Rais Samia Suluhu ana emotional intelligence, utulivu wa hali ya juu

Anakaa kimya mno. Mpaka minyukano ya kidini imeanza.
 
''Mataikuni wa fasihi'' kama wewe wanapatikana Tanzania tu. Tuna hasara kubwa!
 
Ubongo wako umetafsiri kiburi ni vyema pia.
 
Hapana, sifa hiyo Hana kabisa. Kama tumekosa watu wa kusifia hivyo basi tuache tu. Si lazima kumsifia kwasababu ni kiongozi. Narudia sifa hiyo Hana kabisa.
 
What is emotional intelligence or EQ? Emotional intelligence (otherwise known as emotional quotient or EQ) is the ability to understand, use, and manage your own emotions in positive ways to relieve stress, communicate effectively, empathize with others, overcome challenges and defuse conflict.

\huwezi kusema ana emotional intelligence huku akituma chawa wake kufungulia kesi za ugaidi na uhaini wapinzani wake. Huo ni uchawi/undumilakuwili
 
Magufuli alisema siku ile ya kuweka jiwe la msingi la fly over ya Ubungo kwamba anachoamua anakifanya bila ya kusikiliza maneno mengi yaliyokuwa yakimwambia amfukuze kazi Paul Makonda, hakufanya kama walivyotarajia.

Samia kusema anakaa kimya tayari ni nongwa!, vipi kama angejibu hovyo kama siku ile alivyojibu hayati JPM pale Ubungo?.

Rais ni amiri jeshi mkuu wa nchi, anakula kiapo na anayo haki ya kuwahakikishia raia anaowaongoza juu ya uwepo wa amani kwenye maisha yao ya kila siku.
 

Hata kama Hana 100% lakini hakosi 60% hiyo inatosha Mkuu.
 
Kukaa kimya wakati unatakiwa kuzungumza siyo hekima hata kidogo!! Kukaa kimya wakati ni wewe peke yako unayetakiwa kutoa suluhisho siyo hekima hata kidogo! Ni woga! ni kukwepa jukumu ambalo ni wewe peke yako unasubiriwa ulitoe!! Kukaa kimya wakati suluhisho la haraka linatakiwa ni kutokujiamini!! Tukubali kuusema ukweli hata kama tunataka nafasi za uteuzi!!! Mama tunampenda lakini hapa amefeli!! Ameamua kuyaacha mambo yaende hivyo hivyo liwalo na liwe!! Historia itamhukumu!!
 
Anakaa kimya kwa sababu hana jibu la yanayoulizwa. Hivi ulishaona mwizi anapokamatwa anakuwa na ya kusema? Anachofanya ni kuwasihi waarabu wabadili mkataba kimya kimya halafu baadae aje aseme ''walipiga kelele kuwa nchi imeuzwa, mbona haijauzwa''?
Waarabu wamemshika pabaya!! Hawana adabu wale!! Lazima watamwaibisha!!
 
mtu yeyote yule mwenye akili timamu lazima awe na emotional inteligence......mama samia huwezi kumlinganisha na baba jesca

..Ni kweli Mama'ake Abduli ni tofaute na Baba Jesca.

..lakini kutoku-act muda wote huu, na kupelekea kuwepo kwa mifarakano ktk jamii, kunaashiria kwamba huyu Mama hana uwezo wa kufanya maamuzi kunapotokea matatizo.

..kama sio hivyo basi atakuwa hajali kwa hayo yanayoendelea.

..kama tatizo limejitokeza halafu KIONGOZI hatoi ufafanuzi, na zaidi hachukui hatua kutatua tatizo, kwangu mimi hiyo sio emotional intelligence.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ