Rais Samia Suluhu ahutubia Mabunge ya Kenya: Biashara kushamiri, Vikwazo Mipakani kutatuliwa, Udugu kudumishwa

Rais Samia Suluhu ahutubia Mabunge ya Kenya: Biashara kushamiri, Vikwazo Mipakani kutatuliwa, Udugu kudumishwa

Ayubu (Job) anune lakini ni kweli kuwa ukilinganisha mabunge haya mawili - uhuru wa Bunge unaonekana kuwa mkubwa Kenya kuliko hapa. Kenya kila jambo linaweza kusemwa Bungeni na mbunge kupata kinga stahiki. Hapa kwetu utasikia “futa kauli” au “maneno ya kuudhi” au “hotuba ya upinzani haitasomwa kwa sababu ina maneno yasiyotakiwa”!!

Bunge la Kenya ninaihoji na kuibana serikali kwa sababu mawaziri (secretaries) hawatoki miongoni mwa wabunge. Hapa nyumbani, mawaziri wanaogopwa na wabunge kwa sababu nao ni wabunge pia!! Kila mbunge anapalilia siku moja kuteuliwa kuwa waziri kwa hiyo anakosa hari na moyo wa kuikosoa serikali!!
 
"Wafanyabiashara nendeni mkashirikiane na sio kushindana, mna bahati kwamba katika Nchi zetu hizi mbili upande mmoja kuna Uhuru wa kufanya biashara na upande mwingine kuna Suluhu ya kuondosha vikwazo vya biashara, hapo mshindwe nyinyi tu".

Mwisho wa kunukuu.

Kabla upande mmoja ulikuwa na UHURU na upande wa pili MAGUFULI, hapo tafasiri yake nini?
 
Hizi sio chokochoko kweli?
 
Ukweli Mungu ametupa

Rais ambaye muda wote anaiweka nchi mbele katika matamshi yake. Hasemi Mimi anasema Tanzania. Hotuba yake Bungeni Kenya imefunika. Very composed President. Hakuna mbwembwe na kujimwambafai. Mungu mlinde Rais wetu Samia. Mpe miaka mingi. Mpe afya na muondolee Maradhi na maadui. Tunakuombea mama yetu.
 
Mama anazidi kumsuta na kumkejeli Ndugai na bunge lake dhaifu lililojaa wacheza ngoma.

Ndugai zamu hii sukari itakuwa inapanda kiholela na vile vijidudu vya umeme wa gridi ya taifa vinaweza kugoma kusikia zile punje anazobugia kila siku.
Na "mzigo wa India" inaelekea umeshaanza kuingia.....RIPs zimeanza tena!
 
Mama anazidi kumsuta na kumkejeli Ndugai na bunge lake dhaifu lililojaa wacheza ngoma.

Ndugai zamu hii sukari itakuwa inapanda kiholela na vile vijidudu vya umeme wa gridi ya taifa vinaweza kugoma kusikia zile punje anazobugia kila siku.
Au lile nundu kichwani laweza kupasuka lenyewe!
Ndugai ukimwangalia hadi unasikia hasira jinsi anavyo lifedhehesha bunge letu.
 
Rais Samia amemshukuru Spika wa bunge la Kenya kwa kumpa heshima ya kuhutubia mabunge mawili ya nchi hiyo kwa pamoja.

Rais Samia amesema yeye ni Rais wa pili kutoka Tanzania kupewa heshima ya kuhutubia bunge hilo linaloheshimika duniani akiwa ametanguliwa na mstaafu Jakaya Kikwete.

Rais Samia amesema bunge la Kenya linavutia kwa upana wa demokrasia yake.

Kazi Iendelee!

Anasema ya kweli toka moyoni mwake, kwani Mh. Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwa Makamu wa Rais alipata kusema jinsi anavyovutiwa na michango ya hoja za wabunge wa upinzani Tanzania

Toka Maktaba :

17 Feb 2020
Samia Suluhu : "Napenda mawazo ya wapinzani, huwa wanajenga hoja vizuri, walini 'inspire' niingie siasa"

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefunguka kuhusiana na historia ya maisha yake ambapo ameeleza siri ya mafanikio na chanzo kilichomvutia kuingia kwenye siasa. Samia Suluhu hoja za upinzani ni moto, walinivutia / inspire, mimi ni activist ...

Anasema ya kweli toka moyoni mwake, kwani Mh. Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwa Makamu wa Rais alipata kusema jinsi anavyovutiwa na michango ya hoja wa wabunge wa upinzani Tanzania

Toka Maktaba :

17 Feb 2020
Samia Suluhu : "Napenda mawazo ya wapinzani, huwa wanajenga hoja vizuri, walini 'inspire' niingie siasa"

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefunguka kuhusiana na historia ya maisha yake ambapo ameeleza siri ya mafanikio na chanzo kilichomvutia kuingia kwenye siasa. Samia Suluhu hoja za upinzani ni moto, walinivutia / inspire, mimi ni activist ...

Kama siyo kununuliwa wapinzani wako vizuri kichwani!
 
Rais Samia amemshukuru Spika wa bunge la Kenya kwa kumpa heshima ya kuhutubia mabunge mawili ya nchi hiyo kwa pamoja.

Rais Samia amesema yeye ni Rais wa pili kutoka Tanzania kupewa heshima ya kuhutubia bunge hilo linaloheshimika duniani akiwa ametanguliwa na mstaafu Jakaya Kikwete.

Rais Samia amesema bunge la Kenya linavutia kwa upana wa demokrasia yake.

Kazi Iendelee!
Ndugai kichaa kitamuwaka tena
 
Back
Top Bottom