Rais Samia Suluhu Hassan ampa onyo Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo

Miradi ya ujenzi wa majengo ya shule na afya kwa mfano kwa nini wasifanye TBA? Kitengo cha uhandisi kule kitoke kiende TBA
TBA ni watendaji sio wasimamizi
Kumbuka pia TBA wali laumiwa ktk miradi kadhaa utendaji mbovu mfano majengo ya makazi ya askari magereza kula Gongo la mboto sijui
 
Fikiria wewe ni waziri, unatumia njia gani kuwatumbua wateule pendwa wa boss wako.
Shida ni aina ya taasis ya watu anaowaongoza. Wengi walikua walioshindwa katika chaguzi, walipoteuliwa wakaona nao ni marais.
Ujumbe wa onyo ni kutoa wasaidizi/wateule wasiosaidia ustawi wa maeneo yao. Tupo zaidi ya 60mill. Viongozi wenye akili wapo tu.
Mh Jaffo fanya sasa. Ondoa mamluki wote. Tanzania itakukumbuka
 
Hatujui mengi yaliyokua yanaendelea ndani combination (hayati na mama) ila kwa tafsir ya haraka haraka hiki kinachofanyika ni kua kipndi Cha hayati maamuzi yalikua yanatolewa na mtu mmoja tu na mawazo ya mama hayapewi nafasi,ila kwa jicho lingine hotuba ya mama leo inatoa kengele kwa watu wafuatao wajiandae kisaikolojia jafo,waziri mkuu, na Yule wa azina waliochota mapesa kipind cha hayati akiwa mgonjwa
 

Wewe nae povu kama lote bila mpango,hii report imeandaliwa chini ya JPM hadi umauti wake ilishakamilika,kwa hiyo kwakuwa imesomwa mbele ya Samia ndiyo unambagaza JPM? Kwa akili zenu hizi acha CCM itutawale Milele na Milele.
 
Mama yangu wee wakusaidiwa wapo wengi sana humo ndani [emoji17][emoji17][emoji17]
 
Nikweli hata uchaguzi waserikali zamitaa pesa zilitumika sana bila sababu akijua uchaguzi haupo 2019.shame
 
Hivi back in days Tamisemi si ilikuwa chini ya Ofisi ya Waziri mkuu?
 
Praise and Worship gang walishasema Jaffo ni Rais wa JMT anayesubiri muda tu. Leo tena hafai, jamani!!!

Kumbe manyani ni sahihi kushangilia bila kuhofia kufa make kama njaa imetupiga miaka 5 bila kufa sembuse hii miaka 4 iliyobakia ya awamu 5.

Mna miaka 100 ijayo ya kutawaliwa na CCM,hilo likukae kichwani.
 
Jafo wanamuonea tu,wakurugenzi wengi wameingia kwa kiki za uanachama wa kijani pia ni vilaza mno hawawezi kusimamia pesa za serikali.Aanzia kwa hao DED ndo shida zipo
Mkuu usitetee madudu. Ma DED unaosema wapo chini yake, kama ndio wana mkwamisha yeye kama waziri amechukua hatua gani?
 
Sijapenda L
ugha yako, haina staha wala ukomavu japo hoja yako ni murua kabisa. Tatizo la TAMISEMI Hayati Magufuli alilisema sana na katika uongozi wake zaidi ya 82% ya upigaji umeondoka. Bado hizi chache, na Rais wa sasa anatakiwa akaze buti, uzuri walikuwa wote na Rais Magufuli. TAMISEMI haina kikomo kupambana. Sijaona mheshimiwa Rais akiwatoa Wakurugenzi, lakini nina imani atawanyofoa baadhi kama Mtangulizi wake Hayati JPM alivyokuwa anafanya. Na hii report angeipokea JPM (Kama angekuwa hai, yawezekana Jafo angeondoka leo) japo simuombei aondoke. TAMISEMI pagumu sana. Watu wengi kule wanafanya kazi kwa mazoea na hawajali. Kingine Muhimu tusome report ya CAG
 
Katibu Mkuu wa Tanisemi ndio Mtendaji Mkuu Engineer Nyamhanga
Kiukweli waziri wa tamisemi inafaa awe engineer wa kusomea kabisa maana ujenzi ni mwingi tizama mbezi stand BOQ ikasukwa kupigwa bil 15 sasa wamepiga ngapi nani anajua?? huyu bitozi masuti itamtesa apewe kawizara ka mazingira na usafi
 
Dogo mmeshikwa pabaya
 
Tamisemi Kuna uozo mwingi Sana. Fedha za ujenzi wa miradi zinapigwa, hakuna anayejua. Mfano, serikali ilitoa Bil 1.8 kwa ajili ya kujenga Hospitali za wilaya, mpaka Leo sidhani Kama Kuna hospitali hata moja imekamilika. Mawaziri wanakaa ofisini kusubiri ripoti za ujenzi toka kwa Wakurugenz, ripoti zinapikwa na maisha yanaendelea. Mawaziri hata wakija, wanaishia kwenye kumbi za Halmashaur hawafiki site kujionea. Hapa ndipo Hayati JPM enzi za uwaziri wake alipokuwa anawafunika mawaziri wenzake. Miradi mingi ya maji, Shule iko hoi na serikali imeshatoa pesa. Kuna mchwa kuanzia kwenye vitengo vya manunuzi, mhandisi,wakaguzi wa ndani, Fedha na Idara husika.
Ningeshauri mamlaka za Uteuzi kuliangalia upya suala la Wakurugenz. Wabadilishwe, hawa wa Sasa wengi wamechoka Sasa wanaongoza kwa mazoea.
Pia, Kama wizara ya afya ilivyounda timu maalum ya ukaguzi iliyopita kwenye hospitali zote za rufaa za mikoa nchini( na kweli waligundua madudu mengi), TAMISEMI nao waunde kikosi kazi maalumu kipite kila ulipo mradi wa serikali wakague kila Senti ya serikali ilivyotumika. Naamini wataujua ukweli na huo ndio uwe mwanzo mpya.
 
Report ya CAG sisi wananchi wa kawaida tunaipata wapi?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Rais amteue bwana Tickson Nzunda kuwa katibu mkuu Tamisemi maana aliwabana Sana wapigaji akiwa Naibu anaeshughulikia elimu ,atamsaidia.

Pia wazari Jafo kama anaona kuna watu chini yake hawafanyi vizuri si awaseme kwa boss mama wapigwe chini?
Tickson nzunda alifanya kazi yake kwa weledi na alikuwa na maono makubwa ya kuboresha elimu yetu lakini jiwe hakupenda hicho kitu ndio maana akamuondoa kwenye unaibu katibu na kisa cha kuondolewa kwake ni pale Nzunda alipotaka kuajiri walimu wenye digrii kufundisha primary, jiwe akaona anaingizwa kwenye bajeti kubwa ya mishahara akamuondoa
 
Mkuu usitetee madudu. Ma DED unaosema wapo chini yake, kama ndio wana mkwamisha yeye kama waziri amechukua hatua gani?
Wewe unadhani waziri atawachukulia hatua gani maDED? Yeye sio mamlaka ya uteuzi au utenguzi wao, hiyo mamlaka anayo Rais. Jafo hawezi hata kuwaweka ndani siku moja mbili. Hiyo mamlaka wamepewa wakuu wa mikoa. Rejea alivyokuwa analalamika akiwa geita juu ya wale maafisa ardhi na mkurugenzi waliofanya madudu. Ni Mongela RC wa mwanza ndio alikuja kusema hiyo mamlaka yeye anayo na akawaweka ndani.yeye Jafo sana sana atakachoweza kufanya ni kuwabwekea tu na kuwashitaki kwa mamlaka iliyowateua, si zaidi ya hapo. lazima wamvimbie na kumpuuza.
Ana wakati mgumu sana!
 
Jifunze matumizi ya "r" na "l" unaharibu lugha yetu.
 
Angemtumbua yule mjinga maana anatuingiza hasara tu.
 
Tunashauri ukubwa wa Baraza la mawaziri upunguzwe wewe ndo kwanza unataka wizara moja iwe na mwaziri sita! Labda nawe NI mnufaika wa hizo teuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…