According to National Bureau of Statistics (NBS) Pato la Tanzania
(Tanzania Gross Domestic Product GDP ) limekua kwa kasi ya ajabu na kufikia 5.2% robo ya tatu ya mwaka kutoka 4.1% robo ya kwanza wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani 19|03|2021 takribani miezi tisa sasa,
Kwa lughal rahisi tunaweza kusema Rais Samia Suluhu Hassan kwa miezi hii michache amekuza Pato la nchi nzima kwa ukuaji "Chanya" wa Uchumi wa 5.2% wakati huu huu ambapo majirani zetu wakishuhudia ukuaji "Hasi " wa Uchumi wao,
Mtakumbuka,hali ilikuwa mbaya zaidi mwaka 2019 pale ambapo AfDB waliikadiria Tanzania Pato lake kushuka kutoka wastani wa ukuaji wa 7% hadi ukuaji wa 2.1% mwaka 2019|2020 na sababu ikiwa ni Covid 19,
Wakati huohuo baadhi ya nchi za Africa Mashariki walishuhudia ukuaji hasi wa Uchumi mathalani Rwanda ilirekodi ukuaji hasi wa -3.6% huku Kenya wakishuhudia ukuaji hasi wa -2.1% robo ya pili ya mwaka 2021 wakati Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tulirekodi ukuaji Chanja wa 4.4%
Kuimarika kwa kasi kwa Utalii na uwekezaji mkubwa toka nje na kilimo vimetajwa kuwa ni sababu za kukua kwa kasi kwa Uchumi wa Tanzania hasa katika robo ya tatu ya mwaka 2021 uliofikia TZS 32 trilioni kutoka TZS 30.3 trilioni katika robo ya tatu ya mwaka 2020.
Katika robo ya tatu ( Q3 ) mwaka 2020 Tanzania ilipokea Jumla ya Watalii 72,147 pekee wakati katika kipindi kama hicho mwaka 2021 Tanzania imepokea Jumla ya Watalii 243,565 sawa na ongezeko la Watalii 171,418 ambao ni sawa na 338%
Utalii katika robo hii ya tatu ( Q3 ) umechangia 18.1% kwenye Uchumi wa Taifa na hii inachagizwa zaidi utengenezaji wa "Royal Tour Film " itakayozinduliwa rasmi 22|04|2022 huku kilimo kikichangia 15.1%
VIVA TANZANIA VIVA || VIVA SAMIA VIVA