Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Alijipa awamu ya sita ili kujitenga na utawala wa jembe magufuli, pia ili ionekane kwamba yupo kwenye muhula wa kwanza wakati kimsingi ni muhula wake wa pili, ukichukulia kwamba walijinadi kwa pamoja na JPM mwaka 2015....
 
Awamu zinahesabika kwa vichwa vya marais so as to document legacy correctly! Hata akikaa mwezi, AWAMU IMEISHA NA LEGACY YAKE TAYARI, HUWEZI KUIUNGANISHA NA YA RAIS MWINGINE.
Wazee wa legacy wanataka kulazimisha agenda zao🤔.
 
Mi najua awamu ya Urais ni miaka mitano. So hapa tutakuwa tupo awamu sijui ya ngapi, mi tano ya Magu awamu moja, Kikwete 2, Mkapa 2, Mwinyi 2. Nyerere alipigiwa kura mara ngapi? Kama ni kila miaka mitano basi alitawala karibi awamu tano. So tupo awamu ya ngapi?

Hii tupo awamu ya 13.
 
Je, serikali ya kikoloni ilikuwa ni awamu ya ngapi?

Hivi vitu viwe defined na kutambulkka kisheria.
Tukiwaambia katiba mpya wanafinya finya pua na midomo. Kwa hii iliyopo wanakaribia hata kushindwa kutambua kama ni usiku au mchana, bado wanaing'ang'ania tuu.
 
Nchi inaenda hovyo hovyo tu.
 
Msomi Joseph Magata akufafanua vizuri wewe ndiye hukusoma akichoandika.


Hiki hapa ukisome



 
Dah hii nchi hii!

Kwa hio wewe umesoma alichoandika na kweli ukaelewa kwamba Rais Samia ni wa awamu ya 6?

Hebu soma haya maneno aliyoyaandika!

.....
Sasa tuirejee ibara ya 51(2) inayosema rais "akishashika madaraka" atateua waziri mkuu. Je, Rais Samia alishika lini madaraka ya urais? Mfumo wa urithi tuliouona na pia katiba yetu vinajibu swali hili kama ifuatavyo.

Moja, makamu wa rais ni mrithi kama "prince" na "princess", hivyo, si tu madaraka aliyarithi sekunde ya kifo cha Rais Magufuli, bali pia hakulazimika kuapishwa.

Mbili, kwa kuwa anapofanya "kazi zote" za rais ibara ya 47(1)(c) ya katiba haimuhitaji aapishwe, ndivyo pia haikumuhitaji aapishwe sekunde Rais Magufuli alipokosekana kazini kwa kufariki.

Kiapo alichoapa Rais Samia hakikuongeza jukumu jipya nje ya aliyoyapata sekunde ile aliyofariki Rais Magufuli. Hivyo Samia Suluhu ameanza urais tangu sekunde aliyofariki Rais Magufuli.

Hata inapotokea anapishwa, japo si lazima....

Jisomee hayo maneno yake!
 
Mkuu hapa bongo bora liende ,Samia ni rais wa awamu ya tano ,watake wasitake
 
Awamu zinahesabika kwa vichwa vya marais so as to document legacy correctly! Hata akikaa mwezi, AWAMU IMEISHA NA LEGACY YAKE TAYARI, HUWEZI KUIUNGANISHA NA YA RAIS MWINGINE.
Maelezo yameshiba halafu unapotosha waziwazi ,nchi hii?,tuna viazi kweli
 
Mkuu mbona haya mambo hata hayahitaji usomi wowote?

Mwalimu alitawala zaidi ya miaka 10, inahesabiwa awamu 1.
Mwinyi akaingia mihula miwili, hatukuambiwa awamu ya pili na ya tatu japo tulishuhudia chaguzi mbili.

Mkapa mihula miwili hiyo ikawa ni awamu ya tatu.

Kikwete akaingia awamu ya nne akiongoza kwa mihula miwili pia.

JPM amekua wa awamu ya tano aliyoitumikia mhula mmoja kamili na awamu ya pili miezi michache.
Kwa utaratibu huo, awamu inahesabiwa kwa anayeshika usukani.

Kama ni vigezo ulivyovitoa vya vhaguzi na kuunda serikali basi Mwinyi angekua na awamu ya pili na ya tatu, Mkapa hali kadhalika angepojea awamu ya nne na ya tato. Kumbuka hao wote waliunda serikali mara mbili na kushinda chaguzi mihula miwili.
 
Sijasema Samia ni wa awamu ya 6. Niliposoma hii makala nikajua awamu ya 5 inaendelea na Samia hakuhitaji kiapo.

Ninapoga kauli yako kwamba wasomi hawaja analyse hili


 
Mkuu hapa bongo bora liende ,Samia ni rais wa awamu ya tano ,watake wasitake
Mwinyi alitawala mihula mingapi na alihesabiwa kuwa Rais wa awamu ya ngapi?

Rejea vigezo vya mtoa mada anavyohesabu awamu na uone anavyojichanganya.
 
... yote yameshajadiliwa humu; hii ni Awamu ya Sita vs Awamu ya Tano na kinyume chake! Pamekuwa na two strong schools of thought na hakuna upande unaokubali kushindwa! To make it simple, Samia ni Rais wa Sita; that simple! Ondoa takataka inaoitwa awamu sijui hata ipo kwa sheria ipi!
 
Awamu ya urais ni package (Kuomba kura ukiwa na makamu wako + Kuunda Bunge Jipya + Kuteua Waziri Mkuu mpya + Kuteua speaker qa Bunge mpya) na kuendelea!

Haya ni maoni yako au ukweli? Kama ni kweli tupe chanzo; kama ni maoni yako tueleze ni kwa nini unatuona siye wote wajinga kiasi cha kukosa maoni na kwa sababu hiyo tukubaliane na maoni yako!
 
Ni aibu kubwa kwake ndg.Polepole...

Ukatibu wake mwenezi haukumpa elimu ya kujua kuwa AWAMU inahesabiwa kwa KICHWA ofisini?!!!!

Aibu kubwa kwa MROPOKAJI HUYU....

SIEMPRE CCM🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…