Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Atakayefanikisha kukamatwa kwa "KIGOGO" atapewa donge nono..
Mimi na walevi wenzangu tutatoa donge nono kwa Atakayefanikisha kukamatwa kwa atayemkamatisha "KIGOGO"
...... KIGOGO apewe uraisi wa twira... Milele na milele hata akivunja katiba atajua mwenyewe...
Maza SSH piga spanaaaaaaaaa
Means what,kigogo aongezewe muda wa utawala huko Twitter na akikataa,Alazimishwe??
 
Mkurugenzi wa shirika la ndege inabidi aseme lile gawio walilitoa wapi?
Kwani kulikuwa na gawio? Ule ulikuwa usanii wa Meko tu, ili kuaminisha watu kuwa shirika la ndege lilikuwa linapata faida.
Kuna watu walisema ATCL inafanya hasara. Meko akatengeneza huo usanii ili kuwazodoa waliokuwa wanasema ATCL inapata hasara.
 
JPM hakuwa mzalendo alipandikiza watu wake kwenye sekta nyeti tusingeweza kujua uozo kama huu
Ngoja tuone kazi ya mama tusikosee kila jambo, kila mmoja ana mazuri yake ba mapungufu yake, huwezi kuwa [emoji817] mkamilifu
 
Da hoja ya kitoto kweli. Ulishawahi kujiuliza anapokaa Rais, Makamu wake na Waziri mkuu huwa wanajadili nini!?????

Unalotakiwa kujua ni kwamba serikali sio mtu ni taasisi. Na afanyalo rais ni matokeo ya kazi ya wasaidizi wake.

Issue ya huyu kakoko imeanza kushighulikiwa kilichokua kikisubiriwa ni report ili atumbuliwe


KUNA KUKAA NA KUJADILI na kuna kukaa na kuambiwa cha kufanya
 
Kuna watu hapa Tanzania wamesimamishwa kazi au kuvuliwa madaraka na kuambiwa wasubiri kupangiwa kazi nyengine kwa miaka mingi sasa na bado wanakula mishahara yao bila kufanya kazi yeyote ile serikalini. Zanzibar tunao wengi mno.
 
Makontena yaliruhusiwa kwa mbinde Sana Tena unaambiwa mama alienda mpaka ikulu kuonana na mzee mzee akagoma
Kwa hiyo wewe unafurahia watu wasiolipa kodi? Si yalitakiwa kulipiwa kodi au kodi inalipwa kwa watu maalumu tuu.
DG kasimamishwa sababu ya ubadhirifu uliotokea huko,maana wengi walisimamishwa ilibaki yeye tuu.Ndio Raisi kasema nae asimame kupisha uchunguzi kama hana hatia atarudi.
 
Ripoti ya CAG 2020/2021 iliyo tolewa leo mbele ya Mhe. Rais imebainisha kuwa na ubadhirifu wa kutisha mpaka kulazimika kumsimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Bandari.

Bandari kuna mdudu gani hapo asiye kufa!?!

Takukuru na vyombo vingine pamoja na FIU wanao wajibu wa kusafisha ubadhirifu huu unao jitokeza hapo bandarini, inaonekena kila mfanyakazi hapo Bandari ni Mpigaji.
Al asaad wa watu aliposimamia ukweli
Walimtenga na kuona anaharibu nchi
It's just a matter of time everything will be revealed
 
Simlikuwa mnasema kuwa huyu CAG ameletwa hapo na Magufuri ili afiche madhaifu ya serikali, sasahivi anafichua madhaifu mnaanza Magufuri asingeliwatumbua, kwani Samia amejifunzia wapi kutumbua?huyo mkuu wa TPA alikuwa analiwa taming tu maana Muasibu wake mkuu Alisha simamishwa kitambo na Majariwa na kuagiza uchunguzi wa ubadhirifu ufanyike na lipoti itolewe,sasa kuna jipya gani hapo wakati watu tulikuwa tunasubiri lipoti ya Majariwa?
ATCL Faida imeleta faidaaaaaaaaa,wanyonge pigeni makofi tafadhaaaaaaali.

Screenshot_2021-03-28-12-22-56-1.jpg
 
KUNA KUKAA NA KUJADILI na kuna kukaa na kuambiwa cha kufanya

Kwa hiyo Unavyoelewa wewe waziri mkuu alikurupuka kwenda kutoa maagizo bandari?
Halafu kingine unacholazimisha ni kwamba Samia alikua anasubiri kifo ndio huyo mtu atumbuliw?
Rudi kwenye attach,ents nilizokuwekea walau uelewe serikali ni taasisi
 
Back
Top Bottom