Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

2019-2020 wewe, mbona kama unakimbizwa
 
Atastaafishwa huyo kwa maslahi ya umma. Au vinginevyo atapelekwa Utumishi na hatopokea tena mshahara wa DG na badala yake atapewa mshahara wake wa kabla ya kuwa DG. Serikali imejilinda kwenye hilo eneo usifikiri hawajui.
 

Kwa nchi hii hata ufanye reflection ya miaka, ngumu kuongoza. Approach yake ilikuwa na mapungufu mengi, Ila hii ya kusubiri michakato ndio mbaya zaidi. Wabongo ni watu hatari sana, kuongoza watu waliojawa unafiki lazima uangukie pua tu.
 
Hivi mtu imethibitika kaiba tena baada ya uchunguzi wa muda... Adhabu ni kusimamishwa kazi au kiwekwa ndani?
Hizi Bil 3.6 serikali inarecover vp na mwizi yuko hapo, je kisimamishwa kazi inatosha?
Wanasema eti ni "UNTOUCHABLE"
 
Hayati na Dotto James walikua ni vibaka hatari plus mauaji wamefanya sana
 
Usipofanya mambo yako kama wewe ni muajiriwa wa bandarini basi sahahu kutoboa...hii ndio kauli mbiu sasa ni ukiwa bandarini kila mtu anatafuta chake...
 
Huyu kigogo
Huyu kigogo asipodhibitiwa haraka ni hatari Sana, naona jamii inaziamini taarifa zake kwa kasi kuliko serikali, kibaya zaidi anazitoa kabla ya mamlaka husika, polisi wametangaza donge nono kwa atakayempata, changamkieni fursa huenda ukaibuka millionaire
 
Unamzungumziaje hasara za ATCL kwa miaka mitano
Kwanza ni hujuma na kukosa uzoefu wa kuendesha shirika na hili ni tatizo la kitaifa, kwamba hatuna maofisa watendaji wenye uzoefu.

Pili, ATCL pia ilikuwa ni lazima kama shirika hilo limeshindwa kusafirisha ndege zake katika njia za kimataifa kutokana na suala la COVID -19.

Hapa hatuwezi kumlaumu mtu mmoja bali ni kujitathmini kama watanzania kwamba tunalinda na kuenzi mali na rasilimali za serikali.

Lakini hilo haliondoi dhamira ya serikali kuwa na shirika la ndege ambalo lajiendesha lenyewe kwa faida, na kukosa usimamizi haimaanishi kuwa serikali isinunue ndege, maana kuna siku ndege hizo zitaenda London, au New York na kwingine.

Watanzania tumekosa dhamira ya kweli ya kujikomboa kiuchumi na pia tumekosa uzalendo katika kulinda rasilimali zetu.

Mwisho, watanzania tumekosa nidhamu ya tulicho nacho, twataka mafanikio na maisha bora kwa njia rahisirahisi bila kujihangaisha akili zetu.

Mfano ni hao mabosi wa TPA na ATCL wamekosa akili za kuendesha mashirika hayo makubwa ambayo ni nembo ya taifa na njia kuu za mapato ya fedha za kigeni na za ndani.

Tumewakosa wazee kama marehemu kama Aarod Nsekela NBC , Gibson Mwaikambo NIC , Mosha wa Tanesco na yule marehemu mzee wa ilokuwa posta na simu na Kaduma wa ATC ambayo ilikwua yaenda London.

Hawa walikuwa na vichwa vya kubuni na kuendesha mashirika haya na tuliona jinsi yalivyokuwa yameshamiri Tanzania nzima.

Walipotangulia mbele ya haki walobakia nyuma wakaanza zogo na ubadhilifu na kisha kuja kuyavuruga mashirika hayo.

Twapaswa kuanza upya kuandaa maofisa watendaji hodari ambao wataendesha taasisi na mashirika makubwa kama haya ambayo ni vyanzo vikuu vya mapato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…