Rais Samia: Simba alikuwa hatulii kama ‘Mwanangu Lissu’, ndio maana nikasema apewe jina hilo

Anachoweza kukumbukwa lisuu ni
lisuu ni nani kwanza ??
mimameno yake ya ubaguzi, uchochezi na matusi tu.
Lissu kachochea nini?

Lissu kambagua nani?

Mbaguzi ni nani kama sio Samia anayefukuza watu kwenye ardhi yao ya asili huku Lissu akikemea wazi ubaguzi huo sasa hapo mbaguzi nani?

Naungana na mchangiaji mmoja aliyeomba machawa mjengewe uwezo [capacity building] kwenye kujibu hoja baada ya kupandisha mabandiko na mpunguze hizo lullabies.
Lakini Rais wetu amefanya mambo mengi ambayo hayawezi kufutika wala kufutwa na yeyote yule katika Taifa letu.
Yapi ?

Hebu orodhesha 10 tu!
Ni Mama Samia Rais wetu mpendwa ndiye amefanya Elimu kuwa bure kabisa hadi kidato cha sita.ambapo sasa watoto wanasoma kwa furaha na matumaini makubwa sana ya kutimiza ndoto zao.
Elimu bure sio kigezo mmechelewa sana na sikulaumu wewe sababu watanzania wengi exposure ni ndogo.

Mimi nimewahi kutembelea nchi kadhaa elimu ni bure sababu inagharamiwa na kodi za wananchi na si kitu cha kumpa heko mtawala.

Usikute wewe licha ya kuwa Mbeya hujawahi hata kufika nchi jirani kama Malawi na Zambia tu .
Ni Mama Samia Rais wetu mpendwa ambaye ametoa maelfu kwa maelfu ya ajira kwa vijana kila mwaka tangia
Ajira zipi ?

Unaweza kuweka takwimu hapa?

Maana vijana hao hao ndio tunaona humu wamegeuka kujiita "maafisa ubashiri" je kamari ni ajira rasmi,?

Malalamiko ya ajira yamo lukuki humu.
ameingia madarakani.ni Mama Samia amepandisha bajeti ya kilimo kutoka Billion 250 hadi Trilioni 1.2.
Hizi pesa anatoa wapi yeye kama rais?

Hizo ni kodi na tozo wanazolipa wananchi ,rais hana hizo pesa na sio zake hivyo hastahili sifa yoyote hapo wapongezwe watu kwa kulipa kodi sio mtawala.
ni Rais Samia Mama yetu Mpendwa ameweka rekodi ya kuzindua mradi wa treni ya mwendo kasi ,kukamilisha bwawa la mwalimu Nyerere ambalo alilikuta likiwa 34% .
Kuzindua mradi nacho ni kitu cha kujisifia ?

Hizo pesa za kugharamia mradi zimetoka wapi?

Nani watalipia gharama za huo mkopo wa kujenga hiyo miradi kama sio watumiaji wa mwisho ambao ni wananchi?

Samia tangu amezindua hiyo treni kapanda lini tena , mfano huko Kizimkazi alipokuwepo wiki nzima kwenye bonanza alienda na treni ?

Kuzindua sio jambo la kupongezwa hakuna sifa yoyote kwenye kuzindua bali wanaotakiwa kujipongeza ni wanachi kodi zao ndio zimejenga mradi huo uwanufaishe wao.

Je Samia mbona ameshindwa kudhibiti wizi ambao magenge ya wezi yanachepusha makusanyo ya kodi kwenda katika njia zisizo rasmi?

Au kwenye mambo ya wizi , ubadhirifu,matumizi mabaya ya ofisi sio uongozi wa Samia au huko Tanzania ni ya rais mwingine na sio Samia?
 
..Ni Simba wa Tanganyika.

..Zanzibar na Kizimkazi hakuna Simba.

..Jina lingine ambalo Lissu amepewa na Wazanzibari ni "Ronaldo."
Lissu amekosa ushawishi kwa watanzania na ndio maana mpaka leo anahangaika na michango ya kununua gari .wakati angekuwa anakubalika kwa watanzania angekuwa amepata hata billion moja mpaka muda huu.
 
Kuna ubaguzi mbaya kama mama aliowafanyia Massai? Avae kijola aende kwenye...... Hastaili kuwa ikulu
 
Ni usajili ambao CCM wanautaka leo, kesho na keshokutwa……
 
Yani Mh kila mtu nchi hii anamuona kama mwanae.

Kazaliwa 1960, Lissu 1968, ni mwanae kivipi?
Huyo ni mkuu wa nchi ni mama wa nchi hii, hata uwe mzee kiasi gani automatically anakuwa ni mama yako.
 
Ni usajili ambao CCM wanautaka leo, kesho na keshokutwa……

..Nchi hii inahitaji USHINDANI baina ya vyama vya siasa.

..Tunahitaji kufika mahali ambapo uchaguzi ukiitishwa hakutakuwa na uhakika chama kipi kitashinda.

..Sasa hivi kila sehemu wameshika Ccm ndio maana wanachezea pesa kurubuni wapinzani.
 
Tundu anaweza kuwa mtoto wa Samia,I mean kiumri kwamba anaweza kumzaa?
 
..Nchi hii inahitaji USHINDANI baina ya vyama vya siasa.

..Tunahitaji kufika mahali ambapo uchaguzi ukiitishwa hakutakuwa na uhakika chama kipi kitashinda.

..Sasa hivi kila sehemu wameshika Ccm ndio maana wanachezea pesa kurubuni wapinzani.
Hakuna mwenye akili Timamu na anayejitambua vizuri anayeweza kupoteza muda wake kushabikia upinzani. Upinzani na wapinzani ni wasaka Tonge tu na wachumia tumbo.ndio maana wenye akili Timamu na wanaojitambua wanaondoka CHADEMA kila siku kuja CCM
 
Haya mambo uliyomuuliza huyu chawa hawezi kukujibu kwa ufasaha. Huwa hawezi kujenga hoja bali anasifia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…