Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Kwa nini tunaonyesha kila dalili ya kufurahia jambo bila hata kuchukua muda kutafakari?
Amesimamishwa kazi na hajafukuzwa kazi.
Uchunguzi wa kina ufanyike!!
Kipi cha ku celebrate hapo?
Maskini watanzania!!
Hata iweje hatarudishwa TPA, alikuwa jeuri sana huyu kisa urafiki na the Late
 
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Ripoti ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ametoa agizo la kusimamishwa Mkurugenzi Mkuu wa Bandari(TPA) kutokana ubadhirifu mkubwa unaoikumba mamlaka hiyo.

Mkurugenzi mkuu huyo anasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa kina.
Kazi imeanza, mliodhani mama ni soft soft kuliendesha taifa mjitafakari tena
 
TPA yahitaji kuendeshwa kijeshi mpaka inakapoweza kujitambua.

Kakoko asingeweza kudhibiti ubadhilifu, hujuma na wizi bandarini na ni mwepesi sana.

Kuna mtu amemtaja marehemu mzee Janguo lakini yule nae hakuweza kuthibiti TPA basi aliweza kusawazisha kulingana na serikali zilizokuwepo wakti ule.

Nasema hivi kwasababu mimi binafsi nimewahi kufanya kazi ya utoaji mizigo bandarini na naelewa matatizo haya yanoikumba TPA.

Mama Samia mteue mwanajeshi mwenye shahada ya uendeshaji asimamie shirika hili ambalo ni moja ya njia kuu ya mapato Tanzania.

Pili, serikali ikubali igharamie teknolojia katika bandari zetu na iondokane na paperwork. Pia kuwepo idara maalum ya ku-monitor kila tukio kuanzia meli inapotia nanga hadi mizigo inapokuwa "cleared".

Hali hiyo iwe pia kwenye uingizaji mafuta kule TIPPER.

Paperwork ni moja ya njia kuu za ubadhilifu kwenye bandari zetu ikiwemo bandari ya Daesaama.
 
Huenda yupo humo humo ikulu.
Inner cycle! Kuna mole! Shame sijui watamng'oaje?

Everyday is Saturday............................... 😎
Hii ni hatari sana...ni wazi eidha jamaa yuko humo humo au source zake za taarifa ziko huko humo. Haiwezekani akawa na sensitive info kiasi hiki...hata siri zake rais maana yake jamaa anazipata....
 
Duh...
Samia aiunde upya ikulu na taasisi ya tiss, haiwezekani huyu jamaa awe anapata taarifa kiasi hiki...
There is a big fissure somewhere...
TISS imeshakuwa ya hovyo tayari.heshima yao inaporomoka kwa kasi,sema kuna baadhi ya wanasiasa mlengo wa kushoto wana vijana wao kule,imagine umewatoa vijana wako mtaani ukawapa ulaji TISS, hawawezi kukuangusha ukihitaji kitu kutoka kwao. Vita ya ndani kwa ndani ,ngumu sana.
 
Kiufupi ni kwamba Dg aliwahi kuziwia makontena ya mama yetu yule mbunge wa kule Nan. Alie wahi kua first Lady.
Mzee alichachamaa Sana na kufikia Hatua mpaka ya kuita wazee wa Baraza na kuwaambia kua anacho fanya Hayat hajakipenda na Akubalian nacho

Mambo yakaenda wakayamaliza ila Bifu lilibak hasa kwa uyo Dg mana yeye ndie alie toa Amri ya kuziwia contena kipind icho


Pia bila shaka system Ile ya nimeichukua ka hela kaMboga imesha shika uskan walio kua Upande wa Hayat na wakabania watu wa system wajiandae mana soon wanaliwa vichwa pia mama yetu tayar Amesha chagua Upande

Kigogo pia ni mtu Wa Ndan ya ccm Ile ya system ndiomana amejua kua fulan siku fulan hato kuepo atatimuliwa sababu majina yote ya watu wasio hitajika hata yeye anayo so kazi yake ni kuyasoma tu na kuyataja hadharan

Kwa hili ni wazi kabisa kua kigogo ni vigogo time will tell

Mama amesha chagua Upande

Mama hachagua upande jombi. Huu ni mwanzo mpya.

Mama na akaze hapo hapo Chatto Inc ni imani si kabila!
 
Mimi najiuliza hivii...!!
1. Huo ubadhirifu umefanyika baada ya tarehe 6 March 2021?
2. Au huo ubadhirifu umefanyika baada ya tarehe 17 March 2021?
3. Kama ubadhirifu ulikuwepo? Kwanini haukusemwa kabla?
Mkuu nani angethubutu kusema? Hiyo hasara ya ATCL yenyewe imesemwa leo kwa sababu Meko yuko chini ya ardhi, miaka 5 mfulilizo hakuna faida na tulidanganywa kwamba ATCL inaingiza faida kubwa.
 
Back
Top Bottom