mtu anayehustle kupata ugali wake wa kila siku kumvunjia kibanda chake cha kupata rizki

Ajabu sana hii
 
Hio haijaoneshwa kote ila kimekaa kama C class tu jinsi navyokiona sasa kuna C-Class ya million 450??? C-Class ya mwaka 2021 ni U$D 42,000 and im pretty sure hiyo aliyopewa mzee ni toleo la 2020 kama si 2019.
issue si gharama, issue ni principle. Yaani mzee rukhsa hajiwezi hivyooo kiasi anataka usafiri unaomfaa, hamudu?
 
Baada ya kuzindua kitabu chake Jioni ya leo Rais Samia amesema anamshukuru Mungu kwa kumpa Mwinyi miaka 96 na sasa anamwombea afike 100

Pia amesema anaona Mzee Mwinyi akipata shida ya kupanda gari alilonalo na ameamua kumpa zawadi ya benzi la chinichini.

USSR

=====

“Nakushukuru sana Mzee wangu Rais Mstaafu Mwinyi kwa kunikaribisha kuzindua kitabu cha simulizi ya maisha yako, nampongeza Mzee Mwinyi kwa kuamua kuandika kitabu ambacho sio tu kitawasaidia Watanzania na Dunia kumfahamu pia kina historia ya Tanzania” Rais Samia

kwenye uzinduzi kwa kitabu cha Mzee Mwinyi Dar es salaam leo

“Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi inaenda sambamba na kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa, tunamtakia kila la kheri wakati anatimiza miaka 96, tunamuomba Mungu akutunze ufike miaka 100 na zaidi ili tuzidi kuvuna hekima na busara zako” Rais Samia

“Nimemuandalia zawadi Mzee Mwinyi, kwa kutimiza umri wa miaka 96 leo, nimekuwa nikiona usumbufu anaoupata akiwa anapanda na kushuka kwenye Gari lake, kwa niaba ya Serikali Mzee wetu leo tutampatia Benz la chini ambalo litampa raha kwenye Safari zake” Rais Samia
View attachment 1777949
View attachment 1777889
issue si gharama, issue ni principle. Yaani mzee rukhsa hajiwezi hivyooo kiasi anataka usafiri unaomfaa, hamudu?
Yani swali la kitoto sana ilo yani kupewa boxer kama zawadi kwenye birthday yako inamaana huwezi kununua? Tupunguze munkari kwenye petty issues kama hizi mama katoa anachojisikia kinamfaa mbona mwingine kapeleka Airport na mbuga kabisa kwenye alipotokea!!

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Yani swali la kitoto sana ilo yani kupewa boxer kama zawadi kwenye birthday yako inamaana huwezi kununua? tupunguze munkari kwenye petty issues kama hizi mama katoa anachojisikia kinamfaa mbona mwingine kapeleka Airport na mbuga kabsa kwenye alipotokea!!

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
Pengine uko right, lakini hii ni Tanzania ambapo 'benzi kutolewa zawadi' ni excess, kama unafahamu!
 
Back
Top Bottom