Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Huyo kigogo yumo ikulu tena ni zaidi ya mtu mmoja
 
Kwa nini tunaonyesha kila dalili ya kufurahia jambo bila hata kuchukua muda kutafakari?
Amesimamishwa kazi na hajafukuzwa kazi.
Uchunguzi wa kina ufanyike!!
Kipi cha ku celebrate hapo?
Maskini watanzania!!
Enzi za mzee hata hiyo hasara ingetajwa?
 
ingekuwa uwezo wangu viongozi wote wa TPA wachunguzwe, kuanzia vipato vyao binafsi, miradi yao, mali zao zote pamoja na majengo wanayo miliki.

inaonekana wafanyakazi wote wa TPA ni wachafu kunuka, wachunguzwe na mali zao zishikiliwe.
hapo TPA hakuna msafi, TAKUKUTU, FIU, POLISI na TISS tafadhali fuatilieni TPA, imekuwa mfupa huo.
Kwa namna ninavyoelewa, hata hao wote ulio wataja, hamna kitu watafanya wakifika hapo TPA!!niamini,uwizi upo kwenye DNA za waafrica ngozi nyeusi!! Kwani walioko Tiss,Takukuru, IFU,Polisi n.k wanatofauti gani na walioko hapo TPA?!! Wote ni wale wale ata hao uliowataja wakichunguzwa uko kwenye taasisi zao hutaamini madudu yatakayo kutwa!!ngozi nyeusi tunaamini kuiba kwenye taasisi za umma ni ushujaa!!Meko amepeleka miradi mikubwa kwao Chato kinyume cha taratibu (wizi) watu wa kwao wanamuona ni shujaa!! hizo ndio akili zetu ngozi nyeusi,ripoti ya CAG inaonyesha kuna ubadhirifu mkubwa hapo TPA,DG anasimamishwa,watu wanashangilia!! Rais anaogopa kumpeleka jela,mtu kama uyo hastaili kuwa uraiani kwa sasa,pahala panapo mstahili ni ukonga, au gereza la kilimo kitengule uko akajifunze kula kwa jasho halali,unamsimamisha nini wakati ripoti ya wataalamu inaonyesha katafuna pesa ya umma?!!au CAG haaminiki?!!
Taarifa hii ilitosha kumfikisha lupango, uchunguzi wa nini tena!! wakati ripoti imeanika kila kitu!!au ndio anapumzishwa kupisha upepo upite ili atafutiwe nafasi nyingine ya kuiba?!!unakuta hata Rais anamlaumu kwa kuiba bila kutumia akili,na adhabu pekee ni kumsimamisha kwa muda tu!!harafu wananchi wanashangilia!!!
Ila kuongoza waafrica ni kazi rahisi sana ni kama kula papuchi kimasihala.
 
Mkuu nani angethubutu kusema? Hiyo hasara ya ATCL yenyewe imesemwa leo kwa sababu Meko yuko chini ya ardhi, miaka 5 mfulilizo hakuna faida na tulidanganywa kwamba ATCL inaingiza faida kubwa.
Wewe kweli ni mshamba,unafikiri lipoti hii imeandaliwa siku hizi mbili baada ya kufa Magufuri?
 
Ukiangalia jinsi rais alivyomsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa TPA ni uamuzi aliouchukua hapohapo baada ya kusomewa ripoti na CAG,sasa huyu kigogo alijuaje???..au kulikuwa na mipango ya mkurugenzi kutimuliwa kabla ya ripoti kusomwa??..huenda huyu kigogo anafanya kazi vizuri kabisa na serikali,baadhi ya viongozi wakubwa serikalini bila mzee pombe kujua..yaani rais alikuwa anazungukwa na wateuwa wake kwa maslahi Fulani!..
same way alivyoyajua mengine. inside connection man.
 
Mfumo gani mama katengeneza?
Mfumo namaanisha unafanyika uchunguzi kwanza kisha mapendekezo halafu maamuzi.

Faida: Unakuwa na uhakika na maamuzi unayoenda kuchukua. JPM alikuwa hacheleweshi, Anaweza pita barabarani mtu akalalamika kuhusu mkurugenzi akamwita kisha akamtumbua.

Hasara: Habari kuvuja mapema maana uchunguzi unawahusu watu zaidi ya mmoja. Muhusika kujua linalofuata.
 
Back
Top Bottom