Unamzungumziaje hasara za ATCL kwa miaka mitano
Kwanza ni hujuma na kukosa uzoefu wa kuendesha shirika na hili ni tatizo la kitaifa, kwamba hatuna maofisa watendaji wenye uzoefu.
Pili, ATCL pia ilikuwa ni lazima kama shirika hilo limeshindwa kusafirisha ndege zake katika njia za kimataifa kutokana na suala la COVID -19.
Hapa hatuwezi kumlaumu mtu mmoja bali ni kujitathmini kama watanzania kwamba tunalinda na kuenzi mali na rasilimali za serikali.
Lakini hilo haliondoi dhamira ya serikali kuwa na shirika la ndege ambalo lajiendesha lenyewe kwa faida, na kukosa usimamizi haimaanishi kuwa serikali isinunue ndege, maana kuna siku ndege hizo zitaenda London, au New York na kwingine.
Watanzania tumekosa dhamira ya kweli ya kujikomboa kiuchumi na pia tumekosa uzalendo katika kulinda rasilimali zetu.
Mwisho, watanzania tumekosa nidhamu ya tulicho nacho, twataka mafanikio na maisha bora kwa njia rahisirahisi bila kujihangaisha akili zetu.
Mfano ni hao mabosi wa TPA na ATCL wamekosa akili za kuendesha mashirika hayo makubwa ambayo ni nembo ya taifa na njia kuu za mapato ya fedha za kigeni na za ndani.
Tumewakosa wazee kama marehemu kama Aarod Nsekela NBC , Gibson Mwaikambo NIC , Mosha wa Tanesco na yule marehemu mzee wa ilokuwa posta na simu na Kaduma wa ATC ambayo ilikwua yaenda London.
Hawa walikuwa na vichwa vya kubuni na kuendesha mashirika haya na tuliona jinsi yalivyokuwa yameshamiri Tanzania nzima.
Walipotangulia mbele ya haki walobakia nyuma wakaanza zogo na ubadhilifu na kisha kuja kuyavuruga mashirika hayo.
Twapaswa kuanza upya kuandaa maofisa watendaji hodari ambao wataendesha taasisi na mashirika makubwa kama haya ambayo ni vyanzo vikuu vya mapato.