Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Mfumo anaotumia Mama wa Taifa ni 1.3.6 kitaalamu Watasha wanaita ELECTRONIC UPWARD. Hapo anakabia kwa juu mpaka ukose pumzi hivyo utoe pumzi ya akiba iliyopo UKANDA WA CHINI...
SASA HIYO SUB YAKE INAYOPASHA MISULI MNAMJUA NI NANI???.......... Anaitwa Master KIFINYIO..
KWENYE UONGOZI WAZANZIBAR WANATHIBITISHA NI WATU NA NUSU , makofi kwao yawe mengi..
 
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Ripoti ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ametoa agizo la kusimamishwa Mkurugenzi Mkuu wa Bandari(TPA) kutokana ubadhirifu mkubwa unaoikumba mamlaka hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema haya

“Ripoti nimeona, nimeipitia na nimebaini ubadhirifu mkubwa uliofanywa pale bandari, hili suala mnatakiwa kushirikiana, nakuomba Takukuru jishughulishe pale, alipita Waziri Mkuu alilishughulikia.

“Waziri Mkuu aliunda kamati na wakafanya uchunguzi kidogo ambao yaliyotoka, hatua chache zilichukuliwa lakini imani yangu ni kwamba kama kuna ubadhirifu pale waliosimamishwa ni hawa wa chini huku, ninaomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu hatua zaidi ziendelee,”



Barua ya kumsimamisha kazi iko wapi? Hili ni changa la macho.
 
Kuna watu hapa Tanzania wamesimamishwa kazi au kuvuliwa madaraka na kuambiwa wasubiri kupangiwa kazi nyengine kwa miaka mingi sasa na bado wanakula mishahara yao bila kufanya kazi yeyote ile serikalini. Zanzibar tunao wengi mno.
Aiseeeeeeehhhhh
 
Jaffo alichokuwa anajua ni kujipendekeza kwa jiwe tu! Ila hata jiwe wakati anatangaza baraza la mawaziri alionesha kutoridhishwa sana na TAMISEMI ya Jaffo
Kazi yake kukimbiakimbia tuu, hivi mlishamuona alipokuwa kwenye msafara wa Jpm
 
Kwa nini tunaonyesha kila dalili ya kufurahia jambo bila hata kuchukua muda kutafakari?
Amesimamishwa kazi na hajafukuzwa kazi.
Uchunguzi wa kina ufanyike!!
Kipi cha ku celebrate hapo?
Maskini watanzania!!
Taratibu za kisheria zinataka hivyo, mpaka hapo lzma tumpongeze mama kwa kuliona hilo
 
Dah mkuu Ulipoteaga wapi mkuu wangu. Yani nikikumbukaga lile group lenu la upande wa pili mlikuwa mnaingiza makontena bandarini bila kulipia ushuru na kutushambulia wagalatia Ritz @khataan na FaizaFoxy
Mijamaa imefurahi sasa labda inapenda mtu wao mwingine akae tena!!system reboot mission accomplished
 
Back
Top Bottom