Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

kigogo ameongea baada ya rais kumsimamisha kazi tu ndio akatweet. tumieni akili zenu wakati mwingine sio kila kitu uambiwe na watu au kigogo
Nani anatumia tumbo na akili kufikiri?
Screenshot_20210328-125235.jpg
 
Ukiangalia jinsi rais alivyomsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa TPA ni uamuzi aliouchukua hapohapo baada ya kusomewa ripoti na CAG,sasa huyu kigogo alijuaje???..au kulikuwa na mipango ya mkurugenzi kutimuliwa kabla ya ripoti kusomwa??..huenda huyu kigogo anafanya kazi vizuri kabisa na serikali,baadhi ya viongozi wakubwa serikalini bila mzee pombe kujua..yaani rais alikuwa anazungukwa na wateuwa wake kwa maslahi Fulani!..
Kwani Kigogo alisemaje?. Siku akikamatwa sijui itakuwaje.
 
Aliyekwiba bandarini ni mshkaji wake meko na ndiye alikuwa anauza michongo ya TRA kwa meko. Yani ni miongoni mwa waliokuwa wakipiga simu kwa meko muda wowote.

Sasa kiko wapi
 
kigogo ameongea baada ya rais kumsimamisha kazi tu ndio akatweet. tumieni akili zenu wakati mwingine sio kila kitu uambiwe na watu au kigogo
Tweet ya Kigogo iko tangu jana jioni. Sema wewe umeiona leo.
 
I second you. JPM kwa uzalendo alikua namba moja, sidhani kama kuna Rais aliyekua na uchungu na hii nchi kama yule mzee

Tatizo lake kubwa alikua anataka kutengeneza "Cult personality" kwamba watu wote waone juhudi zake yeye kama yeye binafsi sio serikali kwa ujumla. Na watoto wa mjini walilijua hilo wakawa wananata na biti hapo hapo kumpamba huku wanafanya mitikasi yao
Hakuwa mzalendo bali alikuwa mwizi kama wezi wengine tu
 
Kwanza ni hujuma na kukosa uzoefu wa kuendesha shirika na hili ni tatizo la kitaifa, kwamba hatuna maofisa watendaji wenye uzoefu.

Pili, ATCL pia ilikuwa ni lazima kama shirika hilo limeshindwa kusafirisha ndege zake katika njia za kimataifa kutokana na suala la COVID -19.

Hapa hatuwezi kumlaumu mtu mmoja bali ni kujitathmini kama watanzania kwamba tunalinda na kuenzi mali na rasilimali za serikali.

Lakini hilo haliondoi dhamira ya serikali kuwa na shirika la ndege ambalo lajiendesha lenyewe kwa faida, na kukosa usimamizi haimaanishi kuwa serikali isinunue ndege, maana kuna siku ndege hizo zitaenda London, au New York na kwingine.

Watanzania tumekosa dhamira ya kweli ya kujikomboa kiuchumi na pia tumekosa uzalendo katika kulinda rasilimali zetu.

Mwisho, watanzania tumekosa nidhamu ya tulicho nacho, twataka mafanikio na maisha bora kwa njia rahisirahisi bila kujihangaisha akili zetu.

Mfano ni hao mabosi wa TPA na ATCL wamekosa akili za kuendesha mashirika hayo makubwa ambayo ni nembo ya taifa na njia kuu za mapato ya fedha za kigeni na za ndani.

Tumewakosa wazee kama marehemu kama Aarod Nsekela NBC , Gibson Mwaikambo NIC , Mosha wa Tanesco na yule marehemu mzee wa ilokuwa posta na simu na Kaduma wa ATC ambayo ilikwua yaenda London.

Hawa walikuwa na vichwa vya kubuni na kuendesha mashirika haya na tuliona jinsi yalivyokuwa yameshamiri Tanzania nzima.

Walipotangulia mbele ya haki walobakia nyuma wakaanza zogo na ubadhilifu na kisha kuja kuyavuruga mashirika hayo.

Twapaswa kuanza upya kuandaa maofisa watendaji hodari ambao wataendesha taasisi na mashirika makubwa kama haya ambayo ni vyanzo vikuu vya mapato.
Well said kiongozi!!
 
Kiufupi ni kwamba Dg aliwahi kuziwia makontena ya mama yetu yule mbunge wa kule Nan. Alie wahi kua first Lady.
Mzee alichachamaa Sana na kufikia Hatua mpaka ya kuita wazee wa Baraza na kuwaambia kua anacho fanya Hayat hajakipenda na Akubalian nacho

Mambo yakaenda wakayamaliza ila Bifu lilibak hasa kwa uyo Dg mana yeye ndie alie toa Amri ya kuziwia contena kipind icho


Pia bila shaka system Ile ya nimeichukua ka hela kaMboga imesha shika uskan walio kua Upande wa Hayat na wakabania watu wa system wajiandae mana soon wanaliwa vichwa pia mama yetu tayar Amesha chagua Upande

Kigogo pia ni mtu Wa Ndan ya ccm Ile ya system ndiomana amejua kua fulan siku fulan hato kuepo atatimuliwa sababu majina yote ya watu wasio hitajika hata yeye anayo so kazi yake ni kuyasoma tu na kuyataja hadharan

Kwa hili ni wazi kabisa kua kigogo ni vigogo time will tell

Mama amesha chagua Upande
Mshaanza...
 
Kigogo anajua mambo mangapi? Si amekuwa mtabiri tangu enzi za chuma JPM? Hivyo ni visingizio tu.

Tumia akili zako ulizobakiza Mkuu,ukiona mambo ndani ya familia yako yanajulikana tambua yupo mmoja wenu kwenye familia yako anauza info,akigogo sio mtabiri Kigogo ni mtu yupo humo ndani anatoa hotuba za watu kabla yao.
 
Asee nawaonea huruma sana hawa watu wa magu... sahivi hawana mtetezi yaani ni kama vile watoto yatima
 
Raisi aliepita c alikua anafuatilia sana jamani na wezi walibanwa mno?? sasa huu ubadhirifu mkubwa umetoka wapi tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ulifatilia hotuba ya Magufuli wakati anazindua bunge la2020? Kama ukufatilia nenda YouTube usikilize maneno yake, Tanzania ilipokuwa imefikia usiliweza kumaliza ubadhirifu kwa miaka mutano, hata hivyo Magufuli alijitaidi sana pamoja na makelele yote mliokuwa mkipiga.
 
Mwendazake kawaachia msala!!
Noma SANA.
Mfugale towers, kuita hata Dr Omar Ali Juma tower walishindwa.

Everyday is Saturday............................... 😎
Eti Mara ooh, hili siyo Tena daraja la tazara ni daraja la Mfugale,

Mara ooh hili siyo ubungo flyover ni daraja la juu kijazi, ushamba ushamba tuh,

What's so special about Mfugale to us,zile ni pesa zetu walipa kodi,yarudishwe majina yake ya awali.
 
Mungu mbariki KIGOGO 2014.
Huyu ni hatari kwa usalama wa nchi, haiwezekani habari confidential ya nchi mtu wa pembeni anaipata within seconds, sio jambo la kufurahia japo najua wabongo kwa ujumla wetu tunapenda ubuyu. Binafsi sipendi, Rais anaandika kinote then within seconds kigogo ameipublish huko twitani, sio sawa hata kidogo...
 
Back
Top Bottom