Super Sub Steve
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 17,404
- 10,900
Wakulima Bei za mazao zimepanda mara dufuWafanyakazi kila mwaka wanadai nyongeza ya mshahara.
Mbona sisi wakulima hatuongezewi chochote??
Au wenye haki ni wao wenyewe tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakulima Bei za mazao zimepanda mara dufuWafanyakazi kila mwaka wanadai nyongeza ya mshahara.
Mbona sisi wakulima hatuongezewi chochote??
Au wenye haki ni wao wenyewe tu.
Bado hujajifungua tu hiyo mimba inayompenda mboweRaisi wa TUCTA kama Mbowe tu kwa Samia
hamainishi hivyo kama unavyowaza funguka ndani ya boksi hizo ni lugha tu.Punguza makasiriko sasa unategemea hizo milion 10 au 5 alizoahidi zitawasaidia wafanyakazi kama akili zinavyowatuma?
Serikali naamini itakuja na mpango mzuri juu ya wafanyakazi nao watafurahi sana.
Kupunguza bei ya chakula ni unawezekana kw kuongeza miundo mbinu kurahisisha usafirishaji ili kupunguza gharama, pamoja na kuboresha zaidi sekta ya kilimo ili kukuza uwekezaji na mavunoZile mil 10 kwa kila goli, azigawe kwa wafanyakazi maana hazijatoka.
Vitu vimepanda sababu watchman hayupo. Mtu wa kuwabana wafanyabiashara waache upumbavu huo hayupo. Hatuna kiongozi wa aina hio kwa sasa.KUPANDA KWA VITU HAKUNA UHUSIANO NA KUPANDA KWA MISHAHARA mbona Vitu vimepanda na Mishahara haijaongezwa?
Kwa bajeti ipi .huyo mama unamwamin asieeMama kasema mambo ni moto na mambo ni faya kwa wafanyakazi. Mishahara ya nyongeza kila mwaka kwa wafanyakazi itarudishwa kama zamani, sheria za kazi na kanuni litaafanyiwa kazi na kuna chombo mahususi cha serikari cha kusimamia afya na usalama wawa wafanyakazi mahali pa kazi.
"Lakin yote hayo hatutasema hadharan ni kwa kias gan marupurupu haya tumeyaongeza maana wakisikia huko mtaani watongeza bei za bidhaa"
"Walimu pia tumewasikia na swala malipo ya ziada baada ya muda wa kazi tunalifanyia kazi, walimu na madaktari ni chama kubwa" walimu oyeee!
"mwisho kabisa tufanye kazi kwa bidii na kwa kujituma" ahsanten sana
Kutiki chikakaJioni wakitoa barua zao zile kuwa wameongeza % kadhaa,najua utakuja kupongeza "wanaupiga mwingi"...watanzania shida kweli
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kiuhalisia ndo ashatangaza hilo ongezeko..Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) leo tarehe 01 Mei, 2023 mkoani Morogoro.
Rais amewasili uwanjani akiambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson pamoja na Viongozi wengine wa Kiserikali na Vyama vya wafanyakazi.
Kauli Mbiu ya mwaka huu ni “Mishahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi. Wakati ni Sasa.”
Kinachoendelea sasa ni maandamano ya vyama vya wafanyakazi wanapita mbele ya Rais na Meza kuu wakiwa na Mabango yenye jumbe mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Abubakar Mwassa anazungumza;
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Abubakar Mwassa amesema tangu Rais Samia aingie Madarakani, wafanyakazi 7108 mkoani humo wamepandishwa madaraja huku wengine 2030 wameajiriwa kupitia ajira mpya na kibali kingine cha kuajiri watu 3861 tayari kimeshatolewa.
View attachment 2605963
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Abubakar MwassaAidha, mkoa huo kwenye mwaka huu wa fedha umepanga kuanzisha ranchi mpya 4 pamoja na kufufua mashamba mengine makubwa ili kuongeza ajira kwa vijana.
Amemshukuru Rais Samia kwa uongozi mzuri na anatumaini chini ya Utawala wake Maslahi ya wafanyakazi nchini yatazidi kuboreshwa.
Katibu Mkuu wa TUCTA anazungumza;
Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi TUCTA, Hery Mkunda amesema wafanyakazi ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa jitihada anazofanya Rais Samia kwenye nyanja zote za maisha.
View attachment 2605964
Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi TUCTA, Hery MkundaAmesema Kauli Mbiu ya mwaka huu waliibuni kuonesha nia ya kuwawezesha wafanyakazi wapate haki zao, mikataba ya ajira na mishahara iliyo bora ili kuongeza tija na ufanisi kwenye maeneo ya kazi.
Kwa niaba ya Wafanyakazi, amemshukuru Rais Samia kwa kufanya mambo makubwa yanayowagusa. Ametoa ahadi ya kuendelea kuwa watiifu huku wakijituma kwenye maeneo ya kazi.
Mwaka jana ongezeko la Mshahara lilikuwa 23.3% likigusa wafanyakazi wa kika cha chini cha Mshahara, amesema wanaendelea kupiga magoti na kubisha hodi ili aendelee kuwafikiria.
Ameomba kitengo cha Idara ya Kazi kilicho chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kiboreshwe na kuongezewa wafanyakazi, ameishujuru Serikali kwa kuboresha afya kwa watanzania kupitia mpango bima ya afya kwa wote.
Rais Samia anazungumza;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewashukuru waandaji wote wa Maadhimisho ya mwaka huu kwa kuwezesha yafane na yaende kama yalivyopangwa.
Amesema Mei Mosi ni siku ya kutambua mchango na kutoa heshima kwa wafanyakazi kwa kazi kubwa wanayofanya ndani ya taifa. Umadhubuti wa Taifa hili upo kwa sababu ya wafanyakazi.
Pamoja na kudai mishahara bora, uadilifu na weledi kazini ndio utaleta maisha bora kwa wafanyakazi.
Serikali itaendelea kuboresha maslahi ya kazi serikalini na katika sekta binafsi zipatikane ajira zenye usalama na ajira za staha kwa wote. Pia, madai yote ya mwaka jana yametekelezwa kwa zaidi ya 95%
Rais Samia amesema pia nyongeza ya Mishahara ya mwaka sasa itarejeshwa, watu watapandishwa madaraja na vyeo pamoja na kuongeza posho japo hatasema hadharani ataongeza kwa kiasi gani.
Amesisitiza “Kwa hiyo ndugu zangu wafanyakazi, kile watu walichozoea tukiseme hapa ili wapandishe bei madukani mara hii hakuna, tunakwenda kufanya mambo polepole, kupandishana jinsi tulivyosema, wasione tumeongezeana kitu gani ili mwenendo wetu wa bei uwe salama. Kwahiyo mambo mazuri yapo, ila hatutayatangaza hapa”
Kuhusu malalamiko ya makato ya kodi, Raia Samia amesema hilo ameliacha kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi na Mawaziri husika ili walitazame kwa pamoja na kulipatia majibu.
Baada ya Mkutano huu, Waziri Mkuu atazungumza na waajiri ili kutatua kero ya uwasilishaji wa michango ya wanachama.
Madai ya malipo ya Bima yanapaswa kufanyika ndani ya siku 60 kama sheria inayotaka ili wafanyakazi wanufaike.
Akizungumzia kuhusu Maslahi ya walimu upande wa teaching allowance, Rais Samia amelichukua na ataenda kulifanyia kazi, pia amemuagiza Waziri wa Elimu kuhakikisha walimu wanapewa mafunzo ya matumizi sahihi ya vishikwambi walivyopatiwa, na utaratibu unafanyika ili baadae kila mwalimu awe na kishkwambi chake.
Vipi Leo anakuja na package au wasubiri kwan
Tulikuwa naye lini...labda enzi za Ujamaa...Tume ya Bei!Vitu vimepanda sababu watchman hayupo. Mtu wa kuwabana wafanyabiashara waache upumbavu huo hayupo. Hatuna kiongozi wa aina hio kwa sasa.
Ilipanda bei sababu walificha ila sahizi chini ya Bagamoyo Sugar aibu ingebaki kwao. Washamba ni hao waliokuwa wanamuita raisi mshamba kumbe wao ndio hawana akili.Tulikuwa naye lini...labda enzi za Ujamaa...Tume ya Bei!
Kuna mshamba mmoja alikuja, Kila alikuwa anatamani kuwwbana wafanyabiashara bila kutumia akili matokeo yake bidhaa ilipanda Bei ...mfano wa Sukari!
Kwani Bagamoyo Sugar sio mfanya Biashara!?Ilipanda bei sababu walificha ila sahizi chini ya Bagamoyo Sugar aibu ingebaki kwao. Washamba ni hao waliokuwa wanamuita raisi mshamba kumbe wao ndio hawana akili.
Kwani Bagamoyo Sugar sio mfanya Biashara!?
Uhuni unanzishwa na Beuracrats ,na yeye ataingia tu!Ndio amekuja kuondoa uhuni