Rais Samia Suluhu ahutubia Mabunge ya Kenya: Biashara kushamiri, Vikwazo Mipakani kutatuliwa, Udugu kudumishwa

Hakika huyu ni BIG MAMA.

Nimesikiliza hotuba ya Mama SSH mwanzo mwisho...huyu mama amemfunika Hayati Jiwe kwa mbali sana kwene maswala ya KIDPLOMASIA. Mama Samia ameonesha hekima, busara na maarifa ya hali ya juu kwenye ku-SULUHU-isha migogoro!

Mimi amenimaliza aliposema Kenya wana UHURU(Rais) na Tanzania tuna SULUHU(Rais)!

Maana yake ni kwamba Kenya wana Uhuru wa kufanya Biashara na Tanzania wana Suluhu ya kumaliza Matatizo/Migogoro ya Kibiashara inapojitokeza!! Kongole sana mama yetu. Uko juu sana.
 
Bunge la Tanzania linavutia kwa Spika na Naibu Wao kukiuka Katiba Kuwaonea Wapinzani kudhurumu Haki zao
 
dunga atakua kanuna huko
 
Yuko vizuri.
 
Bunge la Ndugai na magufuli marehemu halina tofauti na lile la Somalia
 
Hebu nikuulize jambo, baada ya sifa kemkem hizi:

Hujasahau kitu (jambo) hapo, au ni siri ya baadae, hapo unaposema "Mungu ampe miaka mingi...", ili atawale 10, au mitano zaidi?
 
Kwani job ndugai yeye anasemaje kuhusu hiyo democrasia bungeni?
 
Huo urafiki na ujirani wa Kenya umeanza jana? Ama hizo fursa za Urafiki na ujirani na Kenya zimetokea jana mama Samia alipoenda Kenya?

Ndio maana hii nchi haiwezi kupata maendeleo watanzania wanaendeshwa na mihemko. Wanachemka haraka kama maziwa nakupoa haraka.

Hata Magufuli alipoanza miezi 6 ya kwanza ilikua hivi hivi, leo hii huyu mama mnampa sifa za kijinga hata miezi 2 hajamaliza ofisini.

Muda ni mwalimu mzuri, ngoja tusubiri mnaoimba mapambio na kutoa sifa za kijinga tunawapa muda tu.

Yaani mtu anaongea kama vile sisi na Kenya ujirani umeanza jana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…