Pre GE2025 Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu,

Kwani haiwezekami umeme wa ziada ukawepo lakini kukawa na tatizo la kuunganisha sehemu fulani za nchi kiasi kwamba hizo sehemu iwe rahisi kununua umeme wa nje?

Hata mkono wako unapingana na kichwa chako Kwa haya unayoandika
 
Sema kama kuna kitu nawakubali ni timing za kutoa hizi taarifa, kupiga matukio. Hiki kipindi story kubwa itakuwa ni game ya Simba na Yanga, na unaweza kutwa ilihailishwa kitaalamu tu.

Waache kuchezea hela kwenye mambo yayo ya muhimu, wapeleke sehemu husika mambo yatakaa sawa tu. Hakuna nchi imewahi kujengwa kwa uchawa.
 
Ila hili la kutokuwepo kwa mwendelezo wa mikakati ya kimaendeleo litatufanya tuendelee kubaki pale pale,maana kila utawala unakuja na yake

Mfano kwenye elimu hakuna miendelezo,kila utawala unakuja na utaratibu wake
 
Huu ni upigaji ndo unaoendelea yaani hamjifunzi katika

Escrow
Richmond

Na sasa mmekuja na huu mchongo Mpya na mlivyo wajanja mmeshamtia mkuu wenu ndani.
 
Ww hakika ni zero brain....kwaiyo hiyo back up unayoisemea itakua special kwa ukanda wa kaskazini tu, kanda ya kaskazini pekee ndio Tanzania?
Mkuu Unaelewa Maana ya Grid?
Grid ni Interconnection of Power plants and Transmission infrastructures
Arusha hana Hata Chanzo Kimoja cha Umeme lakini anatumia Umeme unaotoka Kidatu au Mtera hio ndio maana ya Interconnection

Kuunga na Kenya kwetu au option ya Kununua umeme iwe kama back up tu leo tumeungana na Kenya kupitia arusha kwa vile Arusha Nimpakani haimaanishi Umeme huo utatumika Arusha tu no utakuwa distributed Countrywide kutegemea na Kiasi chake

Yani iko Ivi Arusha imekuwa kama Gateway tu ila Ikitokea Total blackout tunaweza kwa haraka kuchukua Umeme kenya na Tukasema umeme huo usitumike Arusha uje moja kwa Moja dar es salam au Dodoma Kwenye Maeneo strategic ili operation ziendelee
 
Mkuu Hili ni dili tu kama yalivo madili mengine hata wanao craft izi Contract watakuwa sehemu ya dili tu

Kwa akili ya kawaida huwezi kuwa na Surplus Then ukaenda tena Kununua nje Umeme
It doesn't make sense kabisa hio hela ya kwenda Kununulia umeme Nje kwanini usifanye facilitation tu Ukajenga Transmission Line yenye uhakika kabisa badala ya Kwenda kununua Umeme nje

Hii ni dili tu
 
Hii ni DP world nyingine,inaingiziwa mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania,kuliko zaliwa Chadema!
 
Umetoa maelezo vizuri kabisa kuliko Gerson msigwa.
 
Hata mkono wako unapingana na kichwa chako Kwa haya unayoandika
Fuatilia mada mwanzo mwisho. Bila kuhemuka.

Halafu elewa kuwa kuna hoja za kidhahania zaidi.

Swali langu hujajibu.
 
N
Ww hakika ni zero brain....kwaiyo hiyo back up unayoisemea itakua special kwa ukanda wa kaskazini tu, kanda ya kaskazini pekee ndio Tanzania?
Acheni wivu wa kike! Nyie wengine si mnapata umeme usiokatikakatika kutoka stigla goji na kinyerezi 1,2,3,4,5...12?
 
Zambia hii hii ya Hichelema au Zambia ipi? Maana hapa Lusaka hatuna umeme hii ni siku ya nne sasa.
Hiyo hiyo na ndio faida ya mikataba ya Kimataifa.

Kwa taarifa Yako tuu Rukwa na Katavi wanatumia umeme wa Zambia.

Nyie mtakaosa umeme hata wiki ila huku lazima walete.
 
Kumbe huu wimbo ya kuuza umeme nje ya nchi tumekuwa tunachezeshwa toka enzi za mzee wa “mitaji yenu niya kujenga viwanda vya juisi”!
Serikali iuze na sgr yetu dubai ili tupate pesa ya kuwanunua wapinzani kwenye uchaguzi ujao.
 
Tangu ipigwe ile K. O ya bandar za tz bara na bado watu wakasifu na kuabudu kwamba ni maamuz sahihi bhas sioni lolote la kupingwa.

Labda tutangaziwe kodi ya pumzi.
 
Sababu umbali, cha kujiuliza umeme siyo mawe useme ni bora ununue mpakani mwa Kenya kuliko kuyafata mawe Rufiji kuyapelela Same, Kwanii umeme wasinunue kutoka Moshi kuliko kwenda kununua Ethiopia
Halafu huo umeme wa bwawa la Nyerere la huko Rufiji watakuja waiuzie Kenya na Uganda ambapo kuna umbali zaidi kuliko Kanda ya kaskazini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…