Rais Samia Suluhu amepokea hundi ya Dola Milioni 30 kutoka kwa Barick Gold Mine

Rais Samia Suluhu amepokea hundi ya Dola Milioni 30 kutoka kwa Barick Gold Mine

Ni makampuni ya madini hayahaya yaliwatajirisha mabilionea mawakili wa CHADEMA na IMMMA, wakiachiana Urais TLS. Wanawatukana mchana, ikifika usiku wanapeleka invoice za taxplanning, wanalipwa vinono kumbe zimetoka makinikia yetu waliyokuwa wanakwiba. Mara kaja Rais mzalendo green hadi mdomoni. Hajamaliza wiki 2 shujaa kakamata malori na malori ya makanikia bandarini. Wakamchukia kina tundulissu, wa TLS, fatmakarume, pamoja na Activists hawampendi Magu hadi leo kaburini.
Vipi Mwanyika alipewa ubunge na JPM ilihali tuliaminishwa ndio alituletea hasara ya trillion 300 plus!!
 
Changa la macho hakuna hela hapo.

Usanii mtupu.
 
Rais Samia Suluhu amepokea hundi ya Dola Milioni 30 (Bilioni 70) kutoka kwa Barick Gold Mine kwa ajili ya ujenzi madarasa nchi nzima hasa kwa ajili ya Wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 watakaoanza masomo katika muhula ujao wa masomo

Rais Samia ameeleza kuwa kwa sasa wanafunzi watakaomaliza masomo mwezi Juni ni 72000 lakini wale wanaotarajiwa kuanza kidato cha 5 wakiwa ni zaidi ya 192000 hivyo kuwa na ongezeko la wanafunzi zaidi ya 120000

Rais Samia amewaomba watanzania wengine kuunga mkono jitihada za serikali huku akisisitiza kuwa kwa sasa suala la madarasa watakayosoma watoto wa Kitanzania wa kidato cha 5 kwa muhula ujao wa masomo ndilo suala linalomnyima usingizi kwa sasa.

Katika mchango walioutoa Barick utawasilishwa kwa awamu tatu tofauti wakianza na kutoa Dola Milioni 10.
kwa hiyo ndani ya miezi hii michache shule zitakamilika na walimu wataajiriwa.kwa sasa hata hizi shule zilizopo madawati hayatoshi watoto wanagombania sehemu za kukaa,walimu hawatoshi halafu tunawaza kujenga madarasa ambayo bado hayatasaidia chochote badala ya kuimarisha miundo mbinu iliyopo.aliyetuloga sijui yuko wapi.
 
Inawezekana kupokea hela bila kuita wakuu wa mihimili, majeshi na mawaziri ikulu, na wazungu wa kupendezesha picha mbele ya kamera live za TV zote nchini na mitandao ya kijamii ya Ikulu?
 
mama yetu atatufikisha pazuri vijana tupige kazi.... huyu ndiyo kiongozi mwenye upeo na maono ndani ya miaka miwili tuu kafunika maraisi watatu bado wawili awe kinara wao
 
Sio mchango. Ni pesa yetu kupitia kampuni yetu ya twiga. Hayo ni moja ya matunda ya Magufuli na Kabudi. Ila hawatasema.
Zile noa zetu ziliishia wapi? Huu ni mchango/msaada barric wametoa sio Kodi Wala sio gawio ni mchango wao baada ya kulipa Kodi pamoja na mrahaba
 
Mwambie hakuna kitu kama hicho na hasitafute huruma kwa watanzania anaowanyonya kila siku kupitia viongozi waka hasa M.Rameck Ester big stars, Anakosaje hela ya kujenga madarasa wakati anapata hela ya kununua gori moja 5mln?

Akikujibu, mijadala ianzie hapo.
Hatafuti huruma yako wewe Bali anatekeleza majukumu yake kama raise hutaki hamia Burundi
 
Kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa kuna 'upigaji'mwingi sana.
Nadhani wahusika wameshajua udhaifu wa serikali yao.
Ni afadhali kujenga viwanda hata kama wanafunzi wakisomea chini ya mti, wakimaliza wapate ajira.

Kila fedha kuelekezwa kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa kuna tatizo mahali
Hivi mbona hamna jema ninyi watu? Hakuna kazi ngumu kama kuongoza watu ndio maana hata waisrael jangwani walimkwaza Musa mpaka akamkosea MUNGU
 
Hatafuti huruma yako wewe Bali anatekeleza majukumu yake kama raise hutaki hamia Burundi
kwa hiyo hii nchi mshajibinafsisha mapunga tu,burundi hatuendi na upinde wenu wa mvua tutaupasua na huyo mwanaharakati wenu na mama tutamkosoa tu.
 
Wasi sahau kutekeleza yale makubalino na selikali ya kujenga refinary,kujenga barabara kutoka kaķola had kahama,na kulipa zile bilion 700.
 
Rais Samia Suluhu amepokea hundi ya Dola Milioni 30 (Bilioni 70) kutoka kwa Barick Gold Mine kwa ajili ya ujenzi madarasa nchi nzima hasa kwa ajili ya Wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 watakaoanza masomo katika muhula ujao wa masomo

Rais Samia ameeleza kuwa kwa sasa wanafunzi watakaomaliza masomo mwezi Juni ni 72000 lakini wale wanaotarajiwa kuanza kidato cha 5 wakiwa ni zaidi ya 192000 hivyo kuwa na ongezeko la wanafunzi zaidi ya 120000

Rais Samia amewaomba watanzania wengine kuunga mkono jitihada za serikali huku akisisitiza kuwa kwa sasa suala la madarasa watakayosoma watoto wa Kitanzania wa kidato cha 5 kwa muhula ujao wa masomo ndilo suala linalomnyima usingizi kwa sasa.

Katika mchango walioutoa Barick utawasilishwa kwa awamu tatu tofauti wakianza na kutoa Dola Milioni 10.
Ni Barick Gold Mine wametoa fedha au ni Twiga ?
 
Ikifika 2030 watanzania mtatambua Samia uwezo wake wa kuiongoza nchi unafanana na Ally Hassan Mwinyi
 
Barrick Gold ni nani mpaka watoe hizo hela kwa ajili ya ujenzi wa madarasa! Kama ni mgao wa faida si inatolewa halafu serikali inaamua kiasi gani kitumike kwenye hili ama lile? Inakuwa kama vile tunapewa msaada na Barrick wakati ni gawio tena la kiwizi mkubwa. Dah!
Umeongea point kubwa sana.
 
Back
Top Bottom