Rais Samia Suluhu ana emotional intelligence, utulivu wa hali ya juu

Rais Samia Suluhu ana emotional intelligence, utulivu wa hali ya juu

Mengine unamsingizia hasa hayo ya kushindwa makesi.

Wapi Watu wanafanya watakavyo Mkuu?
Mnataka Ile ya kila kitu Rais akitolee ufafanuzi kama Hana Wasaidizi wake?
Au unataka Ile ya Rais kudhalilisha Wasaidizi wake hadharani ili aonekane mchapakazi ilhali hafuati sheria kuwawajibisha hao anaowadhalilisha hadharani?

Hutaki kila mmoja abaki kwenye nafasi yake?

Kama ishu ni kusainishana mikataba ya kimangungo, hizi kesi tunazoshindwa sasa hivi Huyo Samia alikuwa Rais?

Simtetei Rais Ila najaribu kuonyesha kuwa kama taifa tunatatizo la kimfumo, kisheria na kimaadili
Oooh!!
So kumbe tumtenge na urais wake? Tumuongelee yeye ksma yete?
Binafsi nje ya Uongozi simfahamu kwakweli, Hapo sitakua na cha kuchangia.
Maana akina Magu na JK nje ya urais/uongozi kuna mahala tulikua tukikutana, lakini mama hapana, sijawahi kumuona wala kukutana naye bila ya kofia na Joho la uongozi
 
Naunga mkono hoja yako kwani ile kauli yake ya kuwa amechagua kukaa kimya na akamalizia kwa kusema hakuna mwenye ubavu ....... anamaanisha kuwa semeni yote mmalize lakini hamna cha kunifanya niliyoamua nimeamua na mkataba upo na utakuwepo kama ulivyo,hizo ni kelele za mlango tu hazimnyimi usingizi mwenye nyumba. Hicho ni kiburi cha kiwango cha juu sana.
Huyu jamaa anachanganya kiburi na utulivu ajenda za taifa haziihitaji viburi vya viongozi vinavyoitwa utulivu
 
😀😀😀
Mkuu Una hasira Sana.
Ni hasira na viongozi wajinga na wapuuzi wasio kuwa na akili wala kujua chochote wanapewa madaraka makubwa ya kuongoza taifa letu masikini hawa watu hawezi kuwa hata wenyeviti wa mitaa huko uchina tuna viongozi useless sana.
 
Ni hasira na viongozi wajinga na wapuuzi wasio kuwa na akili wala kujua chochote wanapewa madaraka makubwa ya kuongoza taifa letu masikini hawa watu hawezi kuwa hata wenyeviti wa mitaa huko uchina tuna viongozi useless sana.

Hoja ni kuwa marekebisho yafanyike.
Hoja za msingi zisikilizwe. Hasa hoja za wenye Akili. Kwa sababu jamii yetu Watu wengi bado wapo Gizani.
Na wengine wanaunga mkono hoja kishabiki
 
Sasa si mmeshaambiwa maoni yamechukuliwa na yanafanyiwa kazi ?au mnataka wana JF wote tupelekwe Dubai au Dar tukaangalie marekebisho yanavofanyika?

Wanazungumzia marekebisho ya vifungu.
Serikali haijakubali wala kukiri kuwa inaenda kufanyia marekebisho hivyo vifungu. Badala yake inavitetea, hapo ndipo utata ulipo
 
Umeandika maneno meengi na nnadhan hii nukuu inakufaa!
"It does not require many words to speak the truth."
Chief Joseph.
 
RAIS SAMIA SULUHU ANA EMOTIONAL INTELLIGENCE, UTULIVU WA HALI YA JUU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Unajua hivi vyeo bhana ukileta mchezo unaweza kujikuta unafanya mambo ambayo hata wewe ukija kutulia unajishangaa. Vyeo vinaleta Kiburi, Jeuri na majivuno. mamlaka na utajiri bhana haviwafai Watu wenye zero emotional intelligence.

Hana Wenge, Hana pupa wala kupaparika. Hana kihedemswede kurukaruka kama mcheza Rede.

Mwanzoni alipochukua madaraka kidogo wenge lilitaka kumvaa, oooh! Mimi mwanamke, ooh! Blah blah! Sisi Watibeli tukasema enhee! Kuna haribika hapa.
Lakini baadaye kidogo akatuliza wenge.
Nafikiri ulikuwa ugeni wa nafasi aliyopewa.

Oooh! Huyo ni mwanamke, Mwanamke hawezi kuongoza bhana!
Mara ohooo! Huyo sijui mzanzibara anaongozaje watanganyika. Mara oooh! Huyu Mama sijui mumetolea wapi, Kwanza anarimotiwa na rimoti Ipo msoga.
Oooh! Huyo Mama yenu anaikabidhi nchi Kwa wajomba zake sijui Ndugu gani Huko arabuni.
Hapajatulia, oooh! Sijawahi kuona Mama dikteta, huyu ndiye atakuwa amevunja rekodi ya Ulimwengu kuwa Mwanamke wa Kwanza kuwa Dikteta.

Maneno hayo na mengine mengi Mno, mengine kuyasema inaweza kuwa ni aibu, lakini Rais Samia bado anautulivu.

Huwezi kuwa na utulivu ukiwa katika mashinikizo ya aina hiyo kama hauna emotional intelligence. Huwezi!

Tena Kwa nafasi kubwa aliyonayo, ukizingati ni Muafrika kama Sisi na wote tunajua jinsi Sisi waafrika tunavyo-act endapo Watu hasa tunaowamudu wakileta kile tutakachoona ni kushushiwa heshima.
Mbali na Uafrika lakini pia ni Mwanamke, ambayo ni Sifa ya dunia nzima kuwa Wanawake wapo very emotional, na wengi wao ni zero emotional intelligence. Lakini Kwa Samia hiyo iko tofauti.

Tumeona viongozi kadhaa waliopita wakitekenywa kidogo jinsi watakavyo react. Tumeona na kama wewe hukuona basi ni wewe. Lakini hata Huko makazini au majumbani tunajua pale kiongozi anapotekenywa kidogo jinsi atakavyo reacts bila kujali sheria zipo au hazipo.

Ni nadra Sana ukute kiongozi mwenye Utulivu, Hekima na busara katika kuyaendea mambo. Ni ngumu kiongozi hasa Kwa level ya Rais kuchokolewa alafu asitumie mamlaka yake bila kujali ni Kwa Njia halali au haramu.

Sisi Watibeli hatusifii Watu ili tupate sijui vyeo au tutambulike au sijui viongozi watuone wamaana. Hiyo kwetu haipo hivyo Kwa sababu Sisi wenyewe tumezaliwa tunavyeo, tunatambulika na kujitambua. Hatuhitaji sijui favour ya Rais au kiongozi kumpongeza au kumkosoa.

Ndio maana pamoja na kumsifia na kumpongeza Rais Samia Kwa utulivu aliuonyesha lakini bado haifichuli ukweli kuhusu mapungufu ambayo anaweza kuwa nayo.
Kuhusu mkataba WA Bandari ni ufanyiwe marekebisho Kwa manufaa ya Nchi.

Kama Rais Samia angekuwa hana emotional intelligence ingekuwa kivumbi na jasho huko kwenye majukwaa.
Angekuwa kila Siku anapambana kujibu makombora anayotumiwa, kisha naye Atume vijembe. Viongozi wa hivyo tumewaona.
Lakini ninyi semeni, yeye atasikia kama mnasema kweli au laa hiyo haina maana yoyote kwake.

Kuhusu wale wakushtakiwa sijui Kwa kesi zisizo na kichwa wala miguu. Hilo Kwa Sisi Watibeli tunaita Wenge au kupaparika. Huko ni kukosa utulivu.

Kiongozi lazima awe na;

1. Akili
Upeo mkubwa wa kupambanua, kuchambua, kutatua changamoto za Watu wake. Maoni.

2. Uwezo wa kudhibiti hisia zake.
Kiongozi hatakiwi kuongozwa na mihemko kama mtoto anayebalehe.
Sikiliza, tulia, tafakari, chukua hatua kama kuna haja.

3. Mtu mwenye uwezo na sio mtu anayejitutumua kuonyesha anauwezo.
Hili ni tatizo Kwa jamii zetu za Afrika.
Yaani Watu uwezo Hawana lakini wanavyojitutumua sasa. Ndio maana dhulma na kutotendeka Kwa Haki kunatawala.

4. Uwezo wa kuwaunganisha Watu.
Unajua kabisa Watu unaowaongoza ni Wengi. Na kila mtu anaupeo na Akili zake. Sasa kutofautiana mawazo ndio unakasirika kama jinga Fulani hivi. Unakasirika nini kama wewe ni Kiongozi Bora kweli. Kiongozi lazima utambue kuwa Watu wanatofautiana na kila mmoja katika tofauti hizo anapaswa kuheshimiwa.
Kuna Watu wapole na wapo wakali, kuna Watu wenye kisirani na watu Watulivu. Kuna wenye Akili na wajinga. Mitazamo ya mafanikio inatofautiana.
Watu hao hawawezi kulingana. Na hata unavyodili nao lazima udili nao Kwa Akili.

Kila mmoja umtumie katika nafasi sahihi. Hata wajinga wanaumuhimu wao katika Dunia. Nafasi zao zipo na zikitumiwa vizuri ni faida Kwa nchi.

Kujua Watu na kujijua mwenye ndio tafsiri ya Hekima na busara Kwa sababu utajua nini chakufanya Kwa usahihi katika Wakati sahihi.

Jambo moja ambalo litanitia mashaka na ninalihofia ni pale Rais Samia ambaye ni Mwanamke awe na utulivu na emotional intelligence ambayo itawashinda viongozi wajao ambao tutakuwa wanaume.

Wanaume kwetu Hii ni challenge. Tumezoea kuona Wanawake ni Watu wa kukurupuka, kufanya vitu Kwa hasira na mihemko lakini Kwa Samia imekuwa tofauti.

Kikawaida ukiona nguvu kubwa inatumika ujue Akili ni ndogo. Na ukiona mtu anaendeshwa na mihemko ujue muda huo Akili haipo. Na ukiona mtu haendeshwi na mihemko ujue Akili yake inafanya kazi vizuri.
Ndio kuna ule msemo usema, usifanye maamuzi ukiwa na hasira au furaha(mihemko). Hiyo ndio maana ya uongozi Kwa namna nyingine.

Hongera Rais Samia, lakini bado hoja ya mkataba WA Bandari uitilie maanani. Penye marekebisho Parekebishwe.

Ni Yule Mtibeli. Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ni mtulivu au ameweka pamba masikioni?
 
Kibongo bongo ukiwa na emotional intelligence unaonekana boya.

Ila kusolve vitu kwako itakua rahisi sana maana hulimbikizi makitu kichwani na huna visasi.
 
Sasa si mmeshaambiwa maoni yamechukuliwa na yanafanyiwa kazi ?au mnataka wana JF wote tupelekwe Dubai au Dar tukaangalie marekebisho yanavofanyika?
Jana kasema yeye Samia ataendelea kukaa KIMYA nina imani wewe ni mtu mzima nadhani umeelewa ana maanisha case closed
 
Back
Top Bottom