Rais Samia Suluhu ataka nafasi 6,000 za walimu kujazwa

Rais Samia Suluhu ataka nafasi 6,000 za walimu kujazwa

Ni nafasi za zilizoachwa na Walimu waliostaafu,walioacha kazi Serikalini na waliofariki.

Rais Samia Suluhu amesema haya....

Natambua kuna Walimu wengi tu karibu Elfu 6 au zaidi ambao wamestaafu, wamefariki n.k na kunahitajika wa kuziba nafasi hawa sio ajira mpya ni wa kuziba nafasi, Utumishi mko hapa na TAMISEMI mkalisimamie, Walimu Elfu 6 warudishwe haraka ili wakawatumikie Watanzania

Jiwe alikuwa na roho mbaya sana ,yaani hakujaza nafasi zilizo wazi kabisa.
 
Ni nafasi za zilizoachwa na Walimu waliostaafu,walioacha kazi Serikalini na waliofariki.

Rais Samia Suluhu amesema haya....

Natambua kuna Walimu wengi tu karibu Elfu 6 au zaidi ambao wamestaafu, wamefariki n.k na kunahitajika wa kuziba nafasi hawa sio ajira mpya ni wa kuziba nafasi, Utumishi mko hapa na TAMISEMI mkalisimamie, Walimu Elfu 6 warudishwe haraka ili wakawatumikie Watanzania

Kwahiyo anaajiri tuliyo mtaani? Ama nini
 
Mchakato huo wa ajira utagubikwa na rushwa sio ya nchi hii... Ila muhimu ni wote wapate hio nafasi
 
Safi sana mama, ajiri watu wengi, hiyo ni baraka.

Mtawala mwenye mkono wa birika hawezi kukumbukwa kwa mabarabara pekee, bali kwa kila kazi njema aifanyayo
 
Kwahiyo anaajiri tuliyo mtaani? Ama nini
Hapa mama alimaanisha kuna mapungufu ya nafasi elfu sita za walimu zinazotakiwa zijazwe. Hao watakaozijaza ni wale walio mtaani na wasio na ajira. Ila sio ajira mpya kwa kuwa haziendi kuongeza idadi ya walimu waliopo bali kuziba mapengo yaliyopo. Ajira mpya ni zile zinazoenda kuongeza idadi ya watumishi waliopo. Ila kwa atakaye ajiriwa, yeye kwake itakuwa ajira mpya.
 
Leo rais Samia ametangaza serikali iajiri walimu 6000 ili kuziba mapengo ya wale waliostaafu, kuacha kazi na kufa, ni jambo zuri na heri kwa vijana wenye taaluma ya ualimu.
Wito wangu kwa serikali ili kujenga uzalendo serikali iajiri walimu waliopo mashuleni wanaojitolea maana hawa ni wazalendo hasa, wapo walimu wanaojitolea bure bila malipo na wengine kwa pesa kidogo sana ya chakula.
Endapo serikali itawaajiri walimu hii itajenga uzalendo na moyo wa kujitolea, isitoshe hawa ndio walionesha utayari na kuwa shida ya kazi.
Namna nzuri ya kuwapata ili kuondoa uwezekano wa wengine kuchomeka ndugu zao timu maalumu iundwe ipite shule moja ikague madaktari ya kusaini mahudhurio ya walimu na class journals zote na kuuliza wanafunzi kama Kuna walimu wanajitolea kwenye shule na endapo wanawaambia kwa sura na wana muda gani hii itaondoa udanganyifu na kuajiri wahusika.
 
Iko wazi waajiriwe walimu elfu6 kuziba yale matundu ya walimu waliostaafu na wengine kufariki ili ibalance kwa idadi iliyokuweko kabla.
 
Back
Top Bottom