Rais Samia: Sitangazi hadharani kiasi cha Ongezeko la Mshahara ili wafanyabiashara wasipandishe bei

Rais Samia: Sitangazi hadharani kiasi cha Ongezeko la Mshahara ili wafanyabiashara wasipandishe bei

Haya mambo yanaenda kitaalamu zaidi, mishahara sio kama mnada wa masufuria unatangazwa hadharani.

Uswazi tu ukienda umenunua nyama au samaki hujaweka kwenye mfuko usioonyesha ndani, unaweza kurogwa, sembuse mshahara
We jamaa 😂😂😂
 
Mishahara ya wafanyakazi itapandishwa kwa kimya kimya Ili kuepuka Upandaji wa bei za bidhaa endapo itatangazwa hadharani

Rais Samia amesema Mambo ni Moto mambo ni fire!

Source ITV

Bibi Ushungi.
 
Sijawahi kuona uchumi wa namna hii
Kupandisha mishahara kila mwaka na uchumi ukapanda
Hebu wana uchumi nisaidieni hili maana sijawahi kuoandishiwa mshahara kila mwaka
 
Namuamini Rais Samia , ni mtu wa kimya kimya lakini kazi inafanyika.
Porojo, kitu ambacho alipaswa kuwasaidia ni kutoa tozo kwenye miamala ya ATM. Unaongeza sh 8000 , alafu unaweka tozo kwenye ATM kila muamala unapofanyika. Hapo unakua umemsaidia nini huyo mfanyakazi?

Hatukuwahi kuwa na tozo za ATM. Hili Leo lilipaswa kusemwa na kuondolewa.

Yaani bongo mtu yupo tayari umuongozee pesa sh 10000 atakushangilia, alafu hapohapo umuwekee makato ya sh 2000 kila wiki na bado hatashtuka
 
Kinachosumbua Akili yangu siyo nyongeza ya mshahara Bali ni namna wanavyo linga kulipa pesa za wastaafu utafikiri waonhawatastaafu!

Kushindwa kupeleka michango ya wafanyakazi Kwa wakati wanaona ni Jambo DOGO Sana natamani waajili wa namna hii wafukuzwe kazi.

Malipo ya UHAMISHO na madai mengine ya watumishi wanajifanya kama hawajui kama WANAMDAI.
sababu za kufanya uhakiki Kwa zaidi ya MIAKA miwili inafikirisha Sana labda wafanya MAHESABU ndiyo wale walioingia Kwa vimemo.

Kulipa posho kulingana na mshahara Kwa baadhi ya taasisi ni ugonjwa wa kudumu kitendo hicho kinawaumiza watumishi na Kuwa na kinyongo cha kudumu
Hivi INAKUWAJE unajua kwamba unastahili kulipwa 500 lakini unalipwa Shs.60 je,ni tofauti gani na wadhulumaji wengine ambao tunawaombea kila siku Mungu atende miujiza juu Yao Kwa kiwango kilekile cha udhalimu wanaoufanya.

Nyumba hii inahitaji usafi katika Sekta hii ya kuwasaidia watumishi ili kupata haki hata kabla ya kupanga mishahara mipya.
 
Sijui, ila nawaza hawa ambao tukiongeza mishahara tu nao wanapandisha bidhaa bei [emoji848]
Kumbe kuna watu wanaweza kupandisha tu bei za bidhaa bila sababu ya msingi...??? FCC wanakuwa wapi muda huo?

Kipindi bei za bidhaa nyingi zinapanda hovyo, wengi walisema kuna udhaifu wa vyombo vya serikali kudhibiti hali hiyo, wakawa wanabisha na kusema ni Urusi na Ukraine

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Haya mambo yanaenda kitaalamu zaidi, mishahara sio kama mnada wa masufuria unatangazwa hadharani.

Uswazi tu ukienda umenunua nyama au samaki hujaweka kwenye mfuko usioonyesha ndani, unaweza kurogwa, sembuse mshahara
Jioni wakitoa barua zao zile kuwa wameongeza % kadhaa,najua utakuja kupongeza "wanaupiga mwingi"...watanzania shida kweli

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Wafanyakazi kila mwaka wanadai nyongeza ya mshahara.

Mbona sisi wakulima hatuongezewi chochote??

Au wenye haki ni wao wenyewe tu.
 
Back
Top Bottom