TPA inahitaji kuendeshwa kijeshi mpaka inakapoweza kujitambua.
Kakoko asingeweza kudhibiti ubadhilifu, hujuma na wizi bandarini na ni mwepesi sana.
Kuna mtu amemtaja marehemu mzee Janguo lakini yule nae hakuweza kuthibiti TPA basi aliweza kusawazisha kulingana na serikali zilizokuwepo wakti ule.
Nasema hivi kwasababu mimi binafsi nimewahi kufanya kazi ya utoaji mizigo bandarini na naelewa matatizo haya yanoikumba TPA.
Mama Samia mteue mwanajeshi mwenye shahada ya uendeshaji asimamie shirika hili ambalo ni moja ya njia kuu ya mapato Tanzania.
Pili, serikali ikubali igharamie teknolojia katika bandari zetu na iondokane na paperwork. Pia kuwepo idara maalum ya ku-monitor kila tukio kuanzia meli inapotia nanga hadi mizigo inapokuwa "cleared".
Hali hiyo iwe pia kwenye uingizaji mafuta kule TIPPER.
Paperwork ni moja ya njia kuu za ubadhilifu kwenye bandari zetu ikiwemo bandari ya Daesaama.