Ujenzi wa JNHPP na Usambazaji wa umeme Rais Samia aongeza bajeti kwa 230% kutoka TZS 1.01T FY2020|22 hadi TZS 2.34T FY2021|22 mnaoshangaa endeleeni kushangaa,
" Hakuna kama Samia "
Lengo la Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ifikapo mwaka 2026 Tanzania iwe na umeme wa Uhakika unaofikia Jumla ya 5,000MW hapa anamaanisha tunakwenda kuwa electricity donor country hakika Watanzania kesho yetu ni bora sana kuliko leo,
Sote tunafahamu mahitaji ya Umeme Tanzania yanaongezeka siku hata siku kwa mfano mwaka 2020 mahitaji ya Umeme yalikuwa 1,151.66MW lakini hadi kufikia mwezi May 2021 mahitaji ya Umeme yalifikia 1,183.28MW sawa na ongezeko la 3% kwa mwaka. Lakini pia, kwa mwaka huku umeme wetu umetajwa kuwa ndio umeme wenye bei chee zaidi African ya Mashariki kwani tunauuza kwa $0.099/KWh,Kwahakika Tanzania ya Rais Samia ni raha sana natutegemee bei hii kushuka zaidi baada ya JNHPP kukamilika,
Faida ya mradi huu sio umeme tu kwani tayari mradi huu pia umeajiri Jumla ya wafanyakazi 7,243 huku wazawa wakiwa ni 6,452 na wageni ni 791,Mradi huu utakapokamilika unatarajiwa kuzalisha Jumla ya MW 2,115 kamwe tusiache kumwomba Mungu,
Mpaka Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani ni 38% tu ya fedha zote za mradi huu wa Tshs 6.55trilioni ndio zilikuwa zimelipwa kwa mkandarasi ambayo jumla yake ni Tshs 2.495trilioni sawa na Pungufu ya Tshs 4.055trilioni, Hii ni sawa na kusema Rais Samia Suluhu Hassan hadi mwisho wa mradi huu atakuwa ameujenga mradi kwa 62%,Hakika Mama huyu anastahili pongezi sana kwa kiwango hiki cha kizalendo kwa nchi yake,
Zikiwa zimesalia miezi kumi ( 10 ) tu kumalizika kwa mkataba huu Rais Samia Suluhu Hassan kupitia bajeti yake hii ya kwanza tayari ameshatenga 58% ya deni lote lililosalia kwani ametoa Tshs 2.34trilioni kwaajili ya usambazaji wa umeme na ukamilishaji wa mradi huu wa JNHPP,Pesa hii ni sawa na pesa yote iliyotolewa tangu kuanza kwa mradi huu wa JNHPP,Unaweza kusema "Bajeti moja ya Rais Samia kwenye usambazaji wa umeme na ujenzi wa JNHPP ni sawa na bajeti zote zilizotolewa kujenga JNHPP tangu ianze May 2019 " Watanzania,Kama kuna mtu wa kuombewa kwa nguvu kubwa kwa sasa basi ni Rais Samia Suluhu Hassan