Rais Samia: Sitangazi hadharani kiasi cha Ongezeko la Mshahara ili wafanyabiashara wasipandishe bei

Nachotaka kufahamu ni kwamba Je lile Ongezeko la mwaka Jana la posho itakuwa zaidi kwa mwaka ujao?

Mwisho Naishauri Serikali ipunguze Kodi kwenye salary maana huko kwenye posho watakaofaidika ni mabosi wenye safari,sie wengine itakuwa maumivu tu.

Wakuu kumekuwepo na tetesi huku halmashauri kuwa kwa mwaka huu upandaji madaraja utafanyika mwezi may na sio julay je hili lina ukweli wowote kwa mlioko jikoni huko?
 
Punguza makasiriko sasa unategemea hizo milion 10 au 5 alizoahidi zitawasaidia wafanyakazi kama akili zinavyowatuma?

Serikali naamini itakuja na mpango mzuri juu ya wafanyakazi nao watafurahi sana.
hamainishi hivyo kama unavyowaza funguka ndani ya boksi hizo ni lugha tu.
 
Zile mil 10 kwa kila goli, azigawe kwa wafanyakazi maana hazijatoka.
Kupunguza bei ya chakula ni unawezekana kw kuongeza miundo mbinu kurahisisha usafirishaji ili kupunguza gharama, pamoja na kuboresha zaidi sekta ya kilimo ili kukuza uwekezaji na mavuno

Ila hawawezi kuamrisha tu bidhaa za kilimo zishuke bei kila mara, hilo ni hapana, mnataka mkulima atumiaye gharama na wenye umaskini mwingi aishi vipi? Nyie wafanyakazi mna mishahara malupulupu na mk8staafu mna kiinua mgongo, huyu mkulima je, mnataka azidi kuwa maskini, azeeke mapema na awe mzee maskini afe mapema, sio haki
 
KUPANDA KWA VITU HAKUNA UHUSIANO NA KUPANDA KWA MISHAHARA mbona Vitu vimepanda na Mishahara haijaongezwa?
Vitu vimepanda sababu watchman hayupo. Mtu wa kuwabana wafanyabiashara waache upumbavu huo hayupo. Hatuna kiongozi wa aina hio kwa sasa.
 
Kwa bajeti ipi .huyo mama unamwamin asiee
 
Kiuhalisia ndo ashatangaza hilo ongezeko..
 
Vitu vimepanda sababu watchman hayupo. Mtu wa kuwabana wafanyabiashara waache upumbavu huo hayupo. Hatuna kiongozi wa aina hio kwa sasa.
Tulikuwa naye lini...labda enzi za Ujamaa...Tume ya Bei!
Kuna mshamba mmoja alikuja, Kila alikuwa anatamani kuwwbana wafanyabiashara bila kutumia akili matokeo yake bidhaa ilipanda Bei ...mfano wa Sukari!
 
Ilipanda bei sababu walificha ila sahizi chini ya Bagamoyo Sugar aibu ingebaki kwao. Washamba ni hao waliokuwa wanamuita raisi mshamba kumbe wao ndio hawana akili.
 
Ilipanda bei sababu walificha ila sahizi chini ya Bagamoyo Sugar aibu ingebaki kwao. Washamba ni hao waliokuwa wanamuita raisi mshamba kumbe wao ndio hawana akili.
Kwani Bagamoyo Sugar sio mfanya Biashara!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…