benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Rais Samia Suluhu amepokea hundi ya Dola Milioni 30 (Bilioni 70) kutoka kwa Barick Gold Mine kwa ajili ya ujenzi madarasa nchi nzima hasa kwa ajili ya Wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 watakaoanza masomo katika muhula ujao wa masomo
Rais Samia ameeleza kuwa kwa sasa wanafunzi watakaomaliza masomo mwezi Juni ni 72000 lakini wale wanaotarajiwa kuanza kidato cha 5 wakiwa ni zaidi ya 192000 hivyo kuwa na ongezeko la wanafunzi zaidi ya 120000
Rais Samia amewaomba watanzania wengine kuunga mkono jitihada za serikali huku akisisitiza kuwa kwa sasa suala la madarasa watakayosoma watoto wa Kitanzania wa kidato cha 5 kwa muhula ujao wa masomo ndilo suala linalomnyima usingizi kwa sasa.
Katika mchango walioutoa Barick utawasilishwa kwa awamu tatu tofauti wakianza na kutoa Dola Milioni 10.