''Something is terribly wrong''
Tumeambiwa umeme wa JNHP unatosheleza nchi na kuuza nje
Tukaambiwa hata mvua isponyesha miaka 3 hatuna shida ya umeme
Kaskazini kuna Nyumba ya Munga na Hale Tanga zinazochangia grid ya Taifa
Tuna Upepo na Jua katika uwanda wa kuanzia Same hadi Singida
Tumejenga ''line' kuunganisha na Kenya ili tuweze kuwauzia umeme wa ziada tulio nao.
Leo tunasikia eti tunataka kuagiza umeme.
Huu mkanganyiko una mambo mawili kwa Wananchi. Ima wakae kimya kwasababu hawaelewi, na wale wanaoelewa wakae kimya kwasababu ya kuchanganyika. Kuna tatizo kubwa sana!
JokaKuu Pascal Mayalla