Rais Samia Suluhu ataka nafasi 6,000 za walimu kujazwa

Rais Samia Suluhu ataka nafasi 6,000 za walimu kujazwa

Ajira mpya ina maana kama watumishi wapo 200,000 serikali inaamua kuajiri watu wengine 30,000 ili iwe na watumishi 230,000 hapo kuna ajira mpya 30,000

Sasa replacement(kuziba nafasi) ni kama mwisho wakuajiri serikali ilikuwa na watumishi 200,000 mwaka 2016 ila hadi 2021 wakafariki 30,000 ina maan serikali inakuwa na watumishi 170,000 sasa ikitaka kurudisha watumishiwafike tena 200,000 ndio inatangaza iyo replacement ya 30,000

Hii ni kujazia wale waliofariki.

Watumishi ni wapya ila ajira siyo mpya.
 
Siyo ajira mpya..
Ni ajira mpya mzee wangu. Inawezekana kiswahili tu kinazingua.

Any way, yote yatasemwa lakini la msingi ni mwalimu asiye na ajira leo hii na yupo mtaani ataingia katika soko la ajira na kutumikia taaluma yake. Hapo ni akina mama kwa akina baba wasipata hata senti tano baada ya kuhitimu elimu yao watapumua.

Habari hii ni sherehe kwa wengi- kwanza kabisa ni kwa wanafunzi wasiokuwa na waalimu hivi punde watapata walimu wa Fizikia, bailojia, kemia na hisabati.

Hongera Mama Samia aka Mama RUKSA. Mama mi 5 tena.
 
Huo mfumo haupo katika suala la kuajiri, wewe kama ulijitolea ni kwa mapenzi yako.
 
Toka ajira za walimu ziwe za kusuasua, TAMISEMI wamekuwa wakikanganya jamii sana kwa kuwa hawaeleeki ni vigezo gani wanatumia kuchagua walimu wakati wa udahili.

Sasa tunaomba waweke wazi vigezo vya kudahili kama ni;
Umri wa mwalimu,
Jinsia,
Ufaulu(G.P.A)
Idadi ya masomo aliyosomea mwalimu(2 vs 1),
Aina ya masomo(Arts vs sciences)
N.k.


Kuna mambo yamekuwa yakijitokeza katika ajira za walimu ambayo yanaleta maswali mengi sana.

Mfano mwalimu aliehitimu chuo mwaka 2015 anaachwa na anachaguliwa mwalimu aliyemaliza mwaka 2018,kwa masomo yaleyale.

Mwalimu mwenye masomo mawili ya kufundishia anaachwa anachukuliwa mwenye somo moja.Na mambo mengine kama hayo.

Basi tunaomba muweke vigezo hadharani ili watanzania tujue na ili kupunguza chuki miongoni mwa walimu(wahitimu) wenyewe.
 
Mheshimiwa Rais ametoa agizo hilo leo 6 apr,2021 alipokuwa akiwaapisha viongozi mbali mbali ikulu, dar es salaam.

Ambapo amezitaka wizara ya utumishi pamoja na tamisemi kuandaa utaratibu wa kuajiri walimu 6000 ili kufidia nafasi za wazi kutokana na baadhi ya walimu kustaafu, kuacha kazi, kufukuzwa, kufariki au matatizo mbali mbali.

Chini hapa ni video fupi wakati anatoa agizo hilo mbele ya mawaziri na viongozi mbali mbali


Kufuatia agizo hilo kwa kipekee nampongeza mheshimiwa Rais kwani ameonyesha dhamira ya kutatua kero na matatizo ya wananchi kwa wakati kwani ni siku chache tu tangu niandike andiko langu kufikisha kilio cha upungufu wa walimu ambapo kilio hicho kimepatiwa majibu siku ya leo.

Zaidi soma hapa,

Thread 'Dkt. John Magufuli amekufa na deni letu, Rais Samia tunaomba suluhu yako' Dkt. John Magufuli amekufa na deni letu, Rais Samia tunaomba suluhu yako
 
Ni nafasi za zilizoachwa na Walimu waliostaafu,walioacha kazi Serikalini na waliofariki.

Rais Samia Suluhu amesema haya....

Natambua kuna Walimu wengi tu karibu Elfu 6 au zaidi ambao wamestaafu, wamefariki n.k na kunahitajika wa kuziba nafasi hawa sio ajira mpya ni wa kuziba nafasi, Utumishi mko hapa na TAMISEMI mkalisimamie, Walimu Elfu 6 warudishwe haraka ili wakawatumikie Watanzania

Haya walimu mambo ni fire...
 
unajua maana ya kuwaza nje ya boksi? kwa mujibu wa wanasiasa watanzania ni kupitisha mrungula upate kazi.
 
Ni nafasi za zilizoachwa na Walimu waliostaafu,walioacha kazi Serikalini na waliofariki.

Rais Samia Suluhu amesema haya....

Natambua kuna Walimu wengi tu karibu Elfu 6 au zaidi ambao wamestaafu, wamefariki n.k na kunahitajika wa kuziba nafasi hawa sio ajira mpya ni wa kuziba nafasi, Utumishi mko hapa na TAMISEMI mkalisimamie, Walimu Elfu 6 warudishwe haraka ili wakawatumikie Watanzania

Iron lady the ERASOR
 
Sijui ni ujinga au makusudi, yeye mwenyewe kasema sio ajira mpya
Kiswahili kwa marais wetu ni shida. Alikuwa Nyerere peke yake ndo aliongea kiswahili fasaha. Wengine wanachanganya na lugha zao za asili.
 
We kweli shibobo "Kasema wale walioachishwa na waliostafishwa warudishwe kwenye ajira zao.
rudia kusoma ulichoandika na alichokisema Rais...


waliofariki unarudishaje kazini🤓
 
Back
Top Bottom