Rais Samia Suluhu ateua Wabunge wapya watatu na kuteua Baraza la Mawaziri

Rais Samia Suluhu ateua Wabunge wapya watatu na kuteua Baraza la Mawaziri

Hongera sana kwa kuweka wazi uongozi utakaoenda nao katika awamu hii ya 6, Baraza ni zuri sana, ila pia ulisema kua Wanapigiana sana vikumbo kwenye kazi zao, na bifu linaanzia kwenye majukumu yao, Mungu saidia Tanzania ikawe stawi ya Taifa pendwa, Makamu Mpango safi sana, Mwigulu ni mzuri sana maana hata wakati Mpango hayupo Aliyekua anasaidia kunibu maswali ni Mwigulu, na aliimudu, Nmeona ametoka Naibu waziri wa Afya na wengine, awe mtulivu tu, maana heshima ni kutulia.

Lakini nlitamani uwaambie mawaziri wengine, wanaangalia sehemu za kwenda kutembelea, vijijini hawaji kabisaaaaaa.
Asante sana
 
Watanzania ujuaji umezidi, tumuache mama apange kikosi anachoona kitamsaidia kusukuma mashambulizi. Tumpe muda na imani please.
 
Zingekuwa kweli asingepewa ubunge. Uwe na akili
Usidhani kila jino bovu hung'olewa Mkuu mengine huachwa yavunjike yenyewe "ndio akili" jino jingine ukitumia maguvu linakuchomoa nafsi... kutoka Katibu Kiongozi hadi..... aaaah tusitaniane hivi kwani waziri na katibu kiongozi nani ni...
 
Baraza jipya? Wenzetu huwa mna ubongo kweli?
Amefanya mabadiliko kidogo, Ila Baraza ni lile lile
 
Kule mambo ya Nje Kabudi alikupenda sana

Namuona kama hakufurahia hizi teuzi. Uso wake ulikuwa tofauti leo. Kweli mambo yamewabadilikia watu fulani fulani ghafla sana. Na speaker nae nilimuona hana raha kabisaa.
 
Hongera sana.

Binafsi nimefurahishwa sana na safu aliyo ipanga. kila mtu kakaa ktk sehemu kulingana na taaluma/ujuzi na uzoefu wake, kwa maaana hiyo tunategemea kila waziri atafanya kazi anayo ijua vyema zaidi, hatutegemei kuona uzembe.

sisi wananchi tunataka kuona matokeo yaliyo kusudiwa ambayo ni kutuletea maendeleo.
 
Mwigulu hiyo nafasi inamfaa sana, ingawa mimi si shabiki wake, kazi iliyopo kwa siku 100 za kwanza ni kurejesha pesa iliyokwapuliwa na iliyofichwa na watu wasio waaminifu, Mpango anampa Mwigulu majina ya hao wezi na Mwigulu anairejesha hiyo fedha, ni mzuri sana akielekezwa nini cha kufanya anafanya kwa ufanisi sana tatizo ni yeye kufanya maamuzi kama yeye! Atasafisha uozo pale Fedha kila mtu atafurahi. Mpeni muda kidogo muone!

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
Haya majizi haya! Mungu asaidie pesa zipatikane na wao wafukuzwe kabisa ikiwezekana yafunguliwe kesi yakafie hata gerezani.
 
Nani Waziri wa kazi na ajira anaitwa nani?!
 
Back
Top Bottom