Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Ripoti ya CAG 2020/2021 iliyo tolewa leo mbele ya Mhe. Rais imebainisha kuwa na ubadhirifu wa kutisha mpaka kulazimika kumsimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Bandari.

Bandari kuna mdudu gani hapo asiye kufa!?!

Takukuru na vyombo vingine pamoja na FIU wanao wajibu wa kusafisha ubadhirifu huu unao jitokeza hapo bandarini, inaonekena kila mfanyakazi hapo Bandari ni Mpigaji.

Kama mhandisi Kakoko kakumbwa na dhoruba, huu ni mwanzo mpya.

Ikumbukwe huyu ni tanroads damu.

Bado yule wa madaraja.
 
ingekuwa uwezo wangu viongozi wote wa TPA wachunguzwe, kuanzia vipato vyao binafsi, miradi yao, mali zao zote pamoja na majengo wanayo miliki.

inaonekana wafanyakazi wote wa TPA ni wachafu kunuka, wachunguzwe na mali zao zishikiliwe.
hapo TPA hakuna msafi, TAKUKUTU, FIU, POLISI na TISS tafadhali fuatilieni TPA, imekuwa mfupa huo.
 
Alisemaje???
Kigogo na Chahali wapewe kombe kuanzia Magu alipougua mpaka sasa. Most of theirs tweets are relible. Ona hii ni Chahali ali-tweet juzi ileeeeee.
''#BreakingNews: Tanzania Port Authority chief, from "Chato Inc" tried to siphon Tsh 48 billion (approx USD 20.7) from TPA's account at Central Bank for purpose of influencing member of powerful ruling party commettee to keep Magufuli's appointees in their current posts''
 
Mh.Samia "pesa za miradi yote tokea mwezi wa Kwanza zichunguzwe zilivoingia,na zikivyotoka" hapa kuna watu wataumia.Alafu Jaffo ni Kama yupo kwenye uangalizi, anytime anaondoka na yeye!mzembe Sana jamaa!
 
Kazi kubwa ya mama ni kukabiliana na wabadhirifu,wazembe na kuelekeza pesa kwenye matumizi sahihi tuu ,aachane na kutekeleza mamiradi ya Magu ni hasara tupu.

Hao wako wengi walikuwa wanakingiwa kifua na aliyepita ,mtu kama Kakoko ni mdau wa Magu toka kitambo na alikuwa na tuhuma kama zote
 
Jaffo alichokuwa anajua ni kujipendekeza kwa jiwe tu! Ila hata jiwe wakati anatangaza baraza la mawaziri alionesha kutoridhishwa sana na TAMISEMI ya Jaffo
Aya sasa ajipange
 
Back
Top Bottom